Unafikia umri umemtamani mtoto wa kike mrembo 18+ kumwita tu anakusalimia shkamoo babu au shkamoo baba.
Ujue bora akusalimie tu shkamoo
Hapo ujue bado upo
Ila akimalizia tu .
Una hali mbaya. Sitaki uzee aisee ngoja nitafute hela
Hauutaki uzee!
Nadhani una tatizo la kisaikolojia linalohitaji wataalamu kukusaidia.
Ujana unaweza kukudanganya na ukajisahau sana kumbe?
Lakini nikuhakikishie, miaka ishiri ama thelathini iloyoko mbele yako ya kuuanza uzee ni michache sana ni kama dakika thelathini kwenye mzunguko wa saa.
Kama Mungu hajakuua na kubaki hai na afya njema, kuuingia uzee ni kufumba na kufumbua tu.
Kama akili zako umezielekeza kwenye ukiruka njia wa kutongoza wasichana, kweli waweza ukateseka, lakini ni mateso ya kujitakia ya kusaikolojia kwa sababu wasichana warembo ni kama matoleo ya magazeti, ukiishalisoma asiyelisoma atatamani alisome na akishalikulisoma hatalihitaji aendelee nalo, hulitupa pembeni.
'Shikamoo zao' ni kelele za chura zisizoweza kuzuia tembo kunywa maji, nadhani umenielewa.
Nihitimishe kwa kusema usijivunie chochote ambacho binadamu unamiliki sasa hivi: ujana, afya, michongo ya pesa na mali na kupelekea kuwaona wasivyonavyo ni mafala, hapana ni mfumo.
Mshukuru tu Mungu wako kwa kukuwezesha uwe hivyo ulivyo leo, lakini mipango ya kesho yako pamoja na mabadiliko ya chochote kizuri unachokimiliki kuwa virse versi chaweza kukutokea wakati wowote ukae ukijua hilo.