Maisha Plus Tv Show ya Masoud Kipanya


Kama waliwalenga vijana wa vijijini au wale ambao kiwango chao cha elimu hakikuwa kigezo katika usaili huo, nadhani ilikuwa ni makosa kuyahusisha maneno kama IQ au Black box katika huo usaili . Hasa ukizingatia kuwa lugha ya taifa si Kiingereza, na lugha ya kufundishia bado ni ugonjwa wa taifa.
 





Haraka haraka, kuna watu wamegusia mfumo wa elimu na tunakolipeleka taifa! kijana wa sasa ni tofauti sana na vijana wa zamani , tunajua utandawazi unavyodumaza ubongo! kama mwendesha kipindi ana tatizo, na wahusika wana matatizo zaidi, then this is starting point ya kujua taifa liko wapi.

Anyway nampongeza huyu kijana , japo naye anataka shule, he is doing right things though.
 
Big up masoud wa kipanya, wasikudiscourage wala nini. Komaa we just fanya marekebisho. Kuna sehemu za kutolea maoni jamani, kama vile mail ambayo wanadisplay kila kipindi kinapokuwa hewani
 
Me nadhani tukimsifia tutakuwa tunampa kichwa bure ukiangalia hiyo show anaiga karibu kila kitu kutoka big brother, ajaribu kuwa creative na sisi tutamuunga mkono.
 
Me nadhani tukimsifia tutakuwa tunampa kichwa bure ukiangalia hiyo show anaiga karibu kila kitu kutoka big brother, ajaribu kuwa creative na sisi tutamuunga mkono.

Wewe umecreate nini?
 

Ni show ya Masoud imetupa firsa ya kuchanganua hapa. Tunachanganua kuhusu swala la elimu etc and we got this from that show... Hatuwezi kusema ni useless. Ni msingi wa kitu cha msingi na cha muhimu siku zijazo baada ya masahihisho muhimu toka kwa wadau.

Ukiangalia Maisha plus ina ladha ya ki_JKT... which i know it can activate some domant potentials..zinazo dumazwa na utandawazi etc... na ni kweli trough the whole thing tunagundua umakini usiokuwepo kwa masood na vijana wake kwenye swala zima la elimu na integrity.... vimaswali wanavyoulizana ...na Vimajibu.... vinavyotolewa.... na main theme...na ..nini hasa kinatakiwa kuwa achived pale ..kuna namna hakijitokezi vizuri...kimechwa loose ...!! Ni kama panatakiwa mtu meenye qualification zaidi kidogo ku smoothen the program!!

Lakini hakuna sababu ya msingi ya kutokumpongeza kijana wetu...
 
Kusema kweli jamaa anajitaidi sana,Nina uhakika kabisa wote tulikuwa nauhakika kwamba kutakuwa na mapungufu,hasa kwa kuwa tayari tuna reference.

kama katika show ya jana,ilikuwa bomba sana.Kama kweli jamaa walilala na njaa na kushindia ugali na mlenda,itawafanya washiriki waanze kuactivate potential zao ili waweze kuishi.pia jana niligundua kuna kitu tunaweza kujifunza kutoka maisha plus.Cha kufanya ni kumpa moyo na kumuelekeza nini kifanyike kwa mtazamo wako ili show izidi kupendeza.

Kusema ile kweli,mwanzo mzuri tena sana hasa ukizingatia na uwezo wa kiuchumi na kiteknolojia tulionao.
 



Tuwape muda wajameni. Mambo hayawezi kuanza na kuwa bomba muda huo huo. Bila shaka mwakani au next time watafanya improvement
 
Masudi kwa ujumla pamoja na mapungufu kiasi anahitaji pongezi tena sana tuu! ameonyesha ubunifu wake na nadhani pia tunatakiwa kumpa ushauri pale tunapoona amekwenda kombo kidogo! wengi huwa tuko kimya na hata tuna wazo kichwani hatulitoi ila wazo linapotolewa na mtu mwingine ndipo tunatafuta makosa, ni kama mpira ukiwa nje unaona makosa kibao ukiingia wewe unaweza kufanya madudu zaidi ya uliyokuwa unayaona..Kijana anastahili pongezi
nimeangalia kipindi cha jana na kimenipa mvuto mno...natamani jioni ifike nione hatma ya wali walume waliolala njaa
 
Mimi maisha plus imenifunza mengi maisha plus, hasa kipindi cha usaili. Inasikitisha sana, elimu ya vijana wetu sasa ni almost zero. Vijana hawana hata ufahamu wa kawaida tu, yaani kweli kabisa zile tape apelekewe jk aone taifa lake linapoelekea, kama ataweza ajitahidi kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye elimu, hasa shule za serikali ambako watoto wetu wengi wanasoma. Maoni yangu akiboresha mapato ya walimu wake (serikalini) bila shaka tutasonga mbele, otherwise kazi ipo, hatujui taifa lijalo litakuwaje.
 


Heshima mbele mkuu, ila huo uchanganyaji wa lugha ukizidi sana hata maana ya ujumbe wako inapotea, na imani ulilotaka kutueleza ungetumia mojawapo ya hizo lugha mbili ulizozitumia ungeeleweka zaidi.
 
At least kijana anaonyesha ubunifu flani ambao tunatakiwa kumpongeza na kutakiwa kumsaidia kwa mawazo ili aboreshe vizuri.Huu ni mwanzo tu, nakumbuka siku za nyuma watu wengi walikuwa wakiwaponda waigizaji wa filamu za kibongo lakini hivi sasa asilimia kubwa ya watu wanazikubali filam za vijana wetu. (kanumba/ray na wengine wengi).
 

Tunavuna tulichopanda..uvivu wa kujisomea ni matokeo ya ile mikakati tuliyoipa msukumo mkubwa wa vijana kufanya tuition zaidi.
Library ni msaada mkubwa wa vijana kuongeza knowledge lakini hazitumiki ipasavyo sasa hivi. Na hata hizo library zilizopo karibu nchi nzima, mpaka za vyuo vikuu, hazina vitabu vya kutosha au ni zina vitabu vya muda mrefu sana.
Inatisha hii hali ya kuwa wavivu wa kujisomea.Masihala masihala haya, Inaweza kuja muda hapa tukawakaribisha investors wa kuja kutusomea somea vitu vyetu mana wenyewe hatuna muda wa kusoma. Kazi kwelikweli
 
Kwanini mara nyingi huwa tunapenda kukosoa tu miradi inayoanzishwa na wajasiliamali wa kitanzania bila hata kutoa maoni ya namna miradi hiyo ingepaswa kuboreshwa? Hivi ni wivu au ni sababu ya utumwa wa tulionao kwa mambo tunayofikiri mazuri ya nchi za wenzetu walikoendelea?

Tunakosoa show za kwenye TV, tunakosoa Movie za kibongo, tunakosoa wasanii wetu (bongo favouvers), sasa tutaanzia wapi kuendelea? kwani hao walioendelea si walianzia huku tuliko sisi ndugu zangu?

Si vibaya kukosoa, lakini tufanye hivyo na kutoa ushauri namna ya kuboresha ili kuwapa nguvu wajasilimali wetu kuendelea zaidi na zaidi!
 

Mkuu MTM, mimi ni miongoni mwa wafuatiliaji na mdau wa elimu hapa TZ. Pia nimefuatilia Maisha Plus toka kwenye usaili. Hawa unaowaona ndio wamefanya vizuri, yaani ni ndio vipanga walioweza kuvuliwa katika ziwa la vijana wa Tz. Amini usiamini hali ni mbaya sana.

kumbuka showbiz bongo bado hailipi na ni alternative ya walioshindwa mainstream life tofauti na developed world where elimu inaweza kuwa alterantive ya walioshindwa sports and entertainment.

Kuna ukweli ndani yake ila kiwango cha kutoelewa kwa hawa vijana, wengine wakisema wamemaliza kidato cha sita ni cha chini sana. Hii imenigusa sana na ikanikumbusha mtoto mmoja ambaye tulimfanyia tathmini baada ya kumaliza darasa la saba na kukuta uelewa wake ni sawa na darasa la 4. Tulimfundisha kuanzia kiwango hicho na sasa yuko Chuo kikuu. Hawa vijana si wapumbavu bali ni wajinga. Kwa maana hiyo wanaweza kufundishwa wakafanya maajabu!

Jaribu kuangalia debates programs hapohapo TBC kwa watoto wa sekondari wapo wanaojitahidi sana tofauti na maisha plus

Ndugu yangu, vijana ambao wanachapa mjadala kwa pointi za nguvu siku hizi wanahesabika. Hata kwenye hiyo mijadala ya TBC1 ambako naamini wanachua wakali tu bado vijana wanapwaya!
Kwa uelwa wangu, tabia zote za binadamu na viumbe wengine zinatengeneza kitu kinaitwa normal distribution. Kwa hili la elimu, ina maana unakuwa na 75% ya watu wakiwa na upeo mzuri tu (average scores) na 12.5% wakiwa wajinga sana wakati 12.5% nyingine wanakuwa vipanga (super genius). Sasa hapa kwetu inakaribia 60-75% wako hoi. Kama ni mfuatiliaji utakuwa umesikia mfano wa mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja hapa nchini aliyebadilishiwa kozi (yeye alitaka kusoma wildlife management) akaandika barua ambayo ni kituko sana; akisema kuwa hakubaliani na uamuzi wa kuhamishwa kozi kwa sababu malengo yake ni kuwa wild animal (mnyama wa mwitu) akishamaliza shule. Hali kwa hao vijana wengi unaoona ni bora, ambao wako elimu ya juu ni kama ya huyo ndugu yetu anayetamani kuwa wild animal.
 

Hii tabia ni mbaya sana kwa sababu inaua vipaji, kwa sababu watu wengi wanashindwa kujaribu kwa kuogopa kutupiwa madongo. KP ni mbunifu kwa mambo mengi na hili mojawapo (hata kama kaiga kwa sababu yeye si wa kwanza).

Naamini atakuwa na nafasi ya kupokea maoni au washikaji wanaopita humu wataweza kumpa baadhi ya maoni mazuri mnayotoa. Itakuwa vizuri pia wenye ushauri wampatie. Ila hata wale ambao wana maoni tofauti wayatoe ili kama yanaweza kusaidia yaonekane kwa wadau. Ujamaa ulishaisha na sasa watu wanatakiwa kujitafutia jinsi ya kuishi bia kuiba au kufisadi. Na hapa ndipo suala la ubunifu linapokuwa la muhimu sana.

Mwenye namba yake ya simu atuwekee hapa tumtwangie. Nitakuwa wa kwanza kumtia moyo. Ila kama ningekuwa mjanja basi hii kwangu ingekuwa fursa ya kutegeneza mradi kwani wateja wapo (vijana wajinga walio na kiu ya kujiendeleza). Kazi nzuri KP
 
Me nadhani tukimsifia tutakuwa tunampa kichwa bure ukiangalia hiyo show anaiga karibu kila kitu kutoka big brother, ajaribu kuwa creative na sisi tutamuunga mkono.

mzeee umesahau siku hizi ni mwendo wa copy, paste and edit! ukija na jipya kila mtu atalichukua na kuliboresha zaidi...na ukisubiri uwe na jipya utasubiri hadi uzeeke bila kutoa mchango wowote humu duniani..sana sana labda mbolea
 

Mkuu,

Mtu unatakiwa kuwa mbunifu uanza sehemu furani, masoud kipanya nayekawa mbunifu huo ni mwanza. Watanzania wenzetu si vema kumponda kiasi hicho, wewe kinaku-bore kuna watu wengi tu wanakifurahia.

Binafsi naona kama umeangalia na kuona mapungufu toa "positive criticism" kwa ajiri ya kuki-improve kipindi wanavyoendelea. Kumbuka leo unamfurahia kupanda ndege lakini mtu wa kwanza wakati anaanza na idea yake kuna watu kama wewe walimpnda kwa kumwoma kama punguani, kuna wale walitoa positive challenge na kufanya improvement kila wakati mpaka leo. Ulizia story ya SUN CITY South Africa utashangaa.

Pia si sahii kufananisha maishaplus na big brother maana hiyo iko tayari level ya juu sana na capital invested ni kubwa sana. Leo hii Masoud Kipanya akipata hela ya kutosha utashangaa, lakini akija hata kwako waafrika wengi walivyo na idea ya ku-improve imeandikwa safi utamwambia humwamini na hauta mpa hela.

Kimsingi wazo la masoud ni zuri linatakiwa kuungwa mkono kimawazo na kipesa ili tuwe na kitu cha kwetu kizuri nchi nyingine za africa na ulaya wawe nao wanafuatilia
 
ebwana weee! sisi tuliopo nje ya tz kumbe tunakosa mambo huko, enhee...! hebu tujuvyeni vizuri mshaiga nini , baada ile BSS?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…