kamjabari
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 1,132
- 1,640
Tayari chama tawala kinatoa taswira kwamba wizi sio dhambi so wananchi watajifunza nini??Tatizo la Tanzania vyombo vya usalama vimeingizwa sana kwenye siasa. Tatizo lingine ukisha ingiza vyombo vya usalama kwenye kazi na siasa utakuwa na matatizo makubwa sana mfano angalieni uchaguzi na wizi wa kura 2020 yaani mgombea anapata kura zero hata kwenye kituo ambacho yeye kapiga kura! Sasa kama nchi ni kwanini tulitumia mabilioni kwenye uchaguzi kama pesa zinapotezwa hivi kwa shughuli ambazo ni za kudanganya wananchi. Hatuwezi kuacha kumlaumu Hayati Magufuli kwa hili kafanya makosa makubwa sana kwa kuingiza usalama na polisi kwa kiasi hiki serikalini. Sasa wanajiona wenyewe ndiyo wanajua wafanye nini kuanzia ulinzi mpaka siasa
Serikali ya ccm ifikirie vingine mbeleni si kuzuri