Tumeongea sana na kujadiliana hata siku ya kutambulishana rasmi.
Kila ninapomshauri juu ya kutoka kwao anasingizia hajamaliza maandalizi ya kuhamia kwake. Hii story ya maandalizi ya kuhamia inaenda mwaka sasa. Kila siku hana pesa kwamba anaandaa mazingira.
Kipato anachokipata yeye ni pombe ingawa anadai ni maandalizi ya ujenzi. Ana mtoto lakini hajishughulishi chochote na mwanae.
Mi nafikiri kuna maandalizi ambayo yaliipaswa kufanyika kabla ya kutambulishana. Kila mara ugomvi ni huo na akiitaka kuondoa ugomvi mara nyingi anatoa hizo story za kutambulishana ambazo hadi leo hazijatimia.
Ni mtu ambaye mnaweza kusema leo mtafanya hivi, akarudi jioni akasema ameghairi.
Ni mtu ambaye mnaweza kugombana ugomvi mkubwa, usiku akarudi kama vile hakuna kilichotokea.
But l need someone ambaye akiongea kitu tusimamie hapo. Mtu ambaye anaweza kusimama aseme hiki hapana kile ni sawa. Sio mtu ambaye chochpte kwake ni sawa. Mfano nikitaka kurudi kwake hapa ni kumpigia simu na kuomba msamaha mnaanza mlipoishia. But l need a person ambaye akisema tumeachana anaelewa kichwani mwake kwamba hapa sipo tena na wala sitakiwi kuwepo tena. Sijui unanielewa point yangu?