GE2025 Mufti Abubakar Zubeir: BAKWATA si vibaraka wa serikali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,096
Reaction score
7,126
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) litaendelea kusimamia maslahi ya Taifa, huku akiwataka Watanzania kuendeleza uzalendo na kulinda amani ya nchi.

Mufti Zubeir ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe, alipokutana na baadhi ya viongozi wa dini na serikali, ambapo amesisitiza kuwa jukumu kuu la BAKWATA ni kuhimiza amani, umoja, na uzalendo miongoni mwa wananchi.

“Tunaizungumzia amani na uzalendo kwa sababu tunajua umuhimu wake katika Taifa. Wapo wanaodhani sisi ni vibaraka wa serikali, hapana — hatutumwi na serikali. Tunatambua wajibu wetu wa kuisaidia jamii kuelewa maana ya kuwa mzalendo wa kweli,” alisema Mufti Abubakar Zubeir.

Yaani Mufti mzima ameshindwa kuzungumzia haki? Hili neno HAKI inaonekana halipo kabisa katika vitabu vinavyotumiwa na BAKWATA.
 
Mufti Zubeir ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe, alipokutana na baadhi ya viongozi wa dini na serikali, ambapo amesisitiza kuwa jukumu kuu la BAKWATA ni kuhimiza amani, umoja, na uzalendo miongoni mwa wananchi.
Ukiongeza neno moja tu:"HAKI" kwenye maneno haya; nitakubaliana na maoni ya kiongozi huyu wa dini.
Lakini unapokazia "AMANI" isiyo kuwa na misingi yake kwenye haki, unaondoa maana kabisa ya hiyo AMANI.
WaTanzania hawawezi kuwa watu wa kugawiwa AMANI na yeyote; ni wao ndio walinzi wakuu wa AMANI ikiwa amani hiyo inaambatana na HAKI.

Huku kusisitiza AMANI; ambako ndiyo lugha inayotumiwa na waovu kama Samia na Genge lake; inawaweka BAKWATA kundi hilo hilo la waovu.

Hiyo AMANI inayolazimishiwa waTanzania ili kuwapa ruhusa watenda maovu kuendelea na uovu wao; hiyo siyo AMANI.
Mufti, usiwe sehemu ya kuwalaghai waTanzania.
 
Back
Top Bottom