Habari yako Mheshimiwa, Swali ulilouliza ni zuri na mchanganuo wake upo hivi.
Kuhusu yeye Mungu anafahamu kila kitu, ujuzi wake umezunguka kila kitu anafahamu ya kabla, ya yatakavyokuwa na baada ya yatakavyokuwa.
Tuje kwenye msingi wa swali lako, ni kweli Mungu anafahamu wa Motoni na Peponi ila si yeye aliyepanga hayo matokeo bali watahiniwa ndiyo waliyochagua hayo makazi. Msingi wa Imani yangu katika hilo upo hivi, kuna hali binadamu tumepewa nayo ni utashi wa kujiamulia mambo na katika hilo yeye Mungu hatuingilii, pengine kwa nini? Kwa sababu ametupa hekima na elimu pasipo kusahau kwamba una utashi wa kujiamulia juu ya utakayofanya. Kisha akatupa uhai ambao ndiyo huu mwisho wa siku tunarudi kwake kwa njia ya kifo.
Kwa vile yeye Mungu ni mjuzi wa yote anafahamu bwana "Fulani" atazaliwa kipindi Fulani na katika makuzi yake atashika njia iliyokuwa mbali na yangu kwa matashi yake yeye mwenyewe kwa sababu ndipo alipoamua yeye kuelekea, kwa muktadha huo amejidhulumu mwenyewe. Usisahau ya kwamba tuna Uhuru wa kuishi kwenye maisha haya, imma kumkufuru au kumshukuru ila mwisho wa siku marejeo kwake.
Na hayo yote ni kwamba Mungu anatuangalia kwa kuona ni yupi atakayetii amri yake pindi alipoiamrisha; kwa sababu akitaka utii amri yake utatii tu na huo uwezo anao, lakini haitokua utiifu bali ni kulazimisha na yeye Mungu hataki kulazimisha bali anaangalia ni yupi mtiifu kati yetu kwake yeye.