Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,261
Kila ninapowaza kuhusu maisha mengine baada ya haya ya duniani huwa najawa na maswali mengi ambayo sijawahi kupata majibu yake mazuri, Mfano
Swali la kwanza ni tofauti kubwa sana kati ya dini/imani za binadamu kuhusu hayo maisha mengine baada ya haya ya duniani.
Katika dini zote wanazoamini mbingu, maelezo ya aina ya mbingu katika hizo dini zote ni tofauti sana kiasi cha kuzua maswali kutakuwa na mbingu ngapi na kama mungu ni mmoja au miungu wako wangapi.
Swali la pili ni kuhusu wanyama, Sijawahi kupata jibu la kueleweka kuhusu hawa wanyama wanaofugwa na binadamu kama kitoweo au pet pamoja na wanyamapori kama watakuwepo au hawatakuwepo mbinguni. Kuku uliyemchinja ukamla utakutana naye mbinguni? Itakuaje
Jambo la tatu, ni lini hasa hayo maisha mengine baada ya haya yanaanza. Kuna wanaoaimini yanaanza pindi tu pale mtu anapokufa, kuna wanaoaimini yataanza kwa pamoja baada ya mwisho wote wa dunia wa watu kufika kwa pamoja.
Jambo la mwisho ni kama hakuna maisha mengine inakuwa Jambo la kuhuzunisha zaidi na kukosesha raha ukifikiria kwamba mnapoachana na ndungu, jamaa, marafiki na wale unaowapenda baada ya maisha haya ndio imetoka hivyo hakuna kuonana tena. Walioteseka katika dunia hii maisha yao yote ndio imetoka hivyo (hawatapata fursa ya kuimba milele na kutosikia njaa, hamu au mateso wakienda mbingu hiyo, kupata mabikiria na vileo wakienda mbingu hiyo) na watu waliofanya maovu makubwa pia hapa duniani ndio imetoka hivyo baada ya maisha haya.