Safari fupi ya kuzimu. Sijutii maisha yangu

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,308
14,207
Sehemu ya kwanza
Habari za wakati huu,

Niite Mark ni mtu mzima nilikuwa na mke na watoto 6. Nimzaliwa wa mkoani Kilimanjaro, moshi mjini Njoro. Elimu yangu ilikuwa ya kulenga kwa manati kutokana na nyumbani hali haikuwa nzuri sana kifedha.

Na hii ni stori yangu fuatana nami hadi mwisho utajifunza mengi.

Nyumbani kwetu tupo 10 wakiume 7 na wakike 3 wote hamna ambaye ananafuu kimaisha hali ni dhofu sana. Baada ya mzee kufariki na mama naye kufuatia, sisi kama ndugu tuliamua kuuza nyumba ya urithi ili kila mtu afe na chake mapema.

Ndipo nilipoamua kujiingiza kwenye biashara ya maparachichi, ambayo nilikuwa naenda vijijini moshi kukusanya mzigo na kuleta sokoni. Biashara sikuwahi kufanya mwanzo ndio mara ya kwanza.

Kiujumla biashara ilianza kuwa nzuri namimi nikaona hii sasa ndio yenyewe nilikuwa wapi sikuzote hizi? Soko likakuwa mpaka siku moja majira ya jioni nikiwa mitaa ya boma mbuzi pasua, nikiwa na mtaji wa kutosha nimetulia walipokuja wazee wa kazi nakunisafisha pesa zote nilizokuwa nazo.

Mvua inanyesha na kaubaridi na hela ya nyumba ya urithi ikawa imeenda hivyo. Sikuwa na lakufanya ila roho iliniuma sana kwasababu nilitakiwa nianze tena moja upya!

Nikajiingiza kwenye kazi za ufundi kwasababu nilikuwa nazijua, hizi za ujenzi na mzee pia alikuwa fundi. Kazi zikawa nazipata kwa kulenga kwa manati ila mafundi wengine naona wao wanapata( wanapeana kazi kwa kujuana).

Kila mja na riziki yake, nikapata kazi ya kujenga nyumba ya room 3, kuipiga plasta pamoja na kupaua. Nikaona hapa ndio penyewe nikaamua kugawa namimi riziki kwa mafundi wengine ili siku nao wakipata wanikumbuke.

Ile kazi ilikuwa nzuri na ilikuwa na hela kwa kweli, kazi ilianza na ilikuwa inaenda vizuri mpaka siku moja baada ya kula msosi wa mchana, kila nikinyanyua tofali nahisi kichomi nikilitua nakuwa freshi.

Nikasema acha niende geto niue siku ya leo. Njiani nikiwa naelekea magetoni niliteleza nikaanguka nikaumia mgongo. Ikabidi ile kazi nimuachie fundi mwingine kwa mapatano.

Baada ya wiki kuisha nikasema nirudi saiti namkuta tajiri kafura kwa hasira kazi chafu ukuta umepinda! Shughuli yangu ikaishia hapo akapewa mkataba fundi mwingine mmoja wa wale niliowaita. Maisha lazima yaendelee.
Nikapata kazi maeneo ya uhuru hostel kupiga plasta.

Tajiri kuleta material sio shida ila kukupa hela yako wewe kama fundi ndio utata unapoanzia. Mara atasema plasta mbona haijanyooka, mara ratio nyepesi sana, sijui umeniibia cement. Ilimradi tu asikupe hela.

Nlipoamua kumkomalia zaidi anipe pesa zangu, akanipa nusu nyingine akasema atanimalizia saiti inasimama kwanza, kumbe saiti haijasimama bali katafuta fundi mwingine namimi ndio kanichinjia baharini. Na hiyo nusu iliobaki hakuwahi kunilipa tena.

Haya maisha haya....... Usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Tena ushukuru Mungu, ungeumia uti wa mgongo ulipoanguka ungekuwa mtu wa kitandani tu. Ila jipe moyo, hebu tupia jicho katika ulimwenguni wa roho, "kuna aliyekushika shati?"
 
Sehemu ya pili.
Mtaani hali ilianza kuwa ngumu kidogo hivyo nikaona nibadili upepo wa maisha na kuanza kuingia kwenye shughuli ya uchanaji wa mbao. Ilikuwa na unafuu kidogo japo ilikuwa risky, kutokana na kuingia mpaka maeneo ya hifadhi kutafuta miti ya kenfa ambayo ndio ilikuwa na hela zaidi.

Siku moja tukiwa pori tunachana, ikasemekana tajiri anakuja kununua miti zaidi na kutulipa hela zetu. Basi tukamsubiri sahiyo tushakaa kama wiki 3 bila bila. Kweli alikuja akapakia mbao zake na akanunua miti mingine. Kumhoji pesa zetu akasema ngoja arudi aende akatuongezee unga na dagaa wa hapo camp. Hiyo ikawa imekula na gia yake ya kuondokea.

Pale pori tukatoboa wiki 3 nyingine, tunaishi kama wanyama hakuna mwenye hata ndururu mfukoni. Kila mtu nyongo ya hasira ilianza kumpanda, tukagoma kuendelea kuchana mbao huku tukishauriana tutafute mteja wa zile mbao. Utasema alikuwa anatusikia, tajiri ghafla huyu hapa. Yule mzee nikama alikuwa anatumia madawa hivi, maana wote tuliingia baridi na tukasahau hata kama tunadai hela zetu.

Siku hiyo katununulia na kambuzi kakutudanganyishia na mchele. Mbao zikapakiwa akatuambia tupige hesabu tunamdai kiasi gani cha fedha, nasisi tukampa hesabu. Akachomoa kibunda akatupooza kidogo, yaani tushakaa wiki 7 katika hela tunayodai katulipa asilimia 5 alafu bado tuendelee kufanya kazi.

Nikaona huu sasa ni ujinga maana kila ukisema utafute mteja wa mbao hupati na ukimpata gari likija linakwama njiani. Fundi mmoja baada ya mwingine akaanza kuondoka bila ya kuaga. Kuja kushtuka nimeachiwa rengeta na chensoo niko mwenyewe. Nikajaa upepo sasa naondokaje na hapa kuna mali za watu. Tajiri naye baada ya siku mbili kaja kabeba mbao kaleta mafundi wengine. Namimi nikaondoka naye mpaka town, kanijizungusha wee mara aingilie huku mara atokee huku mwisho siku kaja kunilipa hela zangu zote saa 6 usiku.

Hela zilikuwa nyingi na nilipanga nianze biashara ya duka. Lakini hata wiki haikuisha hela zote zimekata ukiniuliza nilitumiaje mi mwenyewe sijuwi ila hela zilikata zote. Kesho yake nakutana naye mitaa ya majengo ananiambia ana kazi ya plasta nyumbani kwake niongozane naye, sahiyo nishasema sitofanya kazi naye tena ila nkajikuta kwake nimefika na kazi nimeanza ilikuwa kubwa ni ukuta wa uzio na vyumba 10 vya wapangaji huko shanti town.

Kazi niliuziwa hivyo nikaamua kulala hapo hapo saiti ila usiku ukilala unasikia mtu anabisha hodi, ukienda kufungua hakuna mtu mara unasikia milango mingine inafunguliwa yaani ni full mauzauza. Pesa za jamaa za moto, kazi yenyewe ya moto na hela nazitaka.

Nikasema acha nikomae mimi ni mtoto wakiume, lakini kila ukifanya kazi nikama haiendi vile unaeza ukachapia gara moja ukamaliza na kupiga kibao mara dongo lote linaachia ukutani. Au sanyingine uchapia dongo linaingia machoni macho yanawasha unaosha macho lakini wapi.

Msosi wa mchana ukila ukipumzika tu usingizi unakukamata kuja kushtuka unaamshwa ule cha usiku saa tatu usiku. Nikaomba nifungiwe taa ili niwe nakesha sasa usiku. Ila unaweza shangaa mara umeme umekatika nyumba nzima giza tupu kwa lisaa lizima, kwasababu ya uchovu unaamua kulala na kujipa matumaini kesho nayo siku. Ila ukilala tu unaota ndoto za ajabu ajabu sana sanyingine umetumbukia kwenye shimo la choo, mara ukabwe na jinamizi.

Siku hiyo ndo ilizidi kuwa mbaya maana baada ya mauza uza niliposhtuka nilikuta paka amekufa pembeni yangu na mimi nina chale mwilini. Usiku huo huo hata vifaa sikubeba niliondoka kurudi kwangu nakuona nikiendekeza tamaa ntauwawa huku.

Je, nini kitafuata usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Malizia hii story we jamaa acha utapeli.

Sehemu ya pili.
Mtaani hali ilianza kuwa ngumu kidogo hivyo nikaona nibadili upepo wa maisha na kuanza kuingia kwenye shughuli ya uchanaji wa mbao. Ilikuwa na unafuu kidogo japo ilikuwa risky, kutokana na kuingia mpaka maeneo ya hifadhi kutafuta miti ya kenfa ambayo ndio ilikuwa na hela zaidi.
Siku moja tukiwa pori tunachana, ikasemekana tajiri anakuja kununua miti zaidi na kutulipa hela zetu. Basi tukamsubiri sahiyo tushakaa kama wiki 3 bila bila. Kweli alikuja akapakia mbao zake na akanunua miti mingine. Kumhoji pesa zetu akasema ngoja arudi aende akatuongezee unga na dagaa wa hapo camp. Hiyo ikawa imekula na gia yake ya kuondokea.
Pale pori tukatoboa wiki 3 nyingine, tunaishi kama wanyama hakuna mwenye hata ndururu mfukoni. Kila mtu nyongo ya hasira ilianza kumpanda, tukagoma kuendelea kuchana mbao huku tukishauriana tutafute mteja wa zile mbao. Utasema alikuwa anatusikia, tajiri ghafla huyu hapa. Yule mzee nikama alikuwa anatumia madawa hivi, maana wote tuliingia baridi na tukasahau hata kama tunadai hela zetu.
Siku hiyo katununulia na kambuzi kakutudanganyishia na mchele. Mbao zikapakiwa akatuambia tupige hesabu tunamdai kiasi gani cha fedha, nasisi tukampa hesabu. Akachomoa kibunda akatupooza kidogo, yaani tushakaa wiki 7 katika hela tunayodai katulipa asilimia 5 alafu bado tuendelee kufanya kazi.
Nikaona huu sasa ni ujinga maana kila ukisema utafute mteja wa mbao hupati na ukimpata gari likija linakwama njiani. Fundi mmoja baada ya mwingine akaanza kuondoka bila ya kuaga. Kuja kushtuka nimeachiwa rengeta na chensoo niko mwenyewe. Nikajaa upepo sasa naondokaje na hapa kuna mali za watu. Tajiri naye baada ya siku mbili kaja kabeba mbao kaleta mafundi wengine. Namimi nikaondoka naye mpaka town, kanijizungusha wee mara aingilie huku mara atokee huku mwisho siku kaja kunilipa hela zangu zote saa 6 usiku.
Hela zilikuwa nyingi na nilipanga nianze biashara ya duka. Lakini hata wiki haikuisha hela zote zimekata ukiniuliza nilitumiaje mi mwenyewe sijuwi ila hela zilikata zote. Kesho yake nakutana naye mitaa ya majengo ananiambia ana kazi ya plasta nyumbani kwake niongozane naye, sahiyo nishasema sitofanya kazi naye tena ila nkajikuta kwake nimefika na kazi nimeanza ilikuwa kubwa ni ukuta wa uzio na vyumba 10 vya wapangaji huko shanti town.
Kazi niliuziwa hivyo nikaamua kulala hapo hapo saiti ila usiku ukilala unasikia mtu anabisha hodi, ukienda kufungua hakuna mtu mara unasikia milango mingine inafunguliwa yaani ni full mauzauza. Pesa za jamaa za moto, kazi yenyewe ya moto na hela nazitaka.
Nikasema acha nikomae mimi ni mtoto wakiume, lakini kila ukifanya kazi nikama haiendi vile unaeza ukachapia gara moja ukamaliza na kupiga kibao mara dongo lote linaachia ukutani. Au sanyingine uchapia dongo linaingia machoni macho yanawasha unaosha macho lakini wapi. Msosi wa mchana ukila ukipumzika tu usingizi unakukamata kuja kushtuka unaamshwa ule cha usiku saa tatu usiku. Nikaomba nifungiwe taa ili niwe nakesha sasa usiku. Ila unaweza shangaa mara umeme umekatika nyumba nzima giza tupu kwa lisaa lizima, kwasababu ya uchovu unaamua kulala na kujipa matumaini kesho nayo siku. Ila ukilala tu unaota ndoto za ajabu ajabu sana sanyingine umetumbukia kwenye shimo la choo, mara ukabwe na jinamizi.
Siku hiyo ndo ilizidi kuwa mbaya maana baada ya mauza uza niliposhtuka nilikuta paka amekufa pembeni yangu na mimi nina chale mwilini. Usiku huo huo hata vifaa sikubeba niliondoka kurudi kwangu nakuona nikiendekeza tamaa ntauwawa huku.
Je nini kitafuata usikose kufuatana nami hadi mwisho...........
To be continued...!!!
 
Pasua, boma mbuzi,njoro, matindigani, mtaa wa dhambi, kalimani , don Bosco, bonitee mitaaa yote huko uswahili mwingi ila kama ni chai basi hii ya kahawa maana kazi zote ulizosema mauza uza kawaida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom