Waislamu inabidi murudi katika mafundisho ya Rasulullah.
Bwana Mtume siku zote alihakikisha nafasi za uongozi zinakamatwa na watu wenye uadilifu na wenye uwezo wa kazi hizo. Wasomi aliwapa kazi na kusomesha, wenye nguvu za mwili na akili za kijeshi aliwapa nafasi za usalama na nakadhalika.
Mmoja wa wale akina dada wiwili waliosaidia na nabii Mussa (PBUH) alimwambia baba yake ampe ajira Mussa (PBUH) kwa sababu alikuwa ana qualify na alipohojiwa kwa nini aliamini ana qualify kuajiriwa kuchunga wanyama akasema ni mwaminifu na ana nguvu. Mwishowe akaja kuwa si mtu mwajiriwa wa baba yake bali akaja kuwa mke wa Mussa.
Uislamu umesisistiza sana ulazima wa kuchagua viongozi waadilifu. Leo hii munawakubali viongozi amabao uadilifu wao una mashaka halafu munalalamika!!
Haya mafundisho ya dini na hizi principles zingekuwa zinazingatiwa na wa-Tanzania wote katika kuchagua viongozi tusingekuwa tunafisadiwa na viongozi kiachi hiki.
Waislamu chagueni viongozi kama Quran inavyosema na Wakristu fuateni waraka zenu zilizoandikwa na mapadri, hapo tutakuwa tunaelekea kupata viongozi safi na ndio maendeleo na haki itakapopatikana.
Anayewaambia musichanganye dini na siasa huyo mtu ina maana dini yake haina majibu ya maswali ya kisiasa-dini yake iko limited na Mungu wake hakuona mbali kwamba binaadamu wanahitaji muongozo katika katika maswala ya siasa na utawala.[ /QUOTE]
Mkuu Mzanganyika heshima mbele,
Umezungumza maneno yenye hekma sana imefika mahali nikadhani labda si wewe kuna mtu kaiba password yako lakini hizo sehemu nilizo weka rangi nyekundu ndiyo zikanifanya niami ni wewe.
Kumbe Mzanganyika ukiamua kuandika mambo ya maana unaweza sasa kwa nini kila mara unakimbilia kuandika upupu ?.
Mheshimiwa Ngongo.
Umenichekesha sana kwa madai kwamba nikiamua kuandika mambo ya maana naweza
🙂
sasa mkuu hayo mekundu yana nini kukufanya uamini kwamba ndio mimi na sijaibiwa password?
🙂 Kwa ni wewe unainga mkono unafiki wa kutochanganya dini na siasa?
Kama dini yangu inasema Mungu hapendi ufisadi ni kosa kuamini hivyo nikiwa kazini?