Maigizo: Mbunge wa CCM Stellah Manyanya adondoka chini baada ya serikali kutoa Tsh bilioni 81 ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay

Jionee mwenyewe halafu Tafakari, Jambo la kusikitisha ni kwamba kwenye Maigizo hayo yumo hata Mbunge wa Jimbo letu la Kyela .

Aibu sana !

View attachment 2918431
Nyerere alipokua akipiga makofi pela UN, Muamar Ghadaf alikua anakasirika na kuumia sana moyoni 🐒

ndio hii sasa 🐒
wanafurahi wenye furaha zao wanaumia na kukasirika wenye gubu zao bure tu 🐒
 
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Eng.Stella Manyanya ameshindwa kujizuia na kujikuta akianguka chini Kwa kuzidiwa na furaha Baada ya kufahamishwa kwamba Serikali ya awamu ya 6 chini ya Dk.Samia imemwaga zaidi ya Bilioni 80 kuanza Ujenzi wa Bandari kubwa ya Mbamba Bay Ziwa Nyasa.

View: https://twitter.com/WizarayaUC/status/1762048040544743602?t=wKUTzncyvMe9g6YXj-7WrA&s=19

View: https://twitter.com/WizarayaUC/status/1762048171998351632?t=UxYZvr6wt5tdVQFCTB3kyQ&s=19

Akiwa mwenye furaha Mbunge huyo asemema hiyo ilikuwa ni ndoto yake miaka Mingi na Wananchi wa Wilaya ya Nyasa tangu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Sasa Mbunge wa Nyasa kupata Bandari ambayo itakuwa sana uchumi wao.👇👇

View: https://twitter.com/MwanaHabariNews/status/1762694264159367545?t=TAxuK4j31unE_adkxUSLlQ&s=19

My Take
Wananchi Wanafurahia Maendeleo Chadema wanaandamana kwamba Kuna mtu atawatafutia maisha 😁😁
 
KAZI KILA UPANDE, WA NCHI NI MIRADI TU YA KIMKAKATI, WALE WENZETU NI KUSWAGWA TU KILA SIKU KAMA NGOMBE, JANA WAMETOTA KWENYE MVUA WAKIDAI NI USHUJAA KULOWANA, WAMELOA WAMELOA WAMENYESHEWA MVUA......!
°kwa sera yetu ya kutembea ipo siku
IMG_20240228_085811_297.jpg
taifa litapata maendeleo makubwa sana, hapa bana namuhurumia slaa naye hakubaki nyuma,ametota lakini yumo!
 
Nimependa ujasiri wake wa namna alivyoishikilia maiki bila kuidodosha chini licha ya yeye kudondoka. Ameonyesha ukakamavu na uhodari wa hali ya juu sana kama askari aliyepo vitani au lindo ambaye silaha yake mkononi ndio ushindi wake dhidi ya adui. CCM Ni watu majasiri sana na watu wenye uhodari mkubwa sana katika mapambano ya kuwatetea Watanzania wanyonge.
 
Anajizalilisha tu , inamaana alipata taarifa za kuletwa fedha hizo hapohapo Kwenye huo mkutano?
Kama alikuwa Na taarifa hizo mapema huo ni usanii Na ulaghai wa wanasiasa uchwara wa chama cha majambazi
 
Anajizalilisha tu , inamaana alipata taarifa za kuletwa fedha hizo hapohapo Kwenye huo mkutano?
Kama alikuwa Na taarifa hizo mapema huo ni usanii Na ulaghai wa wanasiasa uchwara wa chama cha majambazi
Umeongea neno zuli......ulaghai aka utapeli......hv hao viongozi ni lini watajua kwamba wtz wana akili?
 
Back
Top Bottom