Mungu hakupi unachotaka

jamaikatz

Member
Jul 11, 2023
51
132
maisha ya mwanadamu ni kama maua huchanua na kusinyaa, wengi wetu tumezaliwa tukiwa na ndoto kibao za mafanikio katika maisha yetu , hakuna mtu asiye penda kuishi maisha mazuri, kila mtu anatamani awe na pesa, jumba, magari na miradi mbalimbali ya kutosha

Nadhani wengi wetu tulipo kuwa bado wadogo katika nyoyo zetu na nyuso zetu tulikuwa tumejenga picha ya maisha yetu ya badae kwamba tutakuwa na maisha mazuri tumejenga nyumba nzuri,tumenunua gari kali la bei mbaya alafu pembeni una mwanamke mzuri. Lakini vyote sivyo bado hatujafanikiwa na tunaendelea kusota na maisha

Siku zote Mungu huwa HAKUPI UNACHOTAKA na anakupa usichotaka ni watu wachache sana ambao wapo kwenye mpango wa Mungu na wakamuomba mahitaji yao wanayo yataka na wakapewa, wengi wetu ndoto zetu nyingi zimeishia njiani kwa sababu tumesha kata tamaa ya maisha.

Sababu maisha ni bahati, maisha ni nasibu mafanikio ya mtu huwa yanakuja automatiki na kila mwanadamu huwa ana road map ya maisha yake yaani mungu anakuwa amesha kuchorea kila kitu kuhusu maisha yako hata ufanye vipi utumie mbinu gani lakini Mungu akipanga amepanga kwamba huyu mtu maisha yake yatakuwa hivi

Embu fikiria una ndoto ya kuwa daktari ila unaishia kuwa mwalimu,
Unataka kuwa injinia unaishia kuwa polisi
Unataka kuwa mwanasheria unaishia kuwa bodaboda
Unataka kumuoa mwanamke fulani ila unaishia kuoa mwingine usiye mdhania
Unapanga nikifungua biashara fulani basi mambo yangu yatanyooka yatakuwa mazuri ila baada ya kufungua mambo yanaenda ndivyo sivyo unaishia kwenye limbi la mawazo kibao.

Lakini haya yote ndio maisha yetu sisi maskini, kwa maana maskini ni wengi kuliko matajiri na wenye mafanikio ni wachache sana tulio wengi ni maskini .

Na baada ya mahangaiko yetu yote duniani lakini mwisho tunaishia kaburini

Ndugu zangu tumtafute sana Mungu kwa bidii ili kila tunacho kitaka tuweze kukipata kwa muda na wakati sahihi

Lakini pia usisahau kuwa sio kila mtu anayepitia nyakati ngumu za kuwa na maisha magumu eti kwamba baadae atapata mafanikio baadae pia unaweza hata ukafa.
 
Mungu anakupa kile ambacho kinachokufaa na kinachokustahili.

Kuna mambo mengine, japo kwa akili ya kawaida yanaweza kuwa ni mazuri, lakini yasikufae wewe au yasikustahili.

inabidi tumshukuru sana Mungu kwa kukosa hayo tuliyoyaomba, kwa maana yangeweza kuwa ndiyo angamizo letu au mateso yetu

Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kila jambo

Tumsifu Yesu Kristu
 
maisha ya mwanadamu ni kama maua huchanua na kusinyaa, wengi wetu tumezaliwa tukiwa na ndoto kibao za mafanikio katika maisha yetu...

Mkuu kwahiyo Mungu ndio kawapangia maisha mazuri ya mafanikio wahalifu wa silaha, dawa za kulevya, utapeli, mafisadi serikalini nk?

Na kawapangia shuruba wale watoto wa kipalestina pale gaza na Somalia, wale vijana kule Sudan na Congo nk?
 
Mungu anakupa kile ambacho kinachokufaa na kinachokustahili.

Kuna mambo mengine, japo kwa akili ya kawaida yanaweza kuwa ni mazuri, lakini yasikufae wewe au yasikustahili...

Mkuu hebu take your time na uende pale Muhimbili jengo la hospitali ya watoto

Kawaangalie wale watoto wenye kansa, matatizo ya moyo nk.

Wale watoto zaidi ya nusu hawatafika umri wa utu uzima watakua wamekufa kwa taabu na mateso makubwa sana kabla magonjwa hayo hayajachukua uhai wao.

Watakao survival maisha yao yataka ya mashaka na taabu kwa side effect za madawa na watakua tegemezi maisha yao yote

HAWA MUNGU KAWAPA KINACHO WAFAA NA KUSTAHILI?

Nenda Kinondoni kuna MADIGALA wauza madawa ya kulevya wanaishi kama wapo peponi vile huku wakihatibu vijana wengi sana kwa madawa ya kulevya

HAWA MUNGU KAWAPA KINACHO WAFAA NA KUSTAHILI?
 
maisha ya mwanadamu ni kama maua huchanua na kusinyaa, wengi wetu tumezaliwa tukiwa na ndoto kibao za mafanikio katika maisha yetu...
Naamini muda mwingine kunyimwa kunaweza kukulinda na kukuepusha na mambo hata wewe mwenyewe ungeyajua ungeomba ubaki tu ulivyo. Tusiwe wepesi wa kulalamika na tusipime neema zetu kwa kuangalia neema za mwingine kwasababu itakuzuia kuona baraka zako na kuishia kujiona huna bahati na kukufuru zaidi.

Tujaribu kuwa watu wa kushukuru sana kuliko kulalamika maana kama unashindwa kutambua kuwa uhai wako tu neema kubwa na utajiri mkubwa ambao kuna matajiri wa mali wanausaka kwa hela nyingi na bado wanaukosa basi sidhani hata kama ukipewa maisha unayoyataka utaridhika nayo ni dhahiri bado utaendelea kulalamika tu!

Tutambue neema tulizojaaliwa nazo kwa sasa na kabla ya kutaka zaidi na unachokiona si cha thamani kwako kwa sasa ukikipoteza ndio utajua thamani yake.
 
Mkuu hebu take your time na uende pale Muhimbili jengo la hospitali ya watoto
Kawaangalie wale watoto wenye kansa, matatizo ya moyo...
Ni ukatili sana.

Tuwape heko binadamu wenzetu wanaojitahidi kuondoa haya maumivu kwa wenye matatizo.
 
maisha ya mwanadamu ni kama maua huchanua na kusinyaa, wengi wetu tumezaliwa tukiwa na ndoto kibao za mafanikio katika maisha yetu...
KIBWAGIZO: ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa, ni nani kwenu ambaye mwanae akimwomba mkata atampa jiwe au akimwomba samaki atampa nyoka? ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watu vitu vyema je si zaidi sana baba yenu wa mbinguni? atawapa mema wale wamchao.

maneno haya yanadhihirisha kwamba, Mungu kuna wakati huwa anakupatia kile kile ulichoomba, lakini endapo anaona kitakudhuru au utamwacha ukikipata, anaweza asikupatie. why? Yakobo 4:3 inasema, Hata mwaomba, wala hampati kwasababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

SWALI KUU: ni maombi gani yatakuwa sahihi ili nijue lazima tu nitajibiwa? Jibu: mtumishi wa Mungu Benny HInn alinifundisha kitu kikubwa sana, yeye anaamini maombi yale ambayo utakuwa na uhakika kwamba utajibiwa yote, ni yale maombi ambayo Roho Mtakatifu amehusika, yaani maombi ya kunena kwa lugha au kuomba kwa Roho Mtakatifu, kwasababu pale Roho Mtakatifu mwenyewe aliaye aba ndani yetu ndiye anakuwa anaomba, ameuteka moyo wako na kuomba pamoja nawe ni sawa ameushika mkono moyo wako anakusogeza kwenye kiti cha enzi, na yeye aijuaye nia ya roho ataopa maombi yale tu yaliyo sahihi na yote yatafika kwa Mungu. NDIO MAANA TUNASEMA MUOKOKE MJAZWE ROHO MTAKATIFU awasaidie kwenye maombi na awaongoza.

WARUMI 8:26 - 28 inasema, Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.

WARUMI 8:14 - 17 inasema, Kwa kuwa wote wanaoogozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia ABA, yaani Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

CONCLUSION: watu wengi wanaomba maombi, hata haya ya kwaresma, lakin hayatajibiwa, wanashinda njaa bure, kwasababu wanafunga kwa kufuata mapokeo ya dini zilizotengenezwa na wanadamu. Mungu hawasikii wenye dhambi ndio maana amesema sikio lake si zito ila maovu yetu yametutenga sisi na yeye. kwahiyo, mnatakiwa kuokoka kwanza, mjazwe Roho Mtakatifu mnene kwa lugha na huyo huyo Roho atawasaidia sio tu kuwaongoza, bali kwenye maombi kama mistari hapo juu ilivyosema, na ukiwa huna Roho wa Mungu wewe sio wake, hata akija leo anakuacha. Mungu awafunulie hili, karibuni kwenye wokovu.
 
Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Hakuna Mungu anayetoa chochote kwa binadamu.

Mungu ni fiction character.

Hayupo katika uhalisia ila katika mawazo ya kufikirika tu, Imaginations just an illusion.
 
Mkuu hebu take your time na uende pale Muhimbili jengo la hospitali ya watoto

Kawaangalie wale watoto wenye kansa, matatizo ya moyo nk.

Wale watoto zaidi ya nusu hawatafika umri wa utu uzima watakua wamekufa kwa taabu na mateso makubwa sana kabla magonjwa hayo hayajachukua uhai wao.

Watakao survival maisha yao yataka ya mashaka na taabu kwa side effect za madawa na watakua tegemezi maisha yao yote

HAWA MUNGU KAWAPA KINACHO WAFAA NA KUSTAHILI?

Nenda Kinondoni kuna MADIGALA wauza madawa ya kulevya wanaishi kama wapo peponi vile huku wakihatibu vijana wengi sana kwa madawa ya kulevya

HAWA MUNGU KAWAPA KINACHO WAFAA NA KUSTAHILI?
Kwanza lazima uelewe kuna kitu kinaitwa fate (something which is destined to happen to you) yaani majaaliwa na kila mtu ana fate yake hapa duniani.

Sasa swali kwanini imekaa hivyo, majibu yake ni from the theological perspective kwamba Mungu alipo umba dunia akaona kila kitu kinafaa na ni chakupendeza kwa lugha laini kazi ya Mungu haina makosa.

Sasa basi, vitu vinavyozungumzwa hapa ni vile ambavyo wewe una viomba, na wengi wetu tunaomba vitu ambavyo pengine tunao wajibu wakuvitafuta kama vile mali, mke, usalama, amani, upendo na ata afya njema.

Sina nia ya kukufuru au kulaumu, matatizo mengi ya watoto wetu pengine yangeweza kuepukika kama tungezingatia kanunu za afya na kufuata maelekezo ya kitabibu. Magonjwa mengine yanayowapata watoto ni ya kurithi au yanatokana na uzembe wa wazazi katika kutunza na kufuata afya ya uzazi. Nakiri pia kwamba matatizo mengine pia yanatokea bila kuwa sababu yoyote na hakuna anayeweza kulaumiwa mfano organ failures and diseases kama cancers.

Ukiacha matatizo yanotokea kwa kujitakia wenyewe kama vile urahibu wa madawa ya kulevya, ngono na ajali kama za bodaboda na nyingine nyingi ambazo zinasababisha madhara makubwa, bado sehemu kubwa ya maisha yetu sisi wanadamu ni majaaliwa ya Mwenye -Enzi Mungu.

Bado naendelea kukusihi, tuendelee kumshukuru Mungu kwakua matendo yake ni makuu na ya ajabu
 
umeandika vitu kishabiki bila ya kuwa na facts na data

Mungu hana ubaguzi, huwapa mvua wema na wabaya

Bwana wetu Yesu Kristu alisema kabisa kwamba wenye afya hawaitaji tabibu bali wagonjwa na hakuja kwaajili ya wema bali waovu ili wapate kutubu (Kasome injili ya Mtakatifu LUKA 5:31-32)

Inapaswa ujue kwamba siyo vyema kujistahilisha neema za Mungu kwa kudhani kwamba kitendo fulani cha kiiimani kina kustahilisha zaidi kuliko watu wengine. Kwa maana, Mungu wetu anatujua kabla ya sisi kuzaliwa na walio wake anawajua pia.

Bwana wetu Yesu Kristu alisema hivi: (Kasome Mtakatifu LUKA 14:8-11)

8.Mtu akiku alika harusini, usikae kwenye kiti cha mgeni wa heshima. Inaweze kana kuwa amealika mheshimiwa akuzidiye, 9 na yule aliyewaalika ninyi wawili akaja kukuambia, ‘Tafadhali mpishe huyu bwana.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kwenda kukaa katika kiti cha nyuma kabisa. 10. Badala yake, unapoalikwa, chagua kiti cha nyuma; na mwenyeji wako akikuona atakuja akuambie, ‘Rafiki yangu, njoo kwe nye nafasi ya mbele zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wote. 11 Kwa maana kila mtu anayejitukuza atash ushwa naye ajishushaye atatukuzwa.

Pia nenda kasome Mathayo Mtakatifu 7:21

Kwamba siyo wote wasemao bwana bwana watauona ufalme wa mbingu bali wale tu wanaotimiza matakwa ya baba yake aliye mbinguni

Mwisho kabisa nakupiga na kitu kizito kabisa ili uache kujistahilisha uokovu

Yohana 10:14

Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu

Swali je Yesu anakufahamu?
 
maisha ya mwanadamu ni kama maua huchanua na kusinyaa, wengi wetu tumezaliwa tukiwa na ndoto kibao za mafanikio katika maisha yetu , hakuna mtu asiye penda kuishi maisha mazuri, kila mtu anatamani awe na pesa, jumba, magari na miradi mbalimbali ya kutosha

Nadhani wengi wetu tulipo kuwa bado wadogo katika nyoyo zetu na nyuso zetu tulikuwa tumejenga picha ya maisha yetu ya badae kwamba tutakuwa na maisha mazuri tumejenga nyumba nzuri,tumenunua gari kali la bei mbaya alafu pembeni una mwanamke mzuri. Lakini vyote sivyo bado hatujafanikiwa na tunaendelea kusota na maisha

Siku zote Mungu huwa HAKUPI UNACHOTAKA na anakupa usichotaka ni watu wachache sana ambao wapo kwenye mpango wa Mungu na wakamuomba mahitaji yao wanayo yataka na wakapewa, wengi wetu ndoto zetu nyingi zimeishia njiani kwa sababu tumesha kata tamaa ya maisha.

Sababu maisha ni bahati, maisha ni nasibu mafanikio ya mtu huwa yanakuja automatiki na kila mwanadamu huwa ana road map ya maisha yake yaani mungu anakuwa amesha kuchorea kila kitu kuhusu maisha yako hata ufanye vipi utumie mbinu gani lakini Mungu akipanga amepanga kwamba huyu mtu maisha yake yatakuwa hivi

Embu fikiria una ndoto ya kuwa daktari ila unaishia kuwa mwalimu,
Unataka kuwa injinia unaishia kuwa polisi
Unataka kuwa mwanasheria unaishia kuwa bodaboda
Unataka kumuoa mwanamke fulani ila unaishia kuoa mwingine usiye mdhania
Unapanga nikifungua biashara fulani basi mambo yangu yatanyooka yatakuwa mazuri ila baada ya kufungua mambo yanaenda ndivyo sivyo unaishia kwenye limbi la mawazo kibao.

Lakini haya yote ndio maisha yetu sisi maskini, kwa maana maskini ni wengi kuliko matajiri na wenye mafanikio ni wachache sana tulio wengi ni maskini .

Na baada ya mahangaiko yetu yote duniani lakini mwisho tunaishia kaburini

Ndugu zangu tumtafute sana Mungu kwa bidii ili kila tunacho kitaka tuweze kukipata kwa muda na wakati sahihi

Lakini pia usisahau kuwa sio kila mtu anayepitia nyakati ngumu za kuwa na maisha magumu eti kwamba baadae atapata mafanikio baadae pia unaweza hata ukafa.
Nadhani Mungu ameweka ground sawa tutafute maisha. hivo ni juhudi zako kutafuta uelekeo sahihi wa kutafuta maisha. maisha siyo ya kukaa na kusubiri yaje mazuri. pia unaweza kupambana in a wrong direction, let us be flexible
Kuna watu kwa kulima tu wametoboa
kuna mzee mmoja kijijini kwetu alikuwa, tangu nimezaliwa nikamkuta ni rika la mzee wangu ,anaondoka kila siku asubuhi akiwa na karai lile la chuma na koleo/spade anaenda mgodini hakufanikiwa kupata kitu cha maana
Yupo mwingine alifiwa na wazazi akalelewa na babu na bibi yake ,akapambana baada ya kujitambua akawa na maisha kiasi chake
Urithi pia waeza kukusogeza mahali
usitegemee watoto wa matajiri wasote kama sisi
 
Mkuu hebu take your time na uende pale Muhimbili jengo la hospitali ya watoto

Kawaangalie wale watoto wenye kansa, matatizo ya moyo nk.

Wale watoto zaidi ya nusu hawatafika umri wa utu uzima watakua wamekufa kwa taabu na mateso makubwa sana kabla magonjwa hayo hayajachukua uhai wao.

Watakao survival maisha yao yataka ya mashaka na taabu kwa side effect za madawa na watakua tegemezi maisha yao yote

HAWA MUNGU KAWAPA KINACHO WAFAA NA KUSTAHILI?

Nenda Kinondoni kuna MADIGALA wauza madawa ya kulevya wanaishi kama wapo peponi vile huku wakihatibu vijana wengi sana kwa madawa ya kulevya

HAWA MUNGU KAWAPA KINACHO WAFAA NA KUSTAHILI?
yaani mtu ku conclude kuwa kila jambo limepangwa na Mungu nadhani haipo sawa
 
Kwanza lazima uelewe kuna kitu kinaitwa fate (something which is destined to happen to you) yaani majaaliwa na kila mtu ana fate yake hapa duniani.

Sasa swali kwanini imekaa hivyo, majibu yake ni from the theological perspective kwamba Mungu alipo umba dunia akaona kila kitu kinafaa na ni chakupendeza kwa lugha laini kazi ya Mungu haina makosa.

Sasa basi, vitu vinavyozungumzwa hapa ni vile ambavyo wewe una viomba, na wengi wetu tunaomba vitu ambavyo pengine tunao wajibu wakuvitafuta kama vile mali, mke, usalama, amani, upendo na ata afya njema.

Sina nia ya kukufuru au kulaumu, matatizo mengi ya watoto wetu pengine yangeweza kuepukika kama tungezingatia kanunu za afya na kufuata maelekezo ya kitabibu. Magonjwa mengine yanayowapata watoto ni ya kurithi au yanatokana na uzembe wa wazazi katika kutunza na kufuata afya ya uzazi. Nakiri pia kwamba matatizo mengine pia yanatokea bila kuwa sababu yoyote na hakuna anayeweza kulaumiwa mfano organ failures and diseases kama cancers.

Ukiacha matatizo yanotokea kwa kujitakia wenyewe kama vile urahibu wa madawa ya kulevya, ngono na ajali kama za bodaboda na nyingine nyingi ambazo zinasababisha madhara makubwa, bado sehemu kubwa ya maisha yetu sisi wanadamu ni majaaliwa ya Mwenye -Enzi Mungu.

Bado naendelea kukusihi, tuendelee kumshukuru Mungu kwakua matendo yake ni makuu na ya ajabu

Mkuu Kwahiyo unawaangushia zigo la lawama wazazi?

Your not seriously

Nimekwambia take your time, andaa laki moja tu nenda pale hospitali ya watoto katoe msaada kisha muulize dr ni kwa nini watoto wanazaliwa na kansa, matatizo ya moyo, mifumo ya chakula, hewa, ulemavu, kuungana nk nk

Mungu hampi wala kumyima mtu kitu chochote kwasababu angeanza na watoto wale ambao wanaomba na kutamani wawe wazima kama wenzao lakini kwa bahati mbaya ama watakufa kwa mateso au wataishi kwa mateso maisha yao yoye...... and God did absolutely NOTHING about
 
Tuliza wenge mkuu, kunywa maji kwanza, Mungu siyo Athumani, njia zake siyo njia zetu, maamuzi yake si maamuzi yetu, vyote afanyavyo ni vya kupendeza, tumrudishie sifa na utukufu

Mkuu kwa mtazamo HALISI Mungu mnaye mtaja kutoka kwenye vitabu vyenu ni JITU MOJA KATILI SANA

Anawezaje kuruhusu mtoto mchanga asiye jua lolote azaliwe na saratani mbaya kabisa itakayo mtesa maisha yake yote na akaacha wahalifu wakubwa wanao “mkufuru” wanakula bata kama wapo “peponi”?

Hakuna Mungu mwenye sifa mnasema anazo anaweza kuwa na njia za kikatili namna hii wakati uwezo anao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom