Nina miaka 77 nakwenda 78 Desemba hii na ngoja nikwambie kitu kijana.
Pesa ndiyo ni muhimu sana huku uzeeni lakini cha muhimu zaidi ni afya yako. Ukizubaa ukajiachia ukakamata presha, kisukari, matatizo ya moyo na figo; na mengineyo; kila kitu kinakuwa kimeparaganyika na hizo hela hutazifaidi. Kwanza hata mtambo wako wa nyuklia utakuwa haufanyi kazi tena imagine!
Kijana Linda sana afya yako. Kama ni lazima unywe pombe basi kunywa kwa wastani (tunaambiwa na wataalamu kuwa usizidishe bia mbili kwa siku). Acha sigara maana hazina faida yo yote kwako. Punguza sukari na matumizi ya caffeine (kunywa kahawa na energy drinks kwa kiasi kidogo sana); na angalia sana mlo wako. Fanya vimazoezi karibu kila siku na kamwe usikubali ukanenepeana kama kifutu.
Kama miaka ingekuwa inarudishwa nyuma kwa hakika ningejitahidi sana kulinda afya yangu maana kuna mambo niliyafanya huko ujanani (hasa pombe, nyama choma sana, ulaji wa hovyo kwa ujumla ..) na mpaka leo nalipia gharama zake japo sina presha, kisukari wala matatizo mengine ya kawaida kwa wazee.
Hitimisho: Kijana tafuta pesa. Kula bata lakini kwa tahadhari na priority namba wani kwako iwe ni kulinda sana afya yako maana mambo unayoufanyia mwili wako kwa sasa madhara yake utaanza kuyaona miaka 15+ huko mbele ya safari; na inaweza kuwa ni too late ukajikuta umeshaharibu kila kitu.
[emoji3591][emoji3591][emoji3591] NB: Hata hizi shida zenu za nguvu za kiume vijana wadogo miaka 35 mnafakamia mivayagra kuna mambo ukiyazingatia, hata huku uzeeni utakuwa sawa tu na wala hutahitaji haya madawa yenu. Wewe hakikisha tu cardiovascular system yako iko sawa na mengine yote ni marahisi. Ongeeni na wazee mjifunze [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji870]