Maisha ni mafupi sana. Fanya yote yakufurahishayo ikiwa tu huvunji sheria za Mungu wala za nchi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,904
Wakuu kwema!

Sisi Watibeli tunajua kabisa miaka 100 ni michache mno. Alafu fikiria karibu asilimia 95% hatutafikia umri huo. Na hao watakaofika watakiona cha moto.

Maisha ni mafupi ndio maana Watibeli siku zote tunafurahi. Kwetu Furaha ni kuishi kwa amani na Watu wote. Hatuweki vinyongo wala hatunaga chuki. Sio ajabu Watibeli hatuwezi kum-block wala kumu-ignore yeyote kwa sababu ya tofauti zetu iwe kimaumbile, kiakili, kiitikadi n.k.

Tutakufa tukiwa tumetendea Haki zawadi ya maisha tuliyopewa na Mungu wetu. Tutakufa tukiwa hatuna deni. Tutakufa tukiwa hatuhitaji muda wa nyongeza.

Tutafurahia hali zetu kwa muda wote.

Tutafurahia Maumbile yetu na mabadiliko yake kwa muda wote.

Tutafurahia Wahusika wapya na wazamani kila mmoja akija kwa kusudi lake katika maisha yetu. Liwe zuri au baya. Tutafurahia.

Sisi kwetu furaha ni vazi. Tunafurahi na yeyote. Hatudharau yeyote.

Maisha ni mafupi. Na ufupi wake ndio furaha tamu zaidi.

Chochote unachohisi kinakupa furaha ikiwa hakivunji sheria za Mungu na sheria za nchi kifanye. Usiifanye nafsi yako ikawa jela. Usiwe mtumwa wa Watu wengine.

Usimuumizd yeyote isipokuwa yule anayetaka kukuumiza.

Usimuumize yeyote isipokuwa yule anayetenda Uovu kwa makusudi na unauwezo wa kumdhibiti.

Furaha ipo ndani yako. Furaha haitoki nje.
Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom