Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,673
- 11,343
Watu kutumia kitu vibaya haimaanishi kuwa idea nzima ni mbaya.
Mahari yanatumiwa na wengi kuunganisha familia tu.
Kumfurahisha babu mjukuu wake kaolewa, basi anapewa shuka jipya; bibi anapata kanga mpya
Sidhani kama kuna asiyependa kupokea zawadi
Mbaya ni kwamba, wakati mwengine tunatumia mahari kama tupo kwenye biashara.
Na hii kwa mwanamme asiyetaadhima, ndipo anapoitumia kuwa kamnunua mwanamke.
Familia zinatakiwa kuwa careful hapo. Ionekane wazi kuwa hii ni a small token of appreciation na sio biashara
Maneno mazuri hayo mkuu kwa kuongezea hapa wazee wetu walikuwa na alama za kujivunia na jamii nzima ilikuwa inazikubali hivyo inapotolewa mahari mfano ya mbuzi au ng'ombe kila mmoja kwenye familia aliona amethaminiwa pamoja na kwamba hata wao hiyo mifugo wanayo. Sasa zama hizi ndio kasheshe mtu kabila lake ni kwa ajili ya kujaza kwenye document au kama kakamatwa na polisi maana ndio huwa wanauliza kabila baada ya hapo hakuna kingine anachojua kuhusu kabila lake plus uwezekano wa kumwoa mtu wa kabila lake ambao wana-share mila na desturi unakuwa mdogo kutokana na mazingira ambayo amekulia hivyo inapofika suala la kuoana ndio yanakuja haya mambo ya mahari milioni kadhaa kwa kuwa wanadhani fedha ndio dhana nzima ya kuoana kumbe mahari ni sehemu ya kuonyesha familia hii na ile imekuwa kitu kimoja, naomba kuwasilisha