The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 376
- Thread starter
- #41
Mkuu siongei kwa ubaya. Ila huyu jamaa tumepitia mambo mengi sana kuliko hata nilivyoandika. Naona kuna mdau Watu8 ametoa mada na inamuhusu yeye.Kesi ya upande mmoja hii.
Kwanza kukaa na mtu miaka 9 yote basi kuna kitu wewe huwa unapata kwake mpaka we unampa doh ye anakugea iko kitu.
Kwani hiyo miaka yote mlokua pamoja hukuwahi kugundua hizo tabia zake??
Na vipi kama asingerudiana na ex wake, mngeendelea kua pamoja??
Wadau hapa naona wanasema sababu ni umarioo wa jamaa ila mi nahisi sababu ni wivu wako kwakua jamaa karudiana na ex wake!! Pole sana ila umri umeenda bibie chukua kale kamchepuko kako kafanye njia kuu maisha yasonge.
So mimi nina mapungufu yangu ila hata ukimuuliza yeye, anajua nilivojitoa kwake. Suala la usaliti lilishajokeza hadi naona kawaida. Hata akienda kwa hao wanawake zake, hakai nao zaidi ya wiki 2. Labda awe ni mtu wa mkoani wawe wanachati ila sio kukaa karibu.
Yeye aliniacha mara kadhaa huko nyuma. Baada ya siku chache anakuja kuomba msamaha. Ila kwa sasa mimi nimeamua kufanya maisha. Nataka mtu ambaye atakua patner katika maisha yangu. Sio mtu wa kuniambia nimtumie pesa akatazame mpira.
I need someone kuniambia tufanye maisha na tupange future yetu ya kesho. Kama yeye hawezi naona ni afadhali nipambane mimi mwenyewe. Hiyo ndio sababu kubwa.
Najua kwamba naweza kurudi katika maisha yake kama mimi nitapenda. Na yeye anataka hivyo. Anapenda nimpende sana kupitiliza lakini hataki kuwa mwanaume.
Niliwahi kukuta siku moja ameomba shilingi elfu kumi toka kwa mwanamke mwingine. So he is that kind of a person.
Yeye kudate na mwanamke asiyemjua na kutumiana mapicha hovyo kwake ni kitu cha kawaida. Hichi nilichoamua ni nje ya wivu.