Maisha baada ya kifo

Mtu huwa hatambui kuwa amekufa pale anapokufa. Yeye hujihisi anaota anakufa, anajihisi analia, anaoshwa, anafungwa na anateremshwa kaburini.
Bado anajihisi kuwa anaota anapofunikwa na mchanga. Kisha hulia kwa makelele na hakuna anae msikia.


Baadae kila mtu anapotawanyika na ameachwa pekee chini ya ardhi, Mungu huirudisha roho yake. Anafungua macho na kuamka kutoka "ndoto yake mbaya". Mwanzoni, hufurahi na kushukuru kuwa alikuwa anaota tu, na sasa ameamka kutoka usingizini.


Kisha hujigusa mwili wake ambao utakuwa umefunikwa na kitambaa cheupe,na kwa mshangao hujiuliza "shati/gauni langu liko wapi?"
Kisha ana anza kujihisi "niko wapi?" "hii ni sehemu gani?" Mbona kuna harufu ya udongo kila mahali? Ni nini haswa ninacho kifanya hapa?
Hapo ndipo atakapo anza kugundua kuwa yuko chini ya ardhi na alicho kihisi haki kuwa ndoto!


Ndiyo, anagundua kuwa ni kweli yeye amekufa, na amezikwa.
Anapiga kelele kadri anavyoweza kuwaita watu waliokuwa karibu nae ambao wangeweza kumuokoa:
"baba"
"mama"
"kaka"
"dada"
"rafiki"

Hakuna anaemjibu. Kisha anagundua kuwa Mwenyezi Mungu ndio tegemeo lake pekee. Akilia na kumuita huku akimuomba msamaha :
...
Eee Mwenyezi Mungu ...
Nisamehe mimi !!!

Anaita akiwa na hofu kubwa,ambayo hakupata kuwa nayo alipokuwa hai .

Kama alikuwa mtu mwema na mcha Mungu, malaika wawili wakiwa na uso ulio na furaha watamkalisha na kumliwazana kumhudumia vizuri.

Kama alikuwa mtu mbaya na hakuwa mcha Mungu, malaika wawili watamwongozea hofu yake na kumpa mateso kufuatana na amali zake mbaya.

Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu, dhambi za baba yangu, mama yangu, mke/mume wangu na wanangu na jamaa zangu na marafiki.

Ewe Mwenyezi Mungu , usiuchukue uhai wangu ila pale nitakapo kuwa tayari kukutana nawe.



Copied, Edited and Pasted.
 
bro kumbuka Mungu aliwapa elimu mitume na manabii na kuwatuma ili waje watufundishe na kumjua yeye (Mungu)
Hata mitume yote hiyo elimu awajafunuliwa,sheteni mmoja -mitume 25 na bado watu wanapotea,yote anayajua Mungu binadamu subiri ufe utayaona
 
Naomba kuuliza: hivi kabla ya Anikajema hajazaliwa, je Mungu anatambua kuwa huyu Anikajema atakuwa na tabia fulani au ataishi maisha fulani ambayo mwisho wa siku atakufa akiwa mtu wa motoni au wa peponi?
Mkuu hili swali nilakumuuliza mhusika mwenyewe Bwana Yesu.
Ninachojua Mimi Mungu Anaujua Mwisho wa MTU mbaya na mwisho wa MTU mwema .
Kuna njia mbili za kufuata niww tu kuamua wapi uelekee

Swali kama hilo ukiliuliza huwa linakosa majibu yenye logic kwa sababu swali linamhusu muumbaji.

Maana ukifikiria Mungu kama anajua mwanzo na mwisho wangu (inamaana kaniumba automatic Mimi niwamotoni); lakini je!; mbona kakupa Akili chaguzi??

Ukijiuliza Kama Mungu hajui mwanzo na mwisho wangu inamaana yey kuna vitu haviwezi?(Lakini mbona kakutumia mitume na hata Yey kuja kuwafundsha watu jinsi ya kuishi vema?))

Ukweli Ni kwamba Sisi tumeumbwa ili tutende mema ( kama tunavyopanda mahindi shambani ili yazae) ndivyo tuluvyopandwa Duniani ili tutende mema (unapopanda mahindi unayapalilia yoote na siku ya kuvuna utayachagua yaliyozaa tu na kuyahifadhi vzur yasiozaa unayachoma moto) ndivyo sisi zao LA Mungu ukweli Ni kwamba tunapaliliwa wooote ila yatayozaa ndiyo yatakuwa Mali ya mpandaji:

+Mwisho kabisa Mungu anazokanuni zake na system zake za utendaji kazi tusimuingilie cha msingi ukimwagiliwa maji zaa)(

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
 
na wale wanaokufa kwa kuliwa na wanyama baharini wanapataje hiyo kitu au una imagine tu usemi wako mkuu???

Mwili hauna mamlaka yoyote unapokuwa umetengana na Roho
 
Mkuu hii kitu naweza iamini kiasi fulani. Huwa nikiamka toka usingizini usiku au asubuhi huwa niweza kuona au kuishi na kufikiri katika namna fulani hivi ambayo ni yatofauti. Combination ya idea na vitendo huwa vya aina yake kabisa na wakati huo akili yangu huwa inaniambia kuwa 'this is real'. Lakini dakika zikisogea kidogo narudi kwenye ubinadamu wa kawaida. Najaribu kufikiri kwa namna ile ya mwanzo, nashindwa kabisa. Najaribu kuunganisha mtiririko wa mawazo na vitendo nilivyofanya dakika chache zilizopita lakini akili yangu kwa muda huo inanambia 'hicho kitu hakiwezekani'.

Sio siri hali hii inanitesa sana kwa sababu huwa najaribu kuishi siku nzima maisha ya soon after kuamka usingizini lakini nashindwa naishia kichwa kuuma tu. Juzi usiku niliamka usingizini nikawa nasikia kama sauti fulani ikinipa sababu kitu fulani (sitaki kukitaja) ni bora kuliko kitu fulani (nacho sikitaji pia) with well organized facts na nilielewa vizuri kabisa na nikapanga kuja kuleta thread humu jf katika jukwaa hilihili. Kwa hiyo nilichokifanya nilitake note ya vitu vya msingi ili nisisahau.
Cha ajabu baada ya kuamka nikashindwa kabisa kuunganisha hoja kama nilivyokuwa nimeelekezwa. Karatasi ninalo naliangalia tu lakini siwezi kuandika chochote cha maana kuhusu jambo hilo. Nimejaribu kurudisha mawazo nyuma ili japo nikumbuke lakini wapi.

Maisha yana siri kubwa sana.
 
aise..pole sana kiongozi...usisahau kushare nasi kila linalowezekana
 
Mkuu bora ungesema hujui. Kuliko kusema kuwa swali aulizwe Yesu mwenyewe halafu mwisho wa siku umetoa hitimisho lisilo na logic. Mungu yeye ndiye muweza wa yote atashindwaje kutengeneza uzao wa mema tu? Mfano wako wa mahindi na suala la uungu ni vitu viwili tofauti. Kwavile yeye Mungu ndiye mwenye uwezo, kazi yake haipaswi kubahatisha. Kama mahindi hayakuzaa basi kapanga mwenyewe yasizae na wala sio kwamba yameshindwa kuzaa kwa bahati mbaya.
 
Haya ndio mambo mnayofikiriaga yasio na logic.
Umepewa Pumzi,akili,na macho na hata masikio hivi vyote Ni vitendea kazi vyako wewe.......umepewa mtihani ambao unapaswa kuuweza ili mwisho utunukiwe taji la ushindi unaanza kusema kwann tumepewa mtihani!?

Fanya mema taji yako iko njema.
Fanya mabaya taji yako iko mbaya.
Tena hii elim kaileta yeye mwenyew muumbaji...
.ukweli nikwamba Mungu Amepanda ngano yake Kama mkulima tena magugu na ngano yanakua pmj ila siku ya mavuno yaliyozaa ndo yatapelekwa ghalani na magugu tunachoma moto.
 
Mkuu ndio maana nimekupa swali hapo juu je lipi kati ya haya tuamini?
1)Mungu mwenyewe anaamua watu gani waende peponi na watu gani waende motoni. Kwavile yeye ndiye anayemuumba mtu na pia kabla hajamleta mtu duniani anajua mwanzo hadi mwisho wa huyo mtu utakuwaje. (Anajua alichokipanda na kitakachoota)

Au

2) Mungu hajui mwanzo(kabla ya mtu kuzaliwa)na mwisho wa mtu utakuaje hivyo jitihada au makosa yaweza kubadilisha hatima ya mtu (anajua alichokipanda ila kitachoota hajui)
 
mi mbona hajaingia mkataba wowote na mm ,inamaana hayuko fair kiasi anaingia mkataba juu ya maisha ya mwingine....
 
Huu ulionandika ndio ukweli mtupu kuhusu maisha ya rohoni. Kimsingi Death is an illusion of the mind tu, ila binadamu halisi yeye anaishi eternity and he is forever pure and forever true in spiritual realm.
Asante sana ndugu umefafanua mno hadi nimefurahishwa na kutoka mafichoni nikupe japo heko.

Nina mengi sana ya kusema juu ya hili suala nikipata muda nitaandika kidogo.

Ila kimsingi, Umenikosha sana mkuu. Heko kwako lifecoded
 
@ManchoG umenitendea haki kwa kuhoji udugu wangu na binadamu anaeishi kwenye 3D dimension akiwa in physical body ..huyu ndugu lifecoded jamaa yuko well enlightened and illuminated utadhani anatoka kwenye Illuminati family ya illuminated fellas.
 
karibu mkuu
 
Mungu wa kweli anakaa kwenye jua na hakuna kiumbe kinachohimili joto la jua , sasa mbingu iko wapi ? Binadamu utayeyuka tu kama mnyama hivyo tumia mda wako vizuri na uifaidi dunia lakini uache photocopy yako kwa ukumbusho
 
Kaka nimesoma andiko hili,nina maswali kadhaa ila na anza na haya :

1. Kaka andiko lako limegubikwa na tamko 'fulani' kwa wingi mno. Hii inaonyesha hiki unachokiongelea unakizungumza bila ya elimu. Ili ukosoe mawazo yangu haya,naomba unipe majibu ya hiyo 'fulani' kila ilipo tumika. Yaani kwanini hiyo 'fulani' unashindwa kuiweka wazi ? au kwanini huiweki wazi ?

2. Vipi wale wanaokufa wakiwa hawana utambuzi wowote ?

3. Kaka kwanini mnapenda kuzungumzia mambo msio na elimu huku mkidhani mna elimu nayo. Inakuwaje unasema kifo hakuna hali ya kuwa unakizungumzia kifo ? Je uhisi kama umeamua kuwa mpotoshaji ?

Kitendo ulicho kizungumzia roho kutengana na mwili hicho ndio KIFO chenyewe.

4. Ni yapi marejeo yako juu ya haya uliyoyaandika ?

5. Je unajua kama kifo nacho ni kiumbe ?

Ukijibu maswali yangu,ninakuja kuendelea hapa nilipo ishia.
 

Kaka mkubwa nakupa angalizo moja tu,kaka suala la kifo na mfano wako haliwezi kuelezewa ki mantiki au kifalsafa na dhana nyinginezo.

Kutokubali au kujua hili ni uchachefu wa maarifa juu ya utofautishaji wa mambo.

Mfano leo hii huwezi kupata maelezo ya utendaji kazi wa computer kwenye vitabu vya dini,bali vitabu vya dini hasa Qur'an inakupa mongozo wapi ukapate maelezo ya utendaji wa Computer. Suala hili wajiitao wana fikra,wayakinifu,wakanamungu wameghafilika nalo. Wao wanaona ya kwamba majaribio ya kisayansi na mfano wake yanaweza kukupa majibu ya kila kitu,wengine wanaona elimu ya mantiki inaweza kukupa majibu ya maswali yako ili mradi tafrani tu na upotoshaji.
 
Mkuu jinsi binadam anavoendelea kuishi ndivyo anavyozidi kujua mambo mengi yanayohusu huu ulimwengu
Hv kama wachina wangetutawala inamana tungemuabudu Mungu yupi?
Kaka naomba uniambie ni jinsi gani kila binadamu anavyo endelea kuishi anazidi kujua mambo katika ulimwengu huu ? Yaani kwa namna gani ?
 
apo umenishawishi kukuelewa, kwaio inamaana kwamba wale hambao hawakupata habari zake hawata hukumiwa??
Watahukumiwa kwa kupewa mtihani,kisha watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli watalipwa moto. Hawa wataingia katika kundi moja na wale watoto waliokufa kabla ya baleghe yaani kabla ya kalamu zao hazija anza kuandika mema na mabaya yao.

Bali watahukumiwa mpaka wanyama waliowapiga wanyama wenzao kwa dhulma. Ukisikia siku ya hukumu ujue hakita achwa chochote katika kupewa haki yake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…