Mahojiano ya Rais Samia na BBC yataongeza maswali na sio majibu

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Ukweli natamani kuwa mshauri wa Rais.

Rais wetu ni muungwana sana. Ana mtazamo chanya kuhusu taifa. Ila kupitia mahojiano ya leo watu wanaofikiri sana atakuwa kama washauri walitakiwa wabuni maswali na majibu yote baada ya mahojiano. Kama mama anaongea kwa kumaanisha ni lazima ajue.

1. Tofauti ya chaguzi na tume zetu za uchaguzi ndio zinazopelekea minyukano ya kisiasa baada ya uchaguzi. Hatuwezi kujilinganisha na nchi za Magharibi kwani uchaguzi wetu uacha makovu makali na yasiyovumilika.

2. Hata Ulaya mabadiliko kufikia Demokrasia ya kweli yalipitia kwenye misuguano na mijadala mikali. Democrasia haikutua tu tokea mbinguni. Kuna French Revolution, Chartisim na Ludism Uingereza na zilikuwa mbaya sana. Kama wapinzani wakihisi hawatendewi haki lazma watashinikiza mabadiliko.

3. Mbowe hakukamatwa peke yake Mwanza, Je wenzake wote ni magaidi.

4. Kwanini mashtaka ya Ugaidi yatokee Mara baada ya ishu ya Katiba?

5. Pia onyo la chokochoko lilitolewa kabla na Rais na Kama alimaanisha wale wanaodai Katiba. Mbowe alipinga vikali Sana kupitia Twitter. hivyo tayari kulikuwa na mabishano juu ya suala la Katiba Kati ya Raisi na Mbowe juu ya Katiba na hili la Ugaidi likaja gafla.

6. Ulipuaji visima vya mafuta ungemsaidiaje Mbowe kisiasa?

7. Magaidi wengi huwa na uhusiano, mfano Alqaida, Alshababu, ISS na Boko Haramu na mengine karibu yote hushirikiana na kusaidia kwa namna moja. Je Mbowe Yuko na uhusiano na kundi lipi la Ugaidi?

8. Kundi la kigaidi linaloongozwa na Mbowe ni lipi? Au ndio CHADEMA.

9. Ni Silaha zipi na mafunzo yapi ya kigaidi CHADEMA humiliki?

10. Viongozi wapi Mbowe aliwalenga kuwaua na kwa namna gani na silaha zipi.

Hayo ndio majibu ambayo dunia inategemea kujua. Na ndio maana dunia inaomba ushahidi.

Nje ya misukosuko na Polisi ukweli CHADEMA kimeepuka kwa 100 asilimia kuanzisha vurugu kwa namna yoyote ile, kuvamia , kupiga watu au kumiliki silaha ata mawe tu.

Nje ya CCM CHADEMA Sasa ndio taasisi iliyojijenga zaidi kila kona Tanzania.

Tujipe nafasi ili kilakitu kikiwa wazi mahakamani Tumjue vizuri gaidi Mbowe Kama ni Osama wa Tanzania. Ila Kama itakuwa kesi ya danadana itatuchafua Sana.

Lazma Raisi afikirie Mara mbili mbili na asimame na ukweli na atafute washauri wapya. Hili swala likiwa la kufungwa litamchafua Sana.

Kuna hatua mama alipiga Sana kwenye utawala Bora. asiruhusu mawazo na Iman za kinaz zikamrudisha nyuma.
 
Bi mkubwa anaongelea MAZITO YA NCHI kwa WEPESI SANA, sijui washauri wake wanamshauri nini, anaongea maneno mengi ya uongo, UWEZO wa rais ni MDOGO kuongoza nchi, hili linaonekana wazi tuu.

Tunahitaji" KATIBA MPYA" hili kuepuka mambo kama hay
 
Inasikitisha sana kama taifa hadi karne hii hatuwezi kujisimamami wenye, hapa hadi mabeberu wapige kelele ndiyo mambo yaende vizuri.
 
Hisia, akili na uelewa wa Madam SSH unapaswa kuhusisha mahusiano ya moja kwa moja kati yake yeye binafsi akiwa ndiye Rais wa JMT sambamba na "understanding level" ya taasisi nyeti ya urais anayoiongoza.

Kukiwa na 'conflicting understanding" basi hapo patakuwa na tatizo kubwa sana. Yeye ndiye Rais wa nchi yetu, anaongoza watu waliochagua chama chake na wale wasiokichagua, wanaokubaliana na itikadi za chama chake na pia wasiokubaliana nazo, wenye mitazamo sawa na yeye na pia wenye kukinzana naye.

Anapaswa kuchuja mambo yenye kuzingatia ukweli na haki yaliyopo mbele yake. Atafute njia yoyote ile iliyo bora ili kuimarisha umoja na utengamano wa kitaifa. Azingatie haki za wananchi zilizopo kikatiba na kisheria.

Mwisho ingawaje si kwa umuhimu, atafute marafiki wapya wenye kumuunga mkono, lakini asirithi maadui wenye malengo ya kimkakati toka kwa mtangulizi wake.
 
Ukweli natamani kuwa mshauri wa Raisi. Raisi wetu NI muungwana Sana. Anamtazamo chanya kuhusu taifa. Ila kupitia mahojiano ya Leo watu wanaofikili Sana atakuwa Kama washauri walitakiwa wabuni maswali na majibu yote baada ya mahojiano...
Kama umemsikiliza akihojiwa na salim kikeke hajashindwa swali hata moja, kikete kaishia kutingisha tu kichwa cha kukubali kwa kila swali.

Hapa ni kwamba yale mafisi yatakosa pa kushikia, kama yalipanga angefeli basi imekula kwao...
 
Kujitekenya mwenyewe ili ucheke, ni tofauti na kupata mtekenyo wa mtu mwingine. Kicheko huja chenyewe na wala si kwa kulazimisha.

Kutafuta visingizio ili kukwepa uhalisia wa hoja ni tofauti sana na kukabiliana na ukweli mchungu. Wapinzani ni marafiki na wakweli kwa kuwa wanaonyesha mapungufu, zaidi ya kundi la wanafiki na wahafidhina wenye kukwepa kukabiliana na ukweli ijapokuwa ni mchungu.
 
Back
Top Bottom