Maisha ya Dodoma ni Magumu sana

Ukiacha mkoa wa Arusha, mtu yeyote akija Dodoma ataona kila kitu ghali. Hapa tunawaondoa wale ndugu zetu wa Masaki na maikocheni.

Alihamia rafiki yangu kutoka iringa kila kitu anashangaa, anashangaa kwenda sokoni na laki kununua mahitaji ya wiki kadhaa kwa mtu mwenye familia ndogo, anasema Iringa ningeenda na elfu 30 ningepata mazagazaga yote ya wiki kadhaa.
 
Sasa mkuu na wewe bana.. si umesema ulienda kwa shughuli za kiofisi? Manake umepewa hela ya kujikimu "per diem" kwa siku zote utakazokua huko. Vipi tena unaanza kutafuta gesti za buku tano na wali wa buku? Ukiibiwa laptop huko vichochoroni na ukapoteza nyaraka muhimu za ofisi utasema ulikua wapi? Acha hizo bana hebu lala gesti zenye viwango..!
kabisaaa yaan
 
Azijapangwa muda wote huwa zinabadilika, unaweza angalia saizi bei ukakuta ni kiasi fulani ukiingia baada kama ya dakika kadhaa unakuta imepanda au imeshuka, bei inabadilika mara kwa mara
Ok.Nilidhani ni fixed.
 
Hapana ndege haina fixed price unaweza siku unanunua ticket labda bei ilikuwa laki moja ila kila inavykuwa inajaa viti vinachukuliwa bei inapanda unaweza kujikuta umekaa na mtu yeye kanunua laki wewe laki 3. wanakuwa wanaweka class zikiwa booking nyingi bei inabadilika. Nadhani kama unaona siku za Xmass stand ya ma bus abiria wakiwa wengi demand kubwa watu wanapigwa bei za juu japo serikali huwa inaingilia lakini wapi mtu yuko tayari kutoa pesa asafiri hiyo ndio maana halisi ya demand and supply. Hata hiz hotel kubwa zikiwa vyumba vinachukuliwa haraka na wakiona wateja wengi bei zinapanda kila siku chumba cha pili labda kalipa dola 100 wewe umelipa 200. Demand and supply
Ok.Aisee hiyo Hali lazima imuumize sana mwananchi wa hali ya chini.
 
Ila kuku wa chako Ni chako watamu balaaa na nyama mnadani tamu Sana sijui wanachomaje maana hapa unguja hakuna wachomaji nyama wengi wote wanakaanga kwenye mafuta.
Offcourse nyama zao kule ni tamu ishu ni bei tu.Waliniambia kuwa nyama yenye bei ndogo ni ya Punda tu,ni 5000/=,kwa kilo ukinunua buchani, wakati ya ng'ombe ni 8,000/=kwa buchani.Wanazidiwa na Njombe ambako Ng'ombe ni wachache Sana lkn nyama ni kati ya 6,000/= hadi 7,000/=, Kitimoto ndo kabisaa hadi 5,000/=.
 
Ukifika mji usioujua kwanza uliza wenyeji ili uelekezwe vijiwe vinavofanana na hadhi yako,sio unavamia tu halafu ukipigwa unaanza kulialia,hivyo vijiwe vya bei poa mbona pale Dodoma viko vingi sana...
Vitaje Mkuu ili siku nyingine nisihangaike.
 
Hii ndiyo sababu halisi, ukame pale ndio tatizo.

Watu hawashangai kuwa mpaka leo viwanja na mashamba siyo ghali Dom! Tatizo liko kny misosi tu.

Dom msosi, bidhaa nyingi tu za kawaida na mzunguko wa pesa. Nisijue hali ipoje baada ya mji kukua kwa kasi na serikali kuhamia pale kiasi
 
Back
Top Bottom