Hakuna maisha ninayoyachukia hapa duniani kama maisha ya kulelewa

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Habarini wakuu,
Nipo hapa kwenye moja ya Bar maarufu sana hapa Sinza. Naona tu kijana anapitishiwa pesa kwenye mapaja ili ampatie mhudumu huku akimtolea bezi mdada wa watu na kumlahumu kuwa haleti huduma kwa wakati

Au maisha yenu na shangazi zenu wa mchongo yamekuwa updated?

Japo sidhani, lakini scenario kama hiyo nimewahi pitia pia. Maisha yale yalikuwa matamu kwa miezi saba tu ya mwanzo, maake alifikia hatua ya kunipangishia mpaka chumba na kunipatia vitu vyote vya ndani. Alinitongoza mwenyewe akiwa amelewa, alitokea kunipenda baada tu ya kushirikiana naye tendo. Miezi yote hiyo, kazi yangu ilikuwa ni kusukuma ukuni, kisha kunyoosha miguu tu magetoni, at any time t, mshiko uliingia

Baada ya hapo aliniomba nihamie kwake kabisaaa. Sasa hapo ndipo nilipoyachukia maisha ya kulelewa. Maake niliishi maisha ya nje (Kwenye jamii) ambapo mimi ndiye niliyekuwa kibesi, pia maisha ya ndani (ambapo yeye ndiye aliyekuwa mwenye mamlaka)

Kilichofuata ni hakuna kutoka ndani pasi na ruhusa maalumu ama bila kuongozana naye. Baada ya hapo nilijikuta nikideki nyumba, kupika, kufua na kuosha vyombo kwenye nyumba ile. Tuliishi wawili tu, maana yake akiwa hayupo, utakaa mwenyewe humo ndani. Kilichofuata niligeuka bwana massage at any time inapombidi, mbandika kucha na mpaka rangi kucha, msugua magaga n.k Kilichofuatia alitaka niwe kwenye muonekano ambao yeye aliupenda. Nilikuwa ni mtu wa kuvaa kiheshima sana, baada ya hapo niliforciwa kusukwa dred, tena ghali (180k kila mwezi), kuvaa vichupa ama pensi za jinzi, raba za blue ama nyeupe, soksi ndefu, earphones nyeupe, na muda wote alipendelea nitembee huku nimeshikilia tablet langu mkononi. Vibao (Chapati) hivyo ni vya kawaida tu kwa makosa madogo madogo, si mnajua tena haya maisha ya ndoa yana mitihani yake?

Kilichonochosha akili ni pale alipoanza tabia ya kuleta masponsa ndani kwake. Hapo litakaa wiki hadi mwezi. Hapo sasa utabadilishwa pozisheni, usije shangaa unaekwa hata mlinzi wa geti ili kuficha uhalisia, na mavazi ya kimasai ukanunuliwa kabisa. Ni mara mia utafutiwe house girl wa muda, kisha wewe ufanywe kuwa mtoto wa dada yake. Mkionekana watatu ndani, hakuna wa kuhisi kirahisi. Yaani masponsa wanaichapa, wakiondoka tu, na wewe utaanza kuichapa kilazima tena mashangazi hayapendagi soksi. Mwisho uungwe kwenye gridi ya taifa

Je, huu ni uungwana?
La Hasha! Huu si Uungwana

Note: Mashangazi, jaribuni kupunguza vikwazo. Sawa serikali imebana pesa kwa vijana. Lakini jitahidini kuishi nasi kiungwana. Tunawaahidi kuwapa kitu roho inapenda tena kwa moyo wetu wote, kwa roho zetu zote, kwa akili yetu yote na kwa nguvu zetu zote

Kama sio Juhudi zako....
Na maisha tungepata wapi

Nachoshukuru, nilimkimbia yule shangazi nikiwa na Tsh. 1.2m ambayo ilinitosha kabisa kuanzisha maisha

Never Forget
 
Duh inanikumbusha kitambo sana nilishi katika mfalme wa mapito, yule mwanamke alikuwa supervisor kazini kwangu, baada ya kuanza mahusiano naye nikawa siendi kazini nashinda kwake yeye ndio anaenda kazini jioni ananikuta naangalia tv. Nampokea kwa mapenzi ya chama na serikali mpaka anamwagamaji.

Usiku napiga tena, asubuhi napiga tena kisha ananiacha na hela ya supu yeye huyo kazini me naamka nakunywa supu narudi kulala, niligeuka kuwa mweupe na mzuri kama ben kinyaiya vile.
 
Habarini wakuu,
Nipo hapa kwenye moja ya Bar maarufu sana hapa Sinza. Naona tu kijana anapitishiwa pesa kwenye mapaja ili ampatie mhudumu huku akimtolea bezi mdada wa watu na kumlahumu kuwa haleti huduma kwa wakati
...
Hatar sana.

Pia hongera kwa kutoka kwneye Hilo shimo.

Ila hapo Kwenye grid ya taifa lazima utakua umeshaungwa
 
Hizi ni story za kutungwa tu mashangazi hawana izo pigo, kwanza wana ubinadamu kushinda hata hawa malaya na kausha damu wa age yetu.
 
Back
Top Bottom