Maisha ya Dodoma ni Magumu sana

Maisha ya Dodoma ni Magumu sana

Wakuu hbr za jioni??,Wiki hii Nilikuwa DODOMA kwa shughuli za Kiofisi,nimependa jinsi jiji la Dodoma linavyokua kwa kasi,Lakini hali ya maisha inaonekana ni ngumu Sana kuliko Dar es salaam.

Nilitafuta guest house,bodabo whyda akaniambia kuwa vyumba vya bei ya chini ni 20,000/=,nikashangaa Sana kwasababu niliwahi kwenda DSM na nikafanikiwa kupata gesti ya 10,000/=, nzuri tu.Chakula kwa Dodoma ndo usiseme,kipimo changu cha kwanza ni kwa Mama ntilie, maana watu wengi wa hali ya chini huenda huko kununua chakula;

Aise kina bei hatari [emoji134][emoji134][emoji134], Kuna sehemu niliambiwa wali nyama 3,000/=,Ugali nyama 3000/=,Wali samaki 3500/=, Ugari Maharage 2000/= na wali Maharage 2500/=, Sehemu nyingi za Mama Ntilie bei ni hizo.Nilipolala ni karibu na Holly Cross Center inayomilikiwa b

Na Kanisa Katoliki Jimbo kuu la DODOMA,Aise hapo kitimoto ya kukaanga kilo ni 10,000/=,Ya kubanikwa ni 12,000/=,Ndizi moja 500/=. Ugari kuku robo 6000/=.Na vyakula vingine bei zipo juu pia.Haya nikasema Niulize Vipi kuhusu nyumba za kupanga?;Kheee!!!,Bei nilizotajiwa nilishangaa Sana.Twende Bodaboda aisee Hivi kweli kutoka Holly Cross Center hadi Mkonze mtu anaanza na 6000/=baada ya kuvutana Sana ndo anaishia kwenye 4000/=.

Sijauliza viwanja.Nastaajabu kwasababu miaka ya Nyuma DODOMA haikuwa ghali kiasi hicho.Nilijiuliza swali moja kuwa DODOMA ni wafugaji wazuri wa mifugo sasa Kwanini bei ya Nyama ya ng'ombe ipo juu hivi?? Mnazidiwa na Morogoro ambao hawafugi km ninyi kweli??!!!.

Serikali ichunguze Hali hii, kwasababu inachangia kwa kiasi kikubwa sana Watumishi wa wizara waliokuwa wamehamishiwa DODOMA kutoka Dar kutamani kurudi Dar kuliko kuishi DODOMA.Tafadhari Serikali inusuru Hali hii.
Mbona hujazungumzia machimbo Hali ikoje mkuu?
 
Sasa hapo humaanishi kutafuta pesa may be unazungumzia watu wawe wezi
Tra wengi hawaishi maisha ya uhalisia wa salary slips zao.
Ukwasi wa rafiki yako ukiauangalia vizuri utagundua kuna pesa nyingi nyeusi , ndo mana hana muda wa kulia lia na bei za huduma .
Hahahaha kwamba watu wawe wezi.. mkuu ulipotea sana asee!

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Sasa mkuu na wewe bana.. si umesema ulienda kwa shughuli za kiofisi? Manake umepewa hela ya kujikimu "per diem" kwa siku zote utakazokua huko. Vipi tena unaanza kutafuta gesti za buku tano na wali wa buku? Ukiibiwa laptop huko vichochoroni na ukapoteza nyaraka muhimu za ofisi utasema ulikua wapi? Acha hizo bana hebu lala gesti zenye viwango..!
Sasa Chifu si Nilikuwa nafanya tathmini km Pana faa kuishi watu wa hali ya chini au lah?!!! [emoji23][emoji23]
 
Sio kiasi hicho wote hasa wamama yanatukuta ukigundua mahali bei chini hata Kwa 200 unahama, lakini Kwa kukuriri huku bei jamaa sijui kama huwa anaacha hata punje moja ya Mchele kwenye sahani[emoji125][emoji125][emoji125]
Huwa hawaachi, kwanza ka chakula kenyewe wanako kuwekea kanakuwa kidogo Sana,kwa wale wanaofanya kazi ngumu wanatakiwa kupiga sahani si chini ya mbili.
 
Mkuu labda ungeniambia Hali ya hewa apo Sawa lakin maisha n rahis Sana kule kiwanja kikubwa unaweza pata kwa laki tatu
Weee!!!, Nitajie niende nikanunue nijenge kwaajili ya kupangisha sio kuishi.
 
Hii kiuchumi wakati mwingine ni dalili chanya kwa maana mzunguko wa pesa umekuwa na wanunuzi ni wengi inakuja kwenye demand and supply, kwa maana demand ni kubwa sasa hapa sio issue ya supply sababu wauza bidhaa wangechangamkia fursa. Mara nyingi bei inahukumiwa na uchumi wa watu kumbuka Dodoma watu wameongezeka sana na wanazidi kuongezeka ili inflation iwe controlled ni supply kwenda sawia na demand haya ni mambo ya kawaida siku supply ikiwa kubwa kuliko soko bei zitashuka tu. mfano mdogo hata Dar ukienda high season mwezi wa 6 mpaka wa 8 appartment ya kukodi 100$ kwa siku utalipa 200$ na utafute. Haya mambo ya kawaida sana sababu wazalishaji Tanzania ni walewale wana supply kote issue inakuja je demand and supply viko balance, demand ikiwa kubwa ni dalili nzuri kuwa pesa ipo dawa ongeza supply na supply ikiwa kubwa kuliko soko bei inaanguka inabidi kupunguza supply, kama OPEC tu...
Hali ilivyo DODOMA inatengeneza gap kubwa la kimatabaka kati ya aliye nacho na asiye nacho.
 
Mfano mzuri ndege mnaweza wote kupanda ndege kutoka Dar to Mwanza lakini humo ndani ya ndege kuna watu wamenunua ticket laki kuna wengine laki na nusu na wengine mpaka laki 3 tofauti ni pale umenunua lini ticket na demand ilikuwa vipi supply iko vilevile labda waongeze ndege nyingine na hii ina reflect katika miji yetu unaweza kula Moro kwa alfu moja na chakula hichohicho ukala kwa 2000 Dar.
Kwani kwenye ndege nauli si tayari walishazipanga??.
 
Kuhusu Guest hizo najua zipo hata za buku 5 chafu balaa...shuka jekundu na lingine kaki..yote machafu kinoma noma.

Bafu za nje na taulo lenye uchafu wakutisha....
Kuhusu misosi na nyumba za kupanga naamini nyumba zitashuka bei baada ya miaka miwili maana watu wengi watakua na nyumba hasa watumishi wa umma.
Mhhhh!!!, Sidhani, kwasababu population ya watu inazidi kuongezeka Kwa hiyo demand ya Nyumba na vyakula itazidi kuongezeka.
 
Siomagumu kihivyo, ulikofikia na kupata data hizo n maeneo karibu na chuo, hyo mitaa wamepanga sana wanafunzi wa St. John
Kuna maeneo mengine ambayo ni pembeni na mji lkn bei ni hizo na wakati mwingine zinazidi hizo, mfano nilienda Mkonze,pale supu bila buku mbili hupati, chapati mbili ni 600/=, Wakati chapati mbili kwa town ni jero.
 
Sasa hapo humaanishi kutafuta pesa may be unazungumzia watu wawe wezi
Tra wengi hawaishi maisha ya uhalisia wa salary slips zao.
Ukwasi wa rafiki yako ukiauangalia vizuri utagundua kuna pesa nyingi nyeusi , ndo mana hana muda wa kulia lia na bei za huduma .
Umeona eenhh??!!,TRA Wana njia nyingi za kujipatia pesa kwa njia zisizo halali.
 
Back
Top Bottom