Serikali mbioni kuanza ujenzi wa Reli ya Mbamba Bay-Mtwara na Matawi yake ya Liganga/Mchuchuma kwa Trilioni 14.5Tsh

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,744
Serikali ya Tanzania Kupitia Shirika la reli TRC inatafuta pesa zaidi ya Shilingi Trilioni 14 sawa na Dola 5.6 Bilioni za ujenzi wa reli Mpya Kwa viwango vya Sgr kutoka Bandari ya Mbamba Bay mwambao mwa Ziwa Nyasa Hadi Bandari ya Mtwara Kwa umbali wa km 1,000.

Reli hiyo itajengwa Kwa ushirikiano na sekta binafsi yaani PPP na itakuwa na Matawi kwenye migodi ya Madini ya Chuma,makaa ya mawe ya Liganga/Mchuchuma. Pia kutakuwa na Matawi kutoka kwenye migodi ya graphite iliyoko mpakani mwa Lindi na Mtwara.

My Take: Tanzania itaendelea ku make headlines Kwa miradi mikubwa hapa Afrika.

Serikali itafute pesa pia Kwa Ajili ya ujenzi wa reli ya Tanga-Arusha-Musoma na Mbeya -Dodoma.
 
SGR kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma inafunguliwa lini?
 
Sasa mtu anajenga nyumba hata haijaisha anaanza plan na msinginwa kujenga nyumba nyingine tatu. Sidhani kama kuna hata moja itakamilika
 
Sasa mtu anajenga nyumba hata haijaisha anaanza plan na msinginwa kujenga nyumba nyingine tatu. Sidhani kama kuna hata moja itakamilika
Serikali haiendeshi mipango yake kama mtu binafsi.Ikifanya hivyo uchumi uta collapse.

Kabla ya 2030 Sgr zote zitakuwa zimemalizika pengine section za kwenda Karema,Burundi na Rwanda ndio zitakuwa Bado ila upande wa Tzn miradi yote itakuwa imeisha saa Kwa nini wasubirie?
 
Asante kwa elimu lakini nilitegemea tuanze kwenda Moro na Dom Kwa dk 60... Na hiyo ingetumika kujifunza kuendesha network zote zitakazoanzishwa. By the way kwa nini network ya mwendokasi posta/kariakoo to kimara ilianza mapema kabla ya mbagala na pugu. Kwa nini tusingesubiria zote zikamilike ndio tuanze,
 
Pesa Inahangaika kuzitafuta wapi? si impe mjerumani ajenge kama masharti ya fidia ya ukoloni alioufanya ! kuomba radhi tu kwenye Mnara Rais wa Ujerumani na kurudisha mafuvu haitoshi huyu ndio aliidumaza kusini na Vita vya majimaji
kwa hivyo masharti yawe kujenga hiyo SGR . Serikali mbona imelala hivyo?
 
Asante kwa elimu lakini nilitegemea tuanze kwenda Moro na Dom Kwa dk 60... Na hiyo ingetumika kujifunza kuendesha network zote zitakazoanzishwa. By the way kwa nini network ya mwendokasi posta/kariakoo to kimara ilianza mapema kabla ya mbagala na pugu. Kwa nini tusingesubiria zote zikamilike ndio tuanze,
Mtaenda tuu kwani Kuna shida? Wako kwenye majaribio
 
Back
Top Bottom