Wakuu Maisha ya Mjini yamenishinda, yaani nikiangalia kipato changu na majukumu niliyonayo naona siwezi kabisa.
Maisha kama haya naona afadhali yale maisha niliishi kwa wazazi wangu enzi za mwalimu pamoja na kuwa babangu alikuwa mkulima lakini tulienda shule na tuliishi maisha mazuri.
Mimi sijui wenzangu mnaishije? mnapata haya machungu nayoyaona mimi? nasimama asubuhi kituoni kwenda kazini naona magari yanapita tu huku mmefunga vioo hivi kweli mna matatizo kama yangu kweli? Hivi nyie pesa mnazipata wapi? mbona najiona mpweke katika nchi yangu hii?
Wakuu siyo siri natafakari kama mambo yakizidi kuwa magumu basi nitafute nauli nirudi kwetu angalau huko nitakuwa na uhakika wa kusogeza siku.
Kipato changu wakuu ni Tshs 542,000/- Nina Mke na mtoto mmoja (5), nimepanga nyumba viwili na sebure - Mambo yamegoma kabisa.
Nipeni ushauri nateketea mtanzania mwenzenu.