Mahusiano yanataka kuniumiza akili

Kesi ya upande mmoja hii.

Kwanza kukaa na mtu miaka 9 yote basi kuna kitu wewe huwa unapata kwake mpaka we unampa doh ye anakugea iko kitu.
Kwani hiyo miaka yote mlokua pamoja hukuwahi kugundua hizo tabia zake??
Na vipi kama asingerudiana na ex wake, mngeendelea kua pamoja??

Wadau hapa naona wanasema sababu ni umarioo wa jamaa ila mi nahisi sababu ni wivu wako kwakua jamaa karudiana na ex wake!! Pole sana ila umri umeenda bibie chukua kale kamchepuko kako kafanye njia kuu maisha yasonge.
Mkuu siongei kwa ubaya. Ila huyu jamaa tumepitia mambo mengi sana kuliko hata nilivyoandika. Naona kuna mdau Watu8 ametoa mada na inamuhusu yeye.

So mimi nina mapungufu yangu ila hata ukimuuliza yeye, anajua nilivojitoa kwake. Suala la usaliti lilishajokeza hadi naona kawaida. Hata akienda kwa hao wanawake zake, hakai nao zaidi ya wiki 2. Labda awe ni mtu wa mkoani wawe wanachati ila sio kukaa karibu.

Yeye aliniacha mara kadhaa huko nyuma. Baada ya siku chache anakuja kuomba msamaha. Ila kwa sasa mimi nimeamua kufanya maisha. Nataka mtu ambaye atakua patner katika maisha yangu. Sio mtu wa kuniambia nimtumie pesa akatazame mpira.
I need someone kuniambia tufanye maisha na tupange future yetu ya kesho. Kama yeye hawezi naona ni afadhali nipambane mimi mwenyewe. Hiyo ndio sababu kubwa.

Najua kwamba naweza kurudi katika maisha yake kama mimi nitapenda. Na yeye anataka hivyo. Anapenda nimpende sana kupitiliza lakini hataki kuwa mwanaume.

Niliwahi kukuta siku moja ameomba shilingi elfu kumi toka kwa mwanamke mwingine. So he is that kind of a person.
Yeye kudate na mwanamke asiyemjua na kutumiana mapicha hovyo kwake ni kitu cha kawaida. Hichi nilichoamua ni nje ya wivu.
 
Habari humu ndani?

Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha JF

Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya wengine tutoe yanayotuumiza mioyoni mwetu.


This is what l wanted to share with you JF family.
Kabla sijasoma comment za wengine kwangu binafsi naweza kukushauri fanya haraka! sielewi siku hizi wazazi tunaleaje vijana miaka zaidi ya 35 kijana wa kiume hajatoka nyumbani? kweli ? anafurahi kuwa tegemezi! kama humu ndani bado tunalea watoto wetu kwa hali hiyo kwa tangazo hili nawaomba WATIMUENI vinginevyo mnaharibu maisha ya watoto wenu.

Nafahamu unahitaji mtu wa kuishi naye lakini sidhani kama ni mtu anayekufaa mwanaume lazima upende kuhonga huo ndo ukweli mwanamke akipendeza ni vizuri uone mchango wako sio unakubali tu kama bonga linashuka kwenye mteremko
 
Mkuu siongei kwa ubaya. Ila huyu jamaa tumepitia mambo mengi sana kuliko hata nilivyoandika. Naona kuna mdau Watu8 ametoa mada na inamuhusu yeye.
So mimi nina mapungufu yangu ila hata ukimuuliza yeye, anajua nilivojitoa kwake. Suala la usaliti lilishajokeza hadi naona kawaida. Hata akienda kwa hao
Unapokosea ni kutaka mtu ujenge nae maisha. Mkuu pole kwa maswahibu na maadam umekiri kua sio wivu unaokuendesha basi achana na hiyo ya kutaka mtu mfanye nae maisha.

Fanya kwa nafasi yako mtu atakuja tu, ila hii itakusumbua kama unaona unapoteza muda na unahitaji familia.
 
Mkuu siongei kwa ubaya. Ila huyu jamaa tumepitia mambo mengi sana kuliko hata nilivyoandika. Naona kuna mdau Watu8 ametoa mada na inamuhusu yeye.
So mimi nina mapungufu yangu ila hata ukimuuliza yeye, anajua nilivojitoa kwake. Suala la usaliti lilishajokeza hadi naona kawaida. Hata akienda kwa hao
Inshort ni kwamba your matured,ushauri wangu ni play your cards well n hit the jackpot hii mambo ya kudate 9years with no future waachie kindagarten mami
 
Umekimbia mwanaume ambaye Hana akili ya maisha lakini ana mapenzi, unakutana na mwanume mwenye akili ya maisha lakini ni hit and run, Hana muda na wanawake Wala mapenzi ......

Huwezi pata mwanaume mkamilifu hii dunia ...

Unachofanya unakimbia tatizo tu ,
Ila hafai bhana, hata kama ni anakimbia tatizo,,mimi bora niwe na huyo ambae hana mapenzi ila anajielewa,,,,hahahha i mean atatunza familia yake ,,mimi na watoto wangu,,unajua wanawake hatujazoea ile kumhudumia mwanaume,,ni kazi sana mkuu asikuambie mtu aisee
 
Kesi ya upande mmoja hii.

Kwanza kukaa na mtu miaka 9 yote basi kuna kitu wewe huwa unapata kwake mpaka we unampa doh ye anakugea iko kitu.
Kwani hiyo miaka yote mlokua pamoja hukuwahi kugundua hizo tabia zake??
Na vipi kama asingerudiana na ex wake, mngeendelea kua pamoja??

Wadau hapa naona wanasema sababu ni umarioo wa jamaa ila mi nahisi sababu ni wivu wako kwakua jamaa karudiana na ex wake!! Pole sana ila umri umeenda bibie chukua kale kamchepuko kako kafanye njia kuu maisha yasonge.
Hapo mimi nimemuelewa sana tu, yaani unamvumilia mtu na matatizo yake halafu anarudiana tena na x wake utasubiria nini sasa hapo? ni vile tu mtu kutaka kutoa la moyoni ila mimi hapo nasepa tu bila kuuliza mtu yeyote,,ni vzr kama alivyosema JF ni sehemu ya kutoa stress unapata mawazo na inapunguza stress

As for me namshauri achukue time yake tu na ajipe muda kuingia katika mahusiano mengine.

TIME heals, usiangalie umri ukupe stress.
 
Wee mwanamke ni mbinafsi tu kwa kuwa jamaa umemzidi kipato leo hii unamwona ana tabia za ajabu mbona wakati mko chuo mmepigika hukuona tabia zake za ajabu,leo umepata kazi yenye mshahara mkubwa kuliko mwenzako unajifanya eti jamaa hana future ,wanawake mkishakua na viajira vyenu na vimishahara mnataka kuvimba na kuwaona wanaume mliotoka mbali hawafai tena. Amerudi kwa Ex wake kwa kuwa ameshakuona una gubu na unataka umtawale kwa hivyo visenti vyako vya dagaa.
Hivi mkuu umewahi kukutana na mwanamke ambaye anakuthamini na ukiwa mkweli mkafanya maisha pamoja? Ni mimi. Ila mwanaume sawa anapokea kidogo basi kwa hicho kidogo chako nunua hata unga. Hakuna. Vocha ya buku nilimuomba tangu hatujakorofishana hadi sasa haijafika. Kweli hayo mahusiano upo na mwanaume?

Akipata shida ni mimi wa kwanza kunishirikisha. Akipata shida hakuna anayemsikiliza zaidi yangu. Lakini yeye anataka nimthamini mimi nikiwa na shida wala hana habari. Kuna siku nimeumwa mafua akagoma kuniletea chakula. Do you think naondoka sababu ya pesa mkuu?
 
eti tikati ya ndege izi drama izi hii chai kamba hii...
Wewe unanijuwa? Mimi mwenyewe nina uwezo wa kujilipia kwa taarifa yako.

Afu nakukumbusha usinione naandika hapa ukajuwa humu hatujuani, ninapoandika hapo najuwa kuna mtu ananifahamu anaweza soma comment hii, na kweli yupo huyu ndo ana uwezo wa kusema chochote dhidi yangu na ni mwanaume. sio wewe ambae bado unaishi kwa shemeji. Ndo uje kunambia bmambo ya drama.
 
hapo mimi nimemuelewa sana tu, yaani unamvumilia mtu na matatizo yake halafu anarudiana tena na x wake utasubiria nini sasa hapo? ni vile tu mtu kutaka kutoa la moyoni ila mimi hapo nasepa tu bila kuuliza mtu yeyote,,ni vzr kama alivyosema JF ni sehemu ya kutoa stress unapata mawazo na inapunguza stress

as for me namshauri achukue time yake tu na ajipe muda kuingia katika mahusiano mengine.

TIME heals, usiangalie umri ukupe stress.
Mkuu hilo suala la kurudiana na ex najua sababu nimepunguza mapenzi. Upendo wangu kwake umeshuka sana. Ni mtu ambaye nikijisikia kurudiana naye its just after masaa matatu naweza kudate naye. So hiko sio kitu kinachoniumiza. Najua anafanya hivyo sababu l told him tuachane. So lazima atafute mtu wa kumkeep busy. Ishu ni kwamba sioni muelekeo yeye akiwa kama kiongozi wa familia tunayotaka kuanzisha
 
Kuna jamaa ana uzi wake hapo nimeshindwa kuichukua ile link nendeni mkausome kichwa cha habari kinasema; kama mwanamke akiwa na elimu kubwa na kipato fedha nyingi kushinda mwanaume wake.. nendeni mkausome ule uzi nashindwa kuufananisha na huu au ndio huu huu umebadilishwa tu kichwa cha habari.. WANAWAKE NYIE DAAH.. mmh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom