Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 77,355
- 111,637
Zamani mahari ilikuwa inatolewa na mwanaume kama asante kwa wazazi kwa kumtunza na kumlinda binti mpaka kufikia wakati huo anapoolewa (ndipo kukawa na hadithi za kama binti anakutwa hana bikira basi mahali inarejeshwa)
Hapa umeeleza vyema kabisa mkuu, na mantiki ya utunzaji wa binti ni kweli ilizingatia kwanza "uanamwali" halafu pili ndio ilikuwa ni kama shukrani kwani baada ya binti kuolewa anakuwa ni sehemu ya milki ya mwanaume.
Kama nilivyoeleza hapo awali inaaminika kwamba pindi mwanamke anapoolewa moja kwa moja huwa ni sehemu ya milki ya mwanaume...kufanya hilo litimilike ndiposa unatoa mahari kama hati ya kupewa miliki.kwa mantiki hiyo basi na ulimwengu huu uliobadilika ambao tunaoa na kuolewa na watu ambao wameshakuwa na minimum ya mahusiano 10 nyuma kuna umuhimu kweli?
Kama utakuwa unafahamu vizuri nadharia za filosofia, ndani yake huwa kuna suala moja linaitwa "mabadiliko ya kitamaduni", mabadiliko haya huletwa na sisi watu kulingana na matakwa kwa wakati uliopo. Kwa mantiki hii ya mabadiliko ya kitamaduni, suala la mwanamke aliyejitunza ndiye mwenye kustahiki ndoa na mahari ni kama limezikwa.
Hivyo mzani ni kama umebadilika na upande ulioegemea ni ule unaotoa taswira kwamba mahari ni shukrani tu ya ambavyo wazazi wa kike walivyomlea binti yao katika makuzi ya kimo na maarifa. Therefore umuhimu bado upo...