Mbunge acharuka Tsh. Bilioni. 64 kutafunwa ndani ya siku 1

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Judith Kapinga, ameliibua bungeni sakata la kutafunwa Sh. bilioni 64.3 kwenye Bandari ya Tanga baada ya kutolewa kwa zabuni iliyogubikwa na utata, akitaka hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika ili kuongeza uwajibikaji.

Judith aliibua hoja hiyo jana alipochangia taarifa ya utendaji wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyochambua ripoti ya ukaguzi wa mashirika ya umma uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake ya mwaka 2020/21 iliyowasilishwa bungeni Aprili 12 mwaka huu.

Akichangia taarifa hiyo ya PAC kwa kipindi kinachoishia Februari mwaka huu, Judith alisema ufisadi katika bandari hiyo ulitokana na mkataba wa mwaka mmoja ambao Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) iliingia na Kampuni ya China Harbour Engineering Company (CHEC) wa Sh. bilioni 172.36.

Alisema mkataba huo uliingiwa Agosti 3, 2019 na ulipaswa kuisha Agosti 2020, ambapo ulilenga kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga, kufanya tathmini ya athari za kimazingira na kununua vifaa kwa ajili ya shughuli za bandari.

Alisema kwa mujibu wa mkataba huo, gharama ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga ilikuwa ni Sh. bilioni 104.92, sawa na asilimia 60 ya mkataba wote.Judith alisema kuwa Agosti Mosi, 2019, Kampuni ya CHEC iliuza kazi hiyo kwa mkandarasi mbia, ikiwa ni siku mbili kabla ya kampuni hiyo ya China haijatia saini mkataba na TPA.

Alisema kuwa baada ya kampuni hiyo kutoa kazi siku moja kabla ya kutia saini mkataba na TPA, siku mbili baadaye, yaani Agosti 3, 2019, ilitia saini rasmi mkataba na TPA wa kufanya kazi hiyo kwa Sh. bilioni 104.92, ilhali tayari CHEC ilishatoa kazi hiyo kwa mkandarasi mbia kwa Sh. bilioni 40.

"Kampuni ya CHEC, yaani China Harbour Engineering Company ilipewa kazi hiyo kwa Sh. bilioni 104.92, haikufanya kazi hiyo ila iliigawa kwa bei rahisi kwa mkandarasi mbia, kwa mkataba wa dola za marekani milioni 18.15 sawa na Sh. bilioni 40.46 kwa kipindi cha miezi 11 bila kutoa taarifa kwa TPA."Pia mkandarasi mkuu, Kampuni ya CHEC, yaani China Harbour Engineering Company iliingia mkataba na ‘mkandarasi mbia’ hata kabla ya kutia saini mkataba wake na TPA kwa kuwa walitia saini Agosti Mosi, 2019 kabla ya Mkataba wa Mkandarasi Mkuu na TPA Agosti 3, 2019," alisema.

Mbunge huyo alisema kuingia mkataba bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari ilikuwa ni kinyume cha kifungu kidogo cha 4.4 cha masharti ya jumla ya mkataba kati ya Mamlaka ya Bandari na mkandarasi mkuu ambacho kinazuia mkandarasi mkuu kutoa sehemu ya kazi kwa mkandarasi mwingine.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, ikiwa kuna uhitaji wa kutoa kazi kwa kampuni nyingine kutekeleza kazi zilizoko kwenye mkataba, mkandarasi mkuu anapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari siku 28 kabla ya kutoa kazi hiyo.Kwa mujibu wa Judith, CAG alibaini jumla ya malipo yaliyolipwa kwa kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli yalikuwa dola za Marekeni milioni 18.22 sawa na Sh. bilioni 40.62.

Alisema kiasi hicho pia kinajumuisha malipo ya dola za Marekani 73,824 sawa na Sh. milioni 164.55 kwa huduma za wakala wa meli kwa mkandarasi mbia.Alisema ulinganifu wa kiasi kilichotozwa na mkandarasi mkuu cha Sh. bilioni 104.92 na kiasi alicholipwa na mkandarasi mbia cha Sh. bilioni 40.62 inaonyesha kiasi kilichotozwa na mkandarasi mkuu kimezidi kiasi halisi kilichotumika kufanya malipo ya kazi hiyo kwa Sh. bilioni 64.3.

Alisema kutokana na hali hiyo, mkandarasi huyo alijipatia Sh. bilioni 64 bila kufanya kazi yoyote, fedha ambazo zingetosha kujenda vyumba vya madarasa 3,200 nchini kwa gharama ya Sh. milioni 20 kwa chumba cha darasa."Inawezekanaje mkandarasi kuchota kiasi kikubwa cha fedha na kukiweka mfukoni bila kufanya kazi wakati viongozi wa serikali wapo na hawachukui hatua?" Mawaziri wapo, makatibu wakuu wa wizara wapo, viongozi wa bandari wapo, lakini wote hawa hawachukui hatua yoyote ili kuokoa fedha zetu ilhali mkandarasi anacheza na akili za Watanzania bila woga," Judith alisema.

Kuhusu sakata hilo, katika ripoti yake ya mwaka 2020/21, CAG Charles Kichere, anapendekeza TPA na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuchukua hatua dhidi ya wahusika kutokana na udanganyifu wa bei uliofanywa na mkandarasi mkuu.CAG pia anapendekeza serikali kuchukua hatua kwa maofisa waliopaswa kufanya utafiti wa gharama ili kujua makisio halisi ya bei kabla ya kuingia mkataba na mkandarasi.

NIPASHE
 
Hivi huyo samia haoni haya au hayasikii haya? Aisee
 
MTAISHIA KUPIGA KELELE,KULALAMIKA TU
HAKUNA HATUA YOYOTE IKATAYO
CHUKULIWA.....
TUNAWAAMBIENI HUKO BUNGENI TUNGENI SHERIA YA KUUA NA KUNYONGA AKIBAINIKA MTU ANA KULA,IBA FEDHA ZA UMMA/MALI
BILA HIVYO NCHI HII MTAISHIA KULIALIA TU

OVA
 
Without harsh and severe punitive measures being imposed and taken, such fraudulent and embezzlement acts won't stop.
 
Hapo mchezo umechezwa vizurI kabisa Kitanzania, huyo aliye pewa kazi ambaye hapo ameitwa kampuni mbia naye aliomba tender hiyo, na bei waliyoitaja ndiyo hiyo hiyo billion 40,hiyo kampuni ya China harbour nayo iliomba tender hiyo hiyo ila kwa utaratibu tofauti, yeye aliweka hivi-kwa kuwa kuna kampuni imeshaonyesha kuweza kukamilisha mradi kwa bilioni 40 basi nipeni mimi tender kwa gharama ya bilioni 102! Na mgawanyo unakuwa huu-kampuni ya China harbour utachukua bilioni 20,inabaki bilioni 82,kamati ya tenda itachukua bilioni 42, it abaki bilioni 40 ambayo ndiyo atapewa huyo mbia apige kazi!! Hiyo ndiyo maana halisi ya win-win.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom