Maisha na Falsafa yake

ONJO

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
215
261
SEHEMU YA 1
Maisha ni mda anaoishi mwanadamu toka kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake.
Tena maisha yanasifa moja kwa kila mwanadamu kama ifuatavyo,
watu wengi wamekuwa wakisema kuwa maisha ni magumu kwa sababu ya changamoto nyingi kama,
Kukosa chakula,kutoolewa,kusalitiwa,ajari za ghafla,magonjwa ya mara kwa mara,kukosa mitaji,kukosa ajira,kufukuzwa kazi,kupigana na mambo mengine yanayofanya maisha yaonekane magumu.Mambo hayo ni kweli kwani tunajionea wenywe kwenye jamii zetu yakitokea.
MZANI WA MAISHA
upo mzani ambao utamuonesha kila mtu kwamba yeye yupo upande gani wa maisha;kwamba ni huzuni au furaha.

kuwa na hasira,wivu,chuki,kisasi,msongo wa mawazo,wasiwasi,hofu,kukosa uaminifu,matukano,kufoka ovyo,umbea,unafiki,upendeleo,ukabila,udini,kutojizuia na kadhalika.
hayo yote ni kipimo tosha kwa maisha yetu,kwani kupitia hayo tumejiharibu wenyewe na kuondoa amani,furaha na upendo juu ya uso wa nchi kwani hayo yote ndiyo tunu mhimu kwa kila Binadamu.Mambo hayo tutajadili kwa kina katika sehemu inayofuata,na ndani ya mada hii tutajifunza kuukubali ukweli ili kuhakikisha amani,furaha na upendo uliopotea unarejea ndani ya jamii zetu.

KWELI NNE ZA MAISHA
1.Maisha ni mzunguko
2.Maisha ni ufahamu
3.Maisha ya watu ni sahihi katika mienendo yao
4.Maisha ni amani,furaha na upendo

MAISHA NI MZUNGUKO
furaha,upendo na amani huja kwa kila binadamu kwa wakati wake na kupotea pia kwa wakati wake.Manung'uniko,kilio,maombolezo na huzuni huja kwa kila binadamu kwa wakati wake na kutoweka kwa wakati wake.Mfano furaha huja mtu anapoolewa,anapopewa zawadi,anapopata ajira,anapopata utatuzi kwenye changamoto zake,anaposaidiwa,anapopendwa na kadhalika.Furaha hukosekana pale anapofiwa,anaposalitiwa,anapokosa chakula,anapokosa pesa ya kulipa kodi,anapokuwa mgonjwa,anapokuwa masikini,anapoona wenzake wamefanikiwa na kadhalika.Haya yote hufanya kujirudiarudia pindi binadamu anapokuwa anaishi,na kuyaepuka haya yote mpaka wakati anapokufa kila kitu kwake hutoweka;kama hakuwahi kuwepo katika Dunia hii.

MAISHA NI UFAHAMU
Kama tukifanikiwa kujua ukweli juu ya kila jambo,basi si kwamba maisha yatakuwa ya furaha bali kwa kuukubali ukweli tutafahamu namna ya kutatua changamoto zetu,si kwamba tuking'atwa na nge hatutaumia bali tutaumia huku tukiwa tunajua kuwa asili ya nge ni kung'ata hivyo tutajifunza kutolipiza kisasi.

MAISHA YA WATU NI SAHIHI KATIKA MIENENDO YAO
Tujifunze kukubaliana na maisha ya kila mtu kwani mtu ni mbaya kwasababu ya matokeo ya mawazo yake kuwa ni mabaya au ni Mzuri kwasababu mawazo ndani ya moyo wake ni mazuri.Basi tukifahamu hilo tujifunze kwa utaratibu kurekebisha tabia mbaya za wenzetu,na sio kukimbilia kuwahukumu kwamba flani ni mwizi au halipi madeni au mchoyo.Hakika nasema yeyote afanyaye hayo amepungukiwa na ufahamu;na ufahamu wenyewe ndio huu kwamba tuujue ukweli na mambo yetu yatakuwa barabara.

MAISHA NI FURAHA,AMANI NA UPENDO
Kwa kuufahamu ukweli juu ya maisha hatutakuwa na kinyongo na mtu yeyote,kwani watu wote tutawaona kuwa ni sawa tena tutawaona kama ndugu zetu,marafiki zetu,watani zetu na kila jina lenye uzuri litaenea ndani ya jamii zetu;furaha,amani na upendo vitakuwa juu yetu.

Nipende tu kusema huu ni kama utangulizi,sehemu ijayo tutachambua kwa kina kuhusu mzani,kwani mzani huo umebebwa na kweli nne za maisha.

Karibuni kwa maoni yote yahusuyo kweli za maisha,wala mimi sijakomaa bali napenda pia kujifunza kutoka kwa wenzangu.
Na ONJO karibuni.

SEHEMU YA 2
Maisha ni ufahamu;wapendwa kujua udhaifu wetu ndiyo chanzo pekee cha ufahamu na jitahada katika kutafuta suluhisho kwa changamoto zetu.Kupitia ufahamu ndio tutajua kuishi kwa usawa hasa tukizingatia mzani wa maisha.

HASIRA;mtu mwenye hasira ni mbaya sana,hufoka ovyo,hutukana na kufanya maumivu kwa wengine.Basi tujifunze kukaa kimya pale tunapo uziwa.Ni afadhali kukaa kimya ili amani itawale kuliko kuropoka na kuondoa amani.
KISASI;Mapatano yamepungua kwasababu ya kulipiza kisasi,jirani yako anakunyima jembe na analo na wewe unamnyima siku akikuomba.Tujifunze kutolipiza kisasi ili tuwe na mapatano na watu wote.
WIVU:unamuona ndugu yako anabiashara nzuri wewe unamwimbia je kipi bora kuwa na cha kwako au kuiba?tutafte vya kwetu.
WASIWASI;Una mtaji unataka uanzishe mradi unawaza sijui nitapata faida?Ndugu ni nani anayevuna bila kupanda?Basi tuache wasiwasi tukiamua jambo tufanye kweli.
UPENDELEO;Watu wengi wamepoteza rasilimali watu kwa sababu ya upendeleo,flani simkopeshi kwa sababu hanisalimii.Je wewe ni Mungu mtu unataka ufanyiwe kama unavyowaza?
MSONGO WA MAWAZO:Mtu unakuta anamawazo toka miaka anakua,flani alinitukana,flani kanicheat nitamfanyia kitu kibaya,flani amenikopa hataki kunilipa na mengine, haya yote hufanya kichwa kuwa kizito na kukosa amani
.Tuache yaliyopita tushughulike na ya leo.
KULAUMU:Mtu analaumu yule Raisi ni mshenzi sana hatoi ajira,au john kaniahid kunioa amenidanganya.Kisa tu mambo yake hayaendi vizuri.Kabla hujalaumu jiulize wewe umefanya lipi la maana?
UDINI NA UKABILA:Watu hukengeuka na kujali watu wa dini zao au kabila,katika kusaidia,kutoa ajira bila uelewa wa jambo lolote
wakisahau kwamba hakuna yeyote aliyezaliwa na dini au kabila wote tumeyakuta tu.Tujifunze kujali watu wote ndipo tutafurahia uzuri wa maisha.

HITIMISHO
Kwa kumalizia katika sehemu hii,naomba tujiepushe na mambo yote ambayo yanahatarisha amani yetu,furaha yetu na upendo.Kwani kwa kuujua ukweli wa maisha tutaweza kutatua kila aina ya changamoto ikiwemo ndani ya serikali,ndani ya mikoa,ndani ya wilaya,ndani ya tarafa,ndani ya kata,ndani ya vijiji,ndani ya vitongoji na ndani ya familia zetu.Hata hivyo falsafa ya maisha itatupatia viongozi bora kwa taifa letu.

SEHEMU YA 3
Maisha ya watu ni sahihi katika mienendo yao,tukijiua hilo kwamba flani ni mwizi,anahasira,anachepuka sana,anasali sana,anacheza sana,mwanaume kusuka.Tusiwashangae kwani hali yao ya ndani ndiyo inawafanya kuwa hivyo.Na hapa tutajifunza kufanya haya.

TUSIWAHUKUMU,Tusiseme flani msimsaidie kwa kuwa halipi madeni.Nawaambia yeyote afanyaye hayo umepungukiwa na ufahamu na kujihesabia kuwa yeye ni mwenye haki kuliko wengine.
TUSIWATENGE,Mtu anayependwa na watu ni yule anayejali au kuwasaidia na wale waliomchukiza siku za nyuma.Na nawaambia lazima tutatukanwa,najua tutaumia lakini wakati huo tusijibu kitu.Kwani ukipewa zawadi lazima uichukue?Tufanyeni hivyo ili kulinda amani.
TUWASAIDIE;Usishangae mtu aliyekuzulumu miaka iliyopita akija kwako umsaidie.Tuendelea kuwasadia kwasababu yote ya nyuma yatakumbushwa na wema wako.Kanuni ya kumsaidia mtu ni kuwa nacho.Je utamsaidia kile usichokuwa nacho?
TUWAELEKEZE:Tujifunze kutoa ushauri kwa yule anayetaka kushauriwa.Mfano kuchepuka ni kosa,kwanini uendelee kuchepuka wakati kile unacho kipata kwa wake za watu na mke wako anacho?Asipoelewa sisi tunawe maana kwa kosa hilo analolifanya ndilo litakalomadhibu.
TUWASAMEHE.Kwa kuujua ukweli tutaweza kumsamehe hata yule aliyetuumiza jana.Jana umemkuta anamke wako lodge akija kutaka msaada kwako tumsaidie.Kwani kati ya mke wako na yeye nani mwenye kosa,kwa kufanya hivyo tutaukubali ukweli na amani itatawala.

SEHEMU YA 4
Maisha ni amani,furaha na upendo.Ili tuwe na amani ndani ya jamii zetu yatupasa kufanya yafuatayo..

KUTOA HAKUNA MWISHO
Tunajua mvua ilikuwepo toka zamani na inanyesha nyakati zetu je hili si fundisho kwetu?
Unaonaje mtu yeye yule yule umemsaidia leo unga,kesho anakuja anaomba maji,unampa,anaomba karanga unampa,yaani kilakitu akiomba unampa je hiyo sawa na mvua;basi tujifunze kutochoka kusaidia watu kwani kwa kufanya hivyo tutakula matunda ya mema yetu.
TUWE NA MSIMAMO MMOJA:angalia nge asili yake ni kung'ata hata umwokea ndani tanuru la moto lazima tu atakung'ata ukimsongezea moto.Yaani ndio alivyo hata tusiumize kichwa kumuua.Kwa mfano huo tutajifunza kutolipiza kisasi,kubagua watu,tutaacha unzinzi;tutaacha wizi,tutaacha kuogopa.Na tutafanya upande wa kutenda mema kuwa asili yetu na kuitetea asili yetu.

TUWE NA IMANI
Tufanye mambo yetu kwa kuamini kwamba tutafanikiwa,bila kulaumu,bila chuki na mtu hakika tutafanikiwa.

MTAZAMO SAHIHI
Mtazamo wetu ukiwa vizuri tutaishi na watu vizuri,changamoto zikija tuone kwamba tunastahili kuzipa tena kwa sura yenye furaha kwani kwa kila changamoto kuna jambo zuri ndani yake.Kwa kufanya hivyo tutasahau kama kuna matatizo,kuna vilio na tutakuwa watu wa furaha siku zote mpaka kufa kwetu.

Nahitimisha kwa kusema hivi maisha yana amani,furaha na upendo kwani kwa kujifunza kuukubali ukweli ndio utatuzi wa changamoto zote.Nimekuwa mtu wa furaha siku zote kwani furaha ipo ndani ya moyo wangu wala haitokani na mtu yeyote.Nimejifunza kuyaepuka mambo yote yanayoondoa furaha yangu,mpaka sasa nimeshasahau kama kuna kulia,kununa,kukasirika.Nimekuwa mtu wa kupendaza kwa watu wote tena mwenye kupendwa na watu kwa sababu nimeielewa falsafa ya maisha ndio maana nikoona niwaandikie makala hii.
Mwisho nisema kuona furaha katika maisha sio kwamba lazma uwekewe mikono na wachungaji hapana bali ukielewa falfasa ya maisha unaweza ukaishi zaidi ya mchungaji,zaidi ya mashehe,zaidi ya mapadri na maaskofu.kwani kuipata njia ya wongofu sio lazma ukeshe makanisani au misikitini bali kwa kuikubali kweli tunaweza tukaishi maisha ya mbinguni tukiwa duniani.Na si lazima tuombewe ndio tuwe watakatifu bali tunaweza tukaishi kitakatifu hata tukiwa majumbani kwetu.

Mimi ONJO najua nivigumu kwenu kuniona kwa sura,bali yeye asomaye mafundisho yangu,akaelewa na akaishi kwa kutenda atamuona ONJO wa kweli katika maisha yake.

Itafuteni amani,furaha na upendo kupitia fundisho hili.Mimi naamini katika kweli,ninaishi katika kweli na ninaitetea kweli.
Mbarikiwe nyote.
2023-01-14-18-13-10.png

MAISHA

MUNGU
WEWE BINAFSI (MIMI)
PESA

MUNGU
Mjue muumba wako na kuzifata sheria zake ukitaka kuzijua hizo soma vitabu vinavyohusu dini yako naushike maagizo upate kujua kweli itakayo kuweka huru

WEWE BINAFSI (MIMI)
jitafute wewe ninani ?
Tafta kipawa chako ili kila utakalo lifanya ulifanye ukiwa na furaha uepuke kufanya mambo kama mtumwa

PESA
PESA huja endapo utafatilia hayo mambo mawili ya mwazo ndio yamsingi zaidi inachotakiwa ukijue kwenye pesa ni namna ya kuieshimu kuifanya itembee kwa kiwango chako isikuzidi wala isikupigukie

Hayo ndio maisha na tunastaili kuishi ili tuyaishi
 
Nashukuru kiongozi
Maswali;
1. Kwanini washika dini hawana hela
2. Waabudu mizimu, washirikina kwanini mambo yao hunyooka?
3. Nguvu ya kiroho nyuma ya mtu huamua mafanikio yake sasa tutamilikije fedha bila nguvu ya kiroho?
4. Tunawezaje kuwatawala binadamu wenzetu bila nguvu ya ziada ya kiroho?
 
Hayo yote yanajibiwa na falsafa ya maisha
 
" Maisha ni mda anaoishi mwanadamu toka kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake."

Nionavyo Mimi:

Maisha ni muda baina ya sasa na mwisho wako.

( Life is a pace between NOW and your END)
 
" Tena maisha yanasifa moja kwa kila mwanadamu kama ifuatavyo,
watu wengi wamekuwa wakisema kuwa maisha ni magumu kwa sababu ya changamoto"

∆ Mungu aliyaweka maisha ya mwanadamu katika mfumo wa changamoto ( na sio ugumu).

Kila changamoto Ina jibu lake, na mungu hampi mwanadamu changamoto ambayo hutaweza kuitatua au kuipatia jibu/majibu.

Ili upate jibu/majibu ya changamoto yoyote Ile angalia mambo haya manne (4) :

1. Matendo Yako
2. Tabia zako
3. Ufanisi wako
4. Sababu/kusudi lako

Mfano; kama wewe ni "mwanandoa"

1. Matendo Yako

Kama ni changamoto inayohusu ndoa Yako angalia "matendo Yako" katika ndoa Yako. Unatenda matendo gani katika ndoa Yako, unaiheshimu ndoa Yako? Unaishi maisha ya ki-ndoa? Unajivunia ndoa yako? Uko tayari kufanya lolote kuinusuru ndoa yako? Unasali na kuiombea ndoa Yako? n.k

2. Tabia zako

Tabia zako juu/kuhusu ndoa Yako zikoje?
Unatenga muda Kwa ajili ya Yako? Unazungumza kuhusu mwenendo wa ndoa Yako na mwenzako? Una marafiki wa maana na wenye ndoa pia ambao anaambatana nao? Uko muwazi juu ya maswala ya kiuchumi na mipango ? n.k

3.ufanisi wako

Ufanisi/efficiency

How efficient are you na ndoa Yako? Ni Kwa kiasi gani unaweka muda wako, nguvu zako kuhakikisha ndoa Yako inasimama imara katika Kila nyanja Yani kiimani, kiuchumi, kijamii, tabia, mienendo n.k

4. Sababu/kusudi

Uliamua binafsi kuingia katika ndoa? Unaishi kiapo Cha ndoa Yako? Uko tayari kutatua lolote muda saa na wakati wote katika ndoa yako? maisha Yako yamezaa maana Kwa wewe kukata shauri kuingia kwenye ndoa?
 
Good indeed hiyo ni nyongeza katika falsafa ya maisha nadhani tukiendelea kuweka vitu.Siku moja tutaweza kuishawishi serikali ianzishe somo la maisha na falsafa yake.
 
Maisha aahah....... Maisha wewe huna kanuni mbaguzi sana wewe

Vp mkuu wewe umebahatika kuyaekewa maisha.
 
SEHEMU YA 1
Maisha ni mda anaoishi mwanadamu toka kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake.
Tena maisha yanasifa moja kwa kila mwanadamu kama ifuatavyo,
watu wengi wamekuwa wakisema kuwa maisha ni magumu kwa sababu ya changamoto nyingi kama,
Kukosa chakula,kutoolewa,kusalitiwa,ajari za ghafla,magonjwa ya mara kwa mara,kukosa mitaji,kukosa ajira,kufukuzwa kazi,kupigana na mambo mengine yanayofanya maisha yaonekane magumu.Mambo hayo ni kweli kwani tunajionea wenywe kwenye jamii zetu yakitokea.
MZANI WA MAISHA
upo mzani ambao utamuonesha kila mtu kwamba yeye yupo upande gani wa maisha;kwamba ni huzuni au furaha.

KWELI NNE ZA MAISHA
1.Maisha ni mzunguko
2.Maisha ni ufahamu
3.Maisha ya watu ni sahihi katika mienendo yao
4.Maisha ni amani,furaha na upendo

MAISHA NI MZUNGUKO
furaha,upendo na amani huja kwa kila binadamu kwa wakati wake na kupotea pia kwa wakati wake.Manung'uniko,kilio,maombolezo na huzuni huja kwa kila binadamu kwa wakati wake na kutoweka kwa wakati wake.Mfano furaha huja mtu anapoolewa,anapopewa zawadi,anapopata ajira,anapopata utatuzi kwenye changamoto zake,anaposaidiwa,anapopendwa na kadhalika.Furaha hukosekana pale anapofiwa,anaposalitiwa,anapokosa chakula,anapokosa pesa ya kulipa kodi,anapokuwa mgonjwa,anapokuwa masikini,anapoona wenzake wamefanikiwa na kadhalika.Haya yote hufanya kujirudiarudia pindi binadamu anapokuwa anaishi,na kuyaepuka haya yote mpaka wakati anapokufa kila kitu kwake hutoweka;kama hakuwahi kuwepo katika Dunia hii.

MAISHA NI UFAHAMU
Kama tukifanikiwa kujua ukweli juu ya kila jambo,basi si kwamba maisha yatakuwa ya furaha bali kwa kuukubali ukweli tutafahamu namna ya kutatua changamoto zetu,si kwamba tuking'atwa na nge hatutaumia bali tutaumia huku tukiwa tunajua kuwa asili ya nge ni kung'ata hivyo tutajifunza kutolipiza kisasi.

MAISHA YA WATU NI SAHIHI KATIKA MIENENDO YAO
Tujifunze kukubaliana na maisha ya kila mtu kwani mtu ni mbaya kwasababu ya matokeo ya mawazo yake kuwa ni mabaya au ni Mzuri kwasababu mawazo ndani ya moyo wake ni mazuri.Basi tukifahamu hilo tujifunze kwa utaratibu kurekebisha tabia mbaya za wenzetu,na sio kukimbilia kuwahukumu kwamba flani ni mwizi au halipi madeni au mchoyo.Hakika nasema yeyote afanyaye hayo amepungukiwa na ufahamu;na ufahamu wenyewe ndio huu kwamba tuujue ukweli na mambo yetu yatakuwa barabara.

MAISHA NI FURAHA,AMANI NA UPENDO
Kwa kuufahamu ukweli juu ya maisha hatutakuwa na kinyongo na mtu yeyote,kwani watu wote tutawaona kuwa ni sawa tena tutawaona kama ndugu zetu,marafiki zetu,watani zetu na kila jina lenye uzuri litaenea ndani ya jamii zetu;furaha,amani na upendo vitakuwa juu yetu.

Nipende tu kusema huu ni kama utangulizi,sehemu ijayo tutachambua kwa kina kuhusu mzani,kwani mzani huo umebebwa na kweli nne za maisha.

Karibuni kwa maoni yote yahusuyo kweli za maisha,wala mimi sijakomaa bali napenda pia kujifunza kutoka kwa wenzangu.
Na ONJO karibuni.

SEHEMU YA 2
Maisha ni ufahamu;wapendwa kujua udhaifu wetu ndiyo chanzo pekee cha ufahamu na jitahada katika kutafuta suluhisho kwa changamoto zetu.Kupitia ufahamu ndio tutajua kuishi kwa usawa hasa tukizingatia mzani wa maisha.

HASIRA;mtu mwenye hasira ni mbaya sana,hufoka ovyo,hutukana na kufanya maumivu kwa wengine.Basi tujifunze kukaa kimya pale tunapo uziwa.Ni afadhali kukaa kimya ili amani itawale kuliko kuropoka na kuondoa amani.
KISASI;Mapatano yamepungua kwasababu ya kulipiza kisasi,jirani yako anakunyima jembe na analo na wewe unamnyima siku akikuomba.Tujifunze kutolipiza kisasi ili tuwe na mapatano na watu wote.
WIVU:unamuona ndugu yako anabiashara nzuri wewe unamwimbia je kipi bora kuwa na cha kwako au kuiba?tutafte vya kwetu.
WASIWASI;Una mtaji unataka uanzishe mradi unawaza sijui nitapata faida?Ndugu ni nani anayevuna bila kupanda?Basi tuache wasiwasi tukiamua jambo tufanye kweli.
UPENDELEO;Watu wengi wamepoteza rasilimali watu kwa sababu ya upendeleo,flani simkopeshi kwa sababu hanisalimii.Je wewe ni Mungu mtu unataka ufanyiwe kama unavyowaza?
MSONGO WA MAWAZO:Mtu unakuta anamawazo toka miaka anakua,flani alinitukana,flani kanicheat nitamfanyia kitu kibaya,flani amenikopa hataki kunilipa na mengine, haya yote hufanya kichwa kuwa kizito na kukosa amani
.Tuache yaliyopita tushughulike na ya leo.
KULAUMU:Mtu analaumu yule Raisi ni mshenzi sana hatoi ajira,au john kaniahid kunioa amenidanganya.Kisa tu mambo yake hayaendi vizuri.Kabla hujalaumu jiulize wewe umefanya lipi la maana?
UDINI NA UKABILA:Watu hukengeuka na kujali watu wa dini zao au kabila,katika kusaidia,kutoa ajira bila uelewa wa jambo lolote
wakisahau kwamba hakuna yeyote aliyezaliwa na dini au kabila wote tumeyakuta tu.Tujifunze kujali watu wote ndipo tutafurahia uzuri wa maisha.

HITIMISHO
Kwa kumalizia katika sehemu hii,naomba tujiepushe na mambo yote ambayo yanahatarisha amani yetu,furaha yetu na upendo.Kwani kwa kuujua ukweli wa maisha tutaweza kutatua kila aina ya changamoto ikiwemo ndani ya serikali,ndani ya mikoa,ndani ya wilaya,ndani ya tarafa,ndani ya kata,ndani ya vijiji,ndani ya vitongoji na ndani ya familia zetu.Hata hivyo falsafa ya maisha itatupatia viongozi bora kwa taifa letu.

SEHEMU YA 3
Maisha ya watu ni sahihi katika mienendo yao,tukijiua hilo kwamba flani ni mwizi,anahasira,anachepuka sana,anasali sana,anacheza sana,mwanaume kusuka.Tusiwashangae kwani hali yao ya ndani ndiyo inawafanya kuwa hivyo.Na hapa tutajifunza kufanya haya.

TUSIWAHUKUMU,Tusiseme flani msimsaidie kwa kuwa halipi madeni.Nawaambia yeyote afanyaye hayo umepungukiwa na ufahamu na kujihesabia kuwa yeye ni mwenye haki kuliko wengine.
TUSIWATENGE,Mtu anayependwa na watu ni yule anayejali au kuwasaidia na wale waliomchukiza siku za nyuma.Na nawaambia lazima tutatukanwa,najua tutaumia lakini wakati huo tusijibu kitu.Kwani ukipewa zawadi lazima uichukue?Tufanyeni hivyo ili kulinda amani.
TUWASAIDIE;Usishangae mtu aliyekuzulumu miaka iliyopita akija kwako umsaidie.Tuendelea kuwasadia kwasababu yote ya nyuma yatakumbushwa na wema wako.Kanuni ya kumsaidia mtu ni kuwa nacho.Je utamsaidia kile usichokuwa nacho?
TUWAELEKEZE:Tujifunze kutoa ushauri kwa yule anayetaka kushauriwa.Mfano kuchepuka ni kosa,kwanini uendelee kuchepuka wakati kile unacho kipata kwa wake za watu na mke wako anacho?Asipoelewa sisi tunawe maana kwa kosa hilo analolifanya ndilo litakalomadhibu.
TUWASAMEHE.Kwa kuujua ukweli tutaweza kumsamehe hata yule aliyetuumiza jana.Jana umemkuta anamke wako lodge akija kutaka msaada kwako tumsaidie.Kwani kati ya mke wako na yeye nani mwenye kosa,kwa kufanya hivyo tutaukubali ukweli na amani itatawala.

SEHEMU YA 4
Maisha ni amani,furaha na upendo.Ili tuwe na amani ndani ya jamii zetu yatupasa kufanya yafuatayo..

KUTOA HAKUNA MWISHO
Tunajua mvua ilikuwepo toka zamani na inanyesha nyakati zetu je hili si fundisho kwetu?
Unaonaje mtu yeye yule yule umemsaidia leo unga,kesho anakuja anaomba maji,unampa,anaomba karanga unampa,yaani kilakitu akiomba unampa je hiyo sawa na mvua;basi tujifunze kutochoka kusaidia watu kwani kwa kufanya hivyo tutakula matunda ya mema yetu.
TUWE NA MSIMAMO MMOJA:angalia nge asili yake ni kung'ata hata umwokea ndani tanuru la moto lazima tu atakung'ata ukimsongezea moto.Yaani ndio alivyo hata tusiumize kichwa kumuua.Kwa mfano huo tutajifunza kutolipiza kisasi,kubagua watu,tutaacha unzinzi;tutaacha wizi,tutaacha kuogopa.Na tutafanya upande wa kutenda mema kuwa asili yetu na kuitetea asili yetu.

TUWE NA IMANI
Tufanye mambo yetu kwa kuamini kwamba tutafanikiwa,bila kulaumu,bila chuki na mtu hakika tutafanikiwa.

MTAZAMO SAHIHI
Mtazamo wetu ukiwa vizuri tutaishi na watu vizuri,changamoto zikija tuone kwamba tunastahili kuzipa tena kwa sura yenye furaha kwani kwa kila changamoto kuna jambo zuri ndani yake.Kwa kufanya hivyo tutasahau kama kuna matatizo,kuna vilio na tutakuwa watu wa furaha siku zote mpaka kufa kwetu.

Nahitimisha kwa kusema hivi maisha yana amani,furaha na upendo kwani kwa kujifunza kuukubali ukweli ndio utatuzi wa changamoto zote.Nimekuwa mtu wa furaha siku zote kwani furaha ipo ndani ya moyo wangu wala haitokani na mtu yeyote.Nimejifunza kuyaepuka mambo yote yanayoondoa furaha yangu,mpaka sasa nimeshasahau kama kuna kulia,kununa,kukasirika.Nimekuwa mtu wa kupendaza kwa watu wote tena mwenye kupendwa na watu kwa sababu nimeielewa falsafa ya maisha ndio maana nikoona niwaandikie makala hii.
Mwisho nisema kuona furaha katika maisha sio kwamba lazma uwekewe mikono na wachungaji hapana bali ukielewa falfasa ya maisha unaweza ukaishi zaidi ya mchungaji,zaidi ya mashehe,zaidi ya mapadri na maaskofu.kwani kuipata njia ya wongofu sio lazma ukeshe makanisani au misikitini bali kwa kuikubali kweli tunaweza tukaishi maisha ya mbinguni tukiwa duniani.Na si lazima tuombewe ndio tuwe watakatifu bali tunaweza tukaishi kitakatifu hata tukiwa majumbani kwetu.

Mimi ONJO najua nivigumu kwenu kuniona kwa sura,bali yeye asomaye mafundisho yangu,akaelewa na akaishi kwa kutenda atamuona ONJO wa kweli katika maisha yake.

Itafuteni amani,furaha na upendo kupitia fundisho hili.Mimi naamini katika kweli,ninaishi katika kweli na ninaitetea kweli.
Mbarikiwe nyote.View attachment 2585402
nimesoma hapa naisi kunakitu naelewa nitakuwa mpole na kueshim wenzangu
kiukweli mpaka sasa mimi sielewi maisha ni nini?je,sisi watu wahali ya chini tinaishi kweli au ndiyo tunamkufulu mungu kila panapokucha maana masikini hatuishi kulaum kila ukuchao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom