kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
Basi mimi mawazo yangu yote yalikuwa katika kuvuliana samaki.Khanga zimetolewa China, alitaka andika "MAISHA KUVUMILIANA"
Pamoja na kukosea vile bado kasema ukweli, kwani bila kuvuliana hakuna uzazi, na bila uzazi hakuna maisha. Mficha uchi ....
Nimecheka hadi basi!
kwanza hicho ni kitenge au shuka au kanga?
khanga
jamaa wameamua kuitandika meza ya baa nini! maana hiyo lazima mama waogope kuivaa...inaweza kuletea kila mtu kukutongoza bure,akidhani u mwepesi wa kuvua.
Si unajua tena utendaji usio makini? Maandishi haya yalihitaji kusomwa (proof reading) kabla ya kuanza kuchapa hizo khanga.Hili ni kosa la kiufundi ila watu wanaweza kutafsiri kuwa ndo mipasho ya kwenye Khanga!sasa huyu aliyetunga hili neno alikua na maana gani ni kuvuliana nini maana kanga mpaka watoto wanavaa kweli hii ni tungo tata!kanga zinavaliwa mpaka na wanaume!
anyway ni tungo tata ila sema kwasababu ni vazi lakina mama ingawa na kina baba huwa wanashona mashati ya kanga hizi naona kwa watoto wao wakiona watajiuliza mama maisha ni kuvuliana nini!!!!
Si unajua tena utendaji usio makini? Maandishi haya yalihitaji kusomwa (proof reading) kabla ya kuanza kuchapa hizo khanga.Hili ni kosa la kiufundi ila watu wanaweza kutafsiri kuwa ndo mipasho ya kwenye Khanga!
Una uhakika gani kama hawakumaanisha hiyo sentensi? Mimi naona hiyo ni dhamira kabisa, ingekosewa isingeingia sokoni bana!...Nahtaji moja nimpelekee mama nanihii pale mtaa wa pili, teh teh