Maisha baada ya kifo

Sio kweli kwani akili salama haikatai ukweli hata siku moja......

Tatizo maelezo yenu hayaja shikana,mkiulizwa maswali kulingana na yale mnayoyaelezea mnashindwa kuyajibu.

Sasa kwanini mnaendelea kuyashikilia mawazo ambayo hamuwezi kuyatetea haya ndio maajabu niyaonayo kwenu.

Nipo........
Level ya concious yako hairuhusu utasumbua watu Tu

Nimejuaje?_Kwa kupitia kuuliza kwako.

Kiwango cha ufahamu alichotumia mdau kuainisha mawazo ya Elimu hiyo

Ungekuwa katika level ya spiritual realm kama yake usingeuliza ungekaa kimya

Naamini hata mtume wako angekaa na kumsoma mdau

Angepiga magoti na kushukuru Mungu wenu kuwa ule uma bora ulio ahidiwa katika mwisho wa kipindi chake basi bila shaka ndio huu

Au ni shida sana anapotamka 3D, 4D na 5D ila angetamka peponi ungeelewa.!?
 
Kabla ya dini gani mkuu? Unakusudia hizi zinazoeleza tokea habari za binaadamu wa kwanza?

Na hao mababu zetu wao waliyajuaje masuala ya Mungu? Mara zote nimekuwa nikijiuliza hili swali.
Kwa kawaida ya maumbile bin adam hukiri kwamba kuna muumba kabla hata ya kupata mwongozo kuhusu huyo muumba, na hili hutokana na jinsi alivyoumbwa yeye binafsi pamoja na vile vilivyo mzunguka mfano anga lilivyoumbwa au ardhi ilivyotandikwa milima miti pamoja na bahari, hivi ni vitu ambavyo bin adam aliyekamilika akijitazama yeye pamoja na vinavyomzunguka basi hukiri ni lazima kuna muumba, changamoto inakuja kwamba ni nani muabudiwa halisi, hapo ndio utakuta tunagawanyika.
 
Hajulikan
Mkuu wewe ndio humjui, bali yeye anakujua mwanzo wako na mwisho wako na anayajua mafikio yako, na amedhibiti matendo yako toka day one till your last breath na atayaweka mbele yako siku ikifika na hutoweza kukanusha.
 
Mkuu ndio maana nimekupa swali hapo juu je lipi kati ya haya tuamini?
1)Mungu mwenyewe anaamua watu gani waende peponi na watu gani waende motoni. Kwavile yeye ndiye anayemuumba mtu na pia kabla hajamleta mtu duniani anajua mwanzo hadi mwisho wa huyo mtu utakuwaje. (Anajua alichokipanda na kitakachoota)

Au

2) Mungu hajui mwanzo(kabla ya mtu kuzaliwa)na mwisho wa mtu utakuaje hivyo jitihada au makosa yaweza kubadilisha hatima ya mtu (anajua alichokipanda ila kitachoota hajui)
Habari yako Mheshimiwa, Swali ulilouliza ni zuri na mchanganuo wake upo hivi.

Kuhusu yeye Mungu anafahamu kila kitu, ujuzi wake umezunguka kila kitu anafahamu ya kabla, ya yatakavyokuwa na baada ya yatakavyokuwa.

Tuje kwenye msingi wa swali lako, ni kweli Mungu anafahamu wa Motoni na Peponi ila si yeye aliyepanga hayo matokeo bali watahiniwa ndiyo waliyochagua hayo makazi. Msingi wa Imani yangu katika hilo upo hivi, kuna hali binadamu tumepewa nayo ni utashi wa kujiamulia mambo na katika hilo yeye Mungu hatuingilii, pengine kwa nini? Kwa sababu ametupa hekima na elimu pasipo kusahau kwamba una utashi wa kujiamulia juu ya utakayofanya. Kisha akatupa uhai ambao ndiyo huu mwisho wa siku tunarudi kwake kwa njia ya kifo.

Kwa vile yeye Mungu ni mjuzi wa yote anafahamu bwana "Fulani" atazaliwa kipindi Fulani na katika makuzi yake atashika njia iliyokuwa mbali na yangu kwa matashi yake yeye mwenyewe kwa sababu ndipo alipoamua yeye kuelekea, kwa muktadha huo amejidhulumu mwenyewe. Usisahau ya kwamba tuna Uhuru wa kuishi kwenye maisha haya, imma kumkufuru au kumshukuru ila mwisho wa siku marejeo kwake.

Na hayo yote ni kwamba Mungu anatuangalia kwa kuona ni yupi atakayetii amri yake pindi alipoiamrisha; kwa sababu akitaka utii amri yake utatii tu na huo uwezo anao, lakini haitokua utiifu bali ni kulazimisha na yeye Mungu hataki kulazimisha bali anaangalia ni yupi mtiifu kati yetu kwake yeye.
 
Mkuu hivi anayemuumba mwizi, mzinifu, tapeli, n.k ni nani kama siyo yeye Mungu mwenyewe? Kitendo cha Mungu kujua kuwa mustakabali wa mtu atakuwa ni mzinzi kabla ya hata huyo mtu hajazaliwa basi inamaana kapanga yeye Mungu huyo mtu awe mzinzi. Hivi mfano Mungu angekuuliza kuwa #Hammaz# nakupeleka duniania ila utakuwa mwizi na mwisho wa siku utakufa ukiwa wa motoni je ungelikubali uletwe duniani?

Kitendo cha Mungu kujua litokealo kwa mtu kabla hata ya kuzaliwa maana yake kapanga yeye mtu aishije.

Mfano wewe ni fundi ujenzi na wakati umeezeka nyumba bati, ukaangalia juu ukaona kuna tobo ambalo mvua ikinyesha nyumba itakuwa inavuja, lakini hujaliziba lile tundu; maana yake umepanga nyumba iwe inavuja.
 
mkuu hongera sana kwa swali lako japo lina utata na wengi huenda chaka kwa kufuata mafundisho ya vitabu vya dini..

Kwanza kabsa naomba nikujulishe kuwa ,katika ulimwengu unaoishi kuna layer nyingi sana zinazoruhusu life proliferation( muendelezo wa maisha) kulingina na concious awareness ya kiumbe atakayokufa akiwa nayo..

Siku nikipata muda nitatolea ufafanuzi juu ya parallel universe na zina kazi zake katika kuruhusu maisha yaendelee..
hapa upo sawa kabisa kitu kingine mtu mpaka afe ni kwamba amepingana na law za nature
kama wanadamu tungeweza kufuata sheria za nature basi tungeishi milele assumption tu lkn
:D:D:D
 
:D :D :D mkuu huu ulimwengu unatuchezesha kama midoli aise...
 
Mengine ni mapokeo. Maisha baada ya kifo ni yale yanayoendelea duniani. Afaye hurudia kuwa udongo ambo hurutubisha vilivyo hai
 
kwa hiyo udongo nao ni kiumbe coz umesema maisha baada ya kifo ni kujeuka udongo
 
Mkuu hivi anayemuumba mwizi, mzinifu, tapeli, n.k ni nani kama siyo yeye Mungu mwenyewe? Kitendo cha Mungu kujua kuwa mustakabali wa mtu atakuwa ni mzinzi kabla ya hata huyo mtu hajazaliwa basi inamaana kapanga yeye Mungu huyo mtu awe mzinzi. Hivi mfano Mungu angekuuliza kuwa #Hammaz# nakupeleka duniania ila utakuwa mwizi na mwisho wa siku utakufa ukiwa wa motoni je ungelikubali uletwe duniani?

Kitendo cha Mungu kujua litokealo kwa mtu kabla hata ya kuzaliwa maana yake kapanga yeye mtu aishije.

Mfano wewe ni fundi ujenzi na wakati umeezeka nyumba bati, ukaangalia juu ukaona kuna tobo ambalo mvua ikinyesha nyumba itakuwa inavuja, lakini hujaliziba lile tundu; maana yake umepanga nyumba iwe inavuja.
"Utashi" ni uwezo wa kuamua, ni uwezo wa kuchagua na ni uwezo unaoongoza kwa sababu kwenye kuchagua au kuamua ndipo utakapoelekea na ndipo utakapojiongoza. Yote hayo ni kwa sababu ya "Utashi" hali ya maumbile ya kiasili ambayo tunayo bindamu. Kwa kila kitendo utakachokifanya katika maisha yanatokana na maamuzi yako na ile nguvu ya kufanya maamuzi na kukielekea kitu huo ndiyo "Utashi" kwa maana unaamua kufanya.

Mantiki ya kuanza na msamiati wa neno Utashi ni ili katika tunachokijadili tupate kuwa pamoja. Fahamu ya kwamba katika mambo ambayo binadamu anayoyaridhia kuyafanya huwa yanatokana na maamuzi yake yeye mwenyewe mwanadamu, na katika hilo Mungu huwa hamuingilii au kumlazimisha au awe ni mwenye kumfanya binadamu awe hivi ama vile. Mungu anachoangalia ni utiifu wetu kwake yeye unaotokana na amri zake. Na amri ni kutekeleza kile ulichoamrishwa sasa kukubali au kukataa ni maamuzi ya aliyeamrishwa. Halikadhalika ndivyo hali ilivyo vivyo hivyo, Mungu kwa nguvu alizokuwa nazo yeye zisizokuwa na ukingo wala mithili ni zenye kujua kabla ya, wakati husika wa, na baada ya. Kwa hiyo kwa kupitia matashi hali ambayo ametuumbia yeye kiasili kwa hilo, yeye Mungu anafahamu ya kwamba mja wangu huyu atakua ni mwenye kushika njia isiyopendeza kwenye jamii na kwangu pia kutokana na matumizi mabaya ya Utashi wake au kuna mja wangu atakuja katika zama Fulani lakini matashi yake atayatumia vizuri na atakuwa ni mwenye kupendeza kwenye jamii na kwa yeye Mungu atapendezwa naye. Hapangi uwe mwema au mbaya ila anafahamu kwamba huyu bwenyenye atakuwa ni malighafi mbovu na yote ni kwa sababu atautumia vibaya Uhuru wake.

Unaweza kuuliza pengine kwa nini alimuumba mtu wa namna hii kama alitambua atakuwa ni muovu ijapokuwa yeye Mungu hakumpangia awe muovu. Dhana/Mantiki ya swali hili inatubidi turejee katika dhana/mantiki ya kwa nini tumeumbwa, kwa Dhana/mantiki ya kwa nini tumeumbwa kwa maana ya aliyetufanya tuwepo ni lazima itajipa kuna mission/sababu maalum ametuumbia ili tuweze kuitekeleza. Sasa matumizi ya Utashi, ya Uhuru tuliyokuwa nao na mission tuliyopewa mwisho wa siku tutarudi kwa aliyetuleta na aliyetupa hiyo mission ili tujijue sisi ni wa namna gani.

Tufahamu ya kwamba Mungu hatuingilii kwenye utashi wetu.
 
Kumuumba mtu ambaye anatambua kuwa atakuwa ni muovu maana yake ni kwamba amepanga awe muovu kama hakupanga awe muovu kwanini asimuumbe huyo mtu awe mkamilifu? Umezungumzia swala la utashi, je anayeumba mtu mwenye utashi mdogo ni nani?

Na kwavile Mungu alishajua kuwa huyo mtu atakuwa muovu akiletwa duniani; inamaana hata ashuke Yesu kumuhubiria au mtume Muhamad (S.A.W) ampe mawaidha kiasi gani hakutobadilisha hatima ya mtu huyo.
 
Pengine lugha ya mifano inaweza kusaidia katika hili.

Ozone layer inasaidia kupunguza makali ya mionzi ya Jua pamoja na athari yake kufika moja kwa moja Duniani, na inazuia hiyo mionzi takribani 97%-99%. Lakini shughuli za binadamu zinaiathiri Ozone layer. Kwa mfano human made chemicals kama Chlorine au bromine zina deplete ozone layer at supersonic speed na hii ni hatari kwa viumbe tunaoishi kwenye hii Dunia.

Turejee kwenye mada yetu sasa, na Mimi kabla ya kujibu swali lako nitakuuliza swali kwa muktadha wa dibaji ya juu ( ya kwanza) hapo. Mungu amemuumba binadamu hali ya kuwa anafahamu ataharibu Ozone layer, Kwa hiyo Mungu amemuumba mwanadamu ili mwanadamu ajimalize mwenyewe? Kwa sababu anajua ataiharibu hiyo ozone layer si ndivyo hivyo?
 
Jibu ni rahisi tu ni kwamba ndivyo. Kwasababu
1. Mungu ni yeye ndiye muundaji, Sasa kama ni muundaji na anauwezo wa kutabiri na kujua athari ya kile anachokiunda mbeleni kitafanya nini lakini kama akiacha bila kurekebisha mapungufu inamaana kaamua kiwe na mapungufu.

Ikiwa wewe ni muundaji wa magari na umeunda gari halafu unajua kabisa kuwa mfumo wa umeme kwenye gari haukukaa sawa na inaweza kusababisha gari kuwaka moto ila hukuparekebisha inamaana umeamua gari lije liwake moto.

2. Akili kwa binadamu inaumbwa na Mungu ambapo wewe umetumia neno utashi, hii akili ni operating system kwa binadamu yeyote yule asa kwanini Mungu asimuumbe kila mtu awe na operating system iliyokamilika?
 
Sasa kama unafahamu ozone layer ni nini, umuhimu wake ni upi, na inaathiriwa na nini, na unafahamu ni kipi cha kufanya kuiathiri na ni kipi cha kufanya kuilinda na hata kama ikiathirika unafahamu ni jinsi gani ya kudhibiti hicho kinachoathiri tabaka la ozone.

Sasa hapo utamlaumu vipi aliyekupa hekima, maarifa na elimu ya namna hiyo? Kama unaufahamu wa hivyo? Uharibifu unaufanya wewe kwa matashi yako halafu unamsingizia aliyekupa huo ujuzi wa wewe kuyatwaa mazingira yako?!

Unaelewa ninapoandika neno Utashi?

Halafu ni nani aliyekuambia Mungu ana mapungufu? Tangu ulipozaliwa mpaka sasa hivi umeshawahi pata kusikia tu Dunia imetoka kwenye Orbit yake na kuelekea pasipojulikana? Unafahamu kani gani iliyopo baina ya Jua na sayari katika mfumo wetu wa Jua unaosaidia sayari zisitoke kwenye orbit zake? Nidhamu na kanuni ya usiku na mchana ulishaiona ikibadilika? Au kwa vile una lala, unaamka, unaandika unachojisikia, unaendelea na mambo yako kama kawaida basi unafanya unachojisikia tu?
 
Sasa hapo utamlaumu vipi aliyekupa hekima, maarifa na elimu ya namna hiyo? Kama unaufahamu wa hivyo? Uharibifu unaufanya wewe kwa matashi yako halafu unamsingizia aliyekupa huo ujuzi?!

Unaelewa ninapoandika neno Utashi?
Ninaelewa. Tunapopishana wewe ni sehemu moja, labda niende nawe taratibu. Je Mungu anapomuumba mtu; anamuumba kwa utashi wa kiwango gani? Na je kiwango cha utashi kwa kila binadamu ni sawa?
 
Nakuuliza tena unafahamu maana ya Utashi?

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford Toleo la 3, maana ya Utashi ni hiari ya kutenda.

Wewe si unatangamana na watu katika jamii, katika kutangamana nao hebu nieleze umeshawahi kukutana na mtu mwenye limit ya hiari? Au huyu ana kiwango flani cha hiari?

Swali lako hilo tu wewe mwenyewe unalionaje?

Unafahamu ninachokiandika lakini?
 
Sasa kama unafahamu ozone layer ni nini, umuhimu wake ni upi, na inaathiriwa na nini, na unafahamu ni kipi cha kufanya kuiathiri na ni kipi cha kufanya kuilinda na hata kama ikiathirika unafahamu ni jinsi gani ya kudhibiti hicho kinachoathiri tabaka la ozone.

Sasa hapo utamlaumu vipi aliyekupa hekima, maarifa na elimu ya namna hiyo? Kama unaufahamu wa hivyo? Uharibifu unaufanya wewe kwa matashi yako halafu unamsingizia aliyekupa huo ujuzi wa wewe kuyatwaa mazingira yako?!

Unaelewa ninapoandika neno Utashi?

Halafu ni nani aliyekuambia Mungu ana mapungufu? Tangu ulipozaliwa mpaka sasa hivi umeshawahi pata kusikia tu Dunia imetoka kwenye Orbit yake na kuelekea pasipojulikana? Unafahamu kani gani iliyopo baina ya Jua na sayari katika mfumo wetu wa Jua unaosaidia sayari zisitoke kwenye orbit zake? Nidhamu na kanuni ya usiku na mchana ulishaiona ikibadilika? Au kwa vile una lala, unaamka, unaandika unachojisikia, unaendelea na mambo yako kama kawaida basi unafanya unachojisikia tu?
Sijasema Mungu ana mapungufu bali alichokiumba ndio chenye mapungufu na amejua kuwa kabisa kuwa kipi kitatokea lakini amekiacha ina maana ameamua yeye Mungu kitokee. Ndio maana nimekupa mfano wa fundi ujenzi anayejenga nyumba kisha akagundua kuwa juu kwenye bati kuna matundu ambayo mvua ikinyesha nyumba itakuwa inavuja. Lakini fundi huyu mbali kugundua huo uwazi lakini hayazibi hayo matundu kwanini?
Mfano huo ni sawa na Mungu ambaye anajua kabla hata hajamleta duniani mtu X, kuwa akienda duniani atakuwa ni mzinzi na mwizi na ataenda motoni lakini bado kamleta duniani hivyo hivyo wakati alikuwa na uwezo wa kumuumba asiwe mwizi na mzinzi?
 
Level ya concious yako hairuhusu utasumbua watu Tu

Nimejuaje?_Kwa kupitia kuuliza kwako.

Kiwango cha ufahamu alichotumia mdau kuainisha mawazo ya Elimu hiyo

Ungekuwa katika level ya spiritual realm kama yake usingeuliza ungekaa kimya

Naamini hata mtume wako angekaa na kumsoma mdau

Angepiga magoti na kushukuru Mungu wenu kuwa ule uma bora ulio ahidiwa katika mwisho wa kipindi chake basi bila shaka ndio huu

Au ni shida sana anapotamka 3D, 4D na 5D ila angetamka peponi ungeelewa.!?
Nacheka sana bro. Usitumie nguvu bro,bila shaka maswali yangu umeyaona,naomba uyajibu kama wewe unasema kweli.

Tatizo lenu mnakariri sana,yaani mmaongea mamboa amabayo kwa yenyewe hayaeleweki.

Kaka jibu maswali yangu niliyomuuliza mtoa mada.

Kaka nikisema AKILI salama ni neema kubwa sana,sasa nyinyi akili zenu zimechafuka,ni jukumu lenu kuzisafisha mkipenda na kama msipoamua kubadilika mtabaki hivyo hivyo mpaka kufa.

Ukija njoo na majibu ya maswali niliyomuuliza mtoa mada.
 
Back
Top Bottom