Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MaxShimba, Oct 8, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Na Anneth Kagenda na Simon Mhina

  Kamati ya Maimamu ya kuokoa mali za Waislamu imetishia kusoma dua ya Ahla-badri kuwashitakia kwa Mwenyezi Mungu, watu wote waliohusika kuwadhulumu Waislam kiwanja chao kilichoko Chang'ombe, Dar es Salaam.

  Sambamba na hatua hiyo, Waislamu hao wamesema watafanya maandamano ya siku mbili yatakayohitimishwa na kongamano kubwa katika viwanja vya Jangwani, kwa lengo la kumshinikiza Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya makazi, Bw. John Magufuli ajiuzulu.

  Maandamano ya kwanza yatafanyika Septemba 7 na ya pili Septemba 17, wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  Akitangaza mkakati huo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Msikiti wa Mtoro, jijini Dar Salaam jana, Katibu wa kamati hiyo, Sheikh Khalifa Khamis, alisema wanaamini Mwenyezi Mungu atawaongoza vyema hadi kufanikisha kurejesha kiwanja chao.

  ``Tarehe 17 Septemba, wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tutaitisha mhadhara kwenye viwanja vya Jangwani na kusoma dua ya Ahla-Badri kumshitakia Mwenyezi Mungu juu ya dhuluma hii kwa Waislam na kumtaka Magufuli ajiuzulu,`` alisema.

  "Kamati inamtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, ajiuzulu kwa kuwa aliwahadaa Waislamu na kushindwa kuwarejeshea kiwanja na kufuta hati ya umiliki aliyopewa mfanyabiashara Bw. Yusufu Manji," alisema.

  Alifafanua kuwa Waziri Magufuli alimuahidi Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Simba, mbele ya Halmashauri Kuu ya BAKWATA kwamba serikali itakirejesha kiwanja hicho kwa Waislam wakati ambao Bw. Manji alikuwa ameshakabidhiwa hati ya ardhi hiyo huku akiwa hajalipa pesa.

  Akisimulia kwa ufupi kuhusu sakata hilo, Sheikh Khalifa alisema kuwa Februari 26 mwaka jana kamati yao ilikutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa kwamba kiwanja namba 311/1 kitalu `T` kilichopo Changombe jijini kimeuzwa isivyo halali na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa BAKWATA kwa mfanyabiashara Manji.

  Alisema baada ya kutolewa kwa tamko hilo, Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Simba, aliunda tume ya kudumu ya kuchunguza na kutoa ripoti kwa kipindi cha wiki tatu, namna kiwanja hicho ambacho ni wakfu, kilivyouzwa.

  Machi 29 mwaka jana Sheikh Simba alikubali mapendekezo ya tume na kuwafukuza katika uongozi wa BAKWATA maofisa saba wa ngazi za juu waliobainika kuwa walikula njama kwa kutumia hati za kughushi na kukiuza kiwanja cha wasilamu kwa Bw. Manji.

  Alisema Kamati hiyo ya Maimamu ilimwandikia barua Waziri Magufuli na kumwomba akirudishe kwa Waislamu kwa vile serikali ya awamu ya kwanza ilikitoa ili kijengwe chuo kikuu cha Waislamu.

  Aliendelea kusema kuwa Mufti aliwaongoza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA wanaowakilisha Waislamu mikoa yote Tanzania na kumwambia Bw. Magufuli kuwa msimamo wao ni kuitaka serikali ikirejeshe kiwanja hicho.

  Alisema walitoa maelezo hayo baada ya Waziri kuitaka halmashauri hiyo ya Waislam kutoa msimamo wake juu ya umiliki wa kiwanja hicho.

  Alisema baada ya kimya cha muda mrefu kamati ilipata taarifa kuwa serikali imekataa kuifuta hati aliyopewa Bw. Manji na badala yake, mfanyabiashara huyo aliweka Sh. milioni 86.7 katika akaunti ya Waisilam.

  Aidha kamati ilimpa Bw. Manji muda wa siku 20 kuamua kwa hiari kukirejesha kiwanja hicho kwa Waislamu naye akaahidi kuwa atakuwa tayari kufanya mazungumzo na kamati kwa nia ya kupata suluhisho juu ya mzozo huo.

  Kwa mara nyingine, Sheikh Khalifa alimuomba Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati sakata hilo ili kurejesha hati ya kiwanji hicho mikononi mwao na kutaka serikali kuheshimu masuala yanayohusu imani za raia.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivi Serikali inafanya juhudi gani kuona kwamba uuzwaji wa mali za jumuia unawekewa sheria ngumu ili kulinda maslahi ya wamiliki, ambayo inaweza kupotea kutokana na maazimio ya wachache bila kuangalia maslahi ya wengine, kama hiyo ya mali za waislamu, vyama vya ushirika nk nk.
   
 3. s

  shabanimzungu Senior Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa Waislamu hawana kazi..Al Badrei tu bas..what else do they know? becuase lack of education
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Maghufuli waziri wa ardhi? Au hii habari ni ya zamani? Kama sio, tutawachuwaje serious watu wanaofanya kosa kama hili?

  Hivi Manji amebatizwa kuwa mkatoliki? Mimi nilidhani mbaya wa waislamu ni mkatoliki na hawezi kuwa muislamu mwenzao! Hiyo serikali wanayoilaumu si hiyo hiyo wanayoisema kuwa inaingilia mno mambo yao? Serikali haiwezi kuzuia watu/vyama/ushirika kufanya maamuzi ya kipuuzi. Wabanane humo humo na kupelekana mahakamani kama wanaona kuna mtu amewadhulumu. Mpaka hapo watakapoweza kujikosoa wenyewe, wajanja wataendelea kuwachezea.

  Amandla.........
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hawa waandishi wawili wameshirikiana kutuonyesha kuwa hawako makini, John Magufuli waziri wa ardhi imerudiwa mara kadhaa,na mhariri akapitisha ichapwe! kazi tunayo!!
   
 6. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Mkuu, kumbe wabaya wa waislamu ni wakatoliki?
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ndivyo hawa wanaojifanya watetezi wa waislamu wanavyotaka tuamini. Haujasoma waraka wao na mabandiko ya wenzao kibao humu? Ni aibu tupu. Sitashangaa kama hawatatafuta namna ya kumbebesha lawama mkatoliki kwa vitendo vya Manji. Kuna jamaa anaitwa Dar es Salaam ni lazima atamuunganisha Nyerere na hii dhulma. Wee ngoja tuu. Iko kazi.

  Amandla........
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hati zipi za kughushi? Sasa wanangoja nini kwenda Mahakamani? Kuwashitaki hao wakorofi pamoja na Manji? Huko itatoka Court injuction mpaka hapo ukweli utakapojulikana.

  Amandla.....
   
 9. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Subiri, Manji akiwapa futari tu basi wanatulia, wakiumwa njaa wanaanza oooh, kiwanja.

  Hebu mwacheni magufuli kwani yeye ndo aliyekigawa kiwanja???

  Juhudi za Magufuli kurudisha Kiwanja ndizo zikamfanya aishie kwenye Wizara ya mifugo na samaki. Kama mna madai ya kiwanja nendeni Wizara ya Ardhi, Magufuli hakuhama na documents za kiwanja.
   
 10. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni ubababaishaji kuuza muuze nyie wenyewe na kulalamika pia au pesa mmeshamaliza?????
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hivi waislam wana beef na Wakatoliki?
   
 12. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Khali inazidi kuwa mbaya sana kwa hawa ndugu zetu, wasaidizi wa allah.
   
 13. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hawa Maimamu nishawastukizia kwa nini bado wamemshupalia Magufuli hata baada ya kuachia ngazi Wizara ya Ardhi na kuhamia Wizara ya Mifugo: Maimamu wanataka Pombe na Kitimoto..bwahahaaaa...

  Na hiyo Al Badhir si lolote wala si chochote bali ni mkwara tuu kwani ni mwaka au miaka miwili sasa tokea Manji atangaziwe Al Badhir. Jiulizeni kwa nini wasiisome muda wote huo (tena waisome kimyakimya bila kutangaza kwenye vyombo vya habari?) Obviously sababu ni kuwa 99.9% ya perceived effect ya dua hii inatokana na madhara ya kufadhaika kiakili apatayo mlengwa mwenye imani kuwa kweli anaweza kudhurika na ibada/dua hii. Wanatumia psychic terror ndiyo maana wanaishia kutangaza tangaza tu ili whoever it is gets all worked up anxiety and depression leading to overall ill health and possible death. In other words, you are relatively safe if you don't happen to buy into this nonsense.
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kumbe suluhisho la mafisadi lipo!!.........jamani nawaomba muwasomee hiyo Albadir the rest of mafisadi..........
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  we utasomewa wewe hiyo sijui alibadiri sijui kitu gani!!
   
 16. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .

  Sioni kama kuna jipya hapo. Waleta habari wenyewe wote wakatoliki kwanini wasichanganye mambo.

  Kilichobainishwa hapo ni kumshitaki Manji kwa mwenyezi Mungu kwa waislamu tunaamini kuwa yeye ndie hakimu wa kweli. hakuna kipengele kinachosema wasomee albadr.

  Labda niiulize jamii Albadr ni nini?
  Tuelewe kuwa kumshitaki kwa mwenyezi mungu ni kusoma maombi na kumwachia Mungu ahukumu.
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hakuna kitu kama hicho!Nyie katika kusoma hiyo...sijui nini...mnataka mtu aokote makopo. Usilete kiswaahili mingi hapa!Na kwanini mumshitakie Mungu, wakati yeye aliona hata kabla hilo tukio halijatokea?Mnamlazimisha Mungu wenu kufanya kazi yake kwa majazba yenu yale mliyozowea! Itawarudieni wenyewe hiyo nanihiino...haimpati mtu!Ama kweli... waacheni wafu wawazike wafu wenzao!
   
 18. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Acha uongo alhbadili uwa mnasoma kisha mashetani yanaenda kudhuru ndo maana mtamtuma mtu njiwa, chumvi gjni na vitu kibao, me nilisha jaribu hiyo kitu tena aliyenishawishi nifanye hivyo was my frend. Lakini kutokana na vitu nilivyo ambiwa ninunue nilipowaonyesha watu wakashangaa kuona mwalimu akifanya uganga huu, mm niliingia madrasa nkavua viatu mimi, jamani baada ya hapo sikununua na wala mwizi wangu hakusomewa.
  Nikaamua kumfuata Yesu.
  Acheni Yesu aitwe Yesu watu tumetoka mbali,
  Hao wanaotaka kusomea wenzao sio watu wazuri hata kidogo na kama mtu kweli unauwezo wa kufikiri uwezi fata dini ya kuangamiza watu, maana vitu vyenyewe mpaka mtu asomewe havifiki elfu 20 .
  Kama Mungu anavyo samehe maovu yetu nawaomba hao watumishi wa allah wasamehe wenzio.
   
 19. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Huna jipya, kwani kutangaza hiyo sijui albadil au albadilini wameanza leo..??? Tangu miaka kadhaa iliyopita walidhumunia kufanya hivyo, issue siyo mtoa habari, ila ni habari yenyewe. AU NDO KAMA KAWAIDA YENU KUBISHA HATA OBVIUS ISSUES....??? Sijui ingekuwaje kama hicho kiwanja angenunua mkatoliki.......... Mtapewa sana viwanja vya serikali na mtauziana sana. Mkauze na kile chuo mlichopewa kule Morogoro..... YAANI DAR MPAKA MORO............DAR MMEPEWA NA MORO MMEPEWA....... Mnakoelekea mtauziana hadi MISIKITI.
   
 20. October

  October JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na wasiishie kuwasomea na mafisadi tu, wazisomee na barabara zote zisozo na lami asubuhi tuliamka tukute zina lami, Wasomee na maji kwenye bwawa la Mtera lijae maji kusiwe na mgao wa umeme...
   
Loading...