john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 142
- 281
Maandiko yanasemaje kuhusu utoaji wa mahari katika ndoa
Kuna maswali kadhaa ambayo baadhi ya watu huulizana mara kwa mara.
Mifano: Je ulipwaji wa mahari ina ulazima wowote? Je ni agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo, je Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?
Mahari ni zawadi ya harusi; zawadi fulani, kama kiasi cha pesa, au mali, ambayo bwana arusi hutoa kwa baba ya bibi-arusi wake, kama ridhisho kabla ya kumpokea (Mwanzo 34:12; Kutoka 22:17; 1Samweli 18:25).
Ndoa ya kwanza duniani ilifungishwa na Mungu mwenyewe. Na hakukuhusika mahari wala viapo. Hiyo yote ni kwa sababu Hawa hakuwa na baba wala mama.
Kwa haraka, unaweza kusema kuwa Adamu hakutoa mahari. Lakini, ukitazama kwa jicho pembuzi, utagundua kuwa kwa kutoa ubavu wake (Mwanzo 2:21-23), Adamu alitoa mahari, kwa maana halisi ya mahari, na mahari iliyo kubwa zaidi, kuliko hata dhahabu na almasi zinazotolewa leo katika jamii.
Siku hizi wake zetu wanao wazazi wao. Hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa. Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao. Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.
Hivyo, siyo vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu. Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu. Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari.
Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke. Ni kumthaminisha yule binti kwamba hajaokotwa tu.
Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu, kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu, hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani. Hapo mahari isingekuwa lazima kwa sababu wametoka kwetu (kwenye miili yetu kama Adamu).
Lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine. Hivyo ni lazima mtu upitie hatua za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake, ikiwemo mahari.
Luka 2:4: “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; 5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, AMBAYE AMEMPOSA, naye ana mimba”.
Hebu tuone Kumbukumbu la Torati 22:28-29, inasemaje kuhusu posa na mahari:
28 Mtu mume akimwona kijana aliye mwanamwali ambaye hajaposwa, akamshika na kulala naye, wakaonekana; 29 yule mtu mume aliyelala naye na ampe baba yake yule kijana shekeli hamsini za fedha, kisha na awe mkewe, kwa kuwa amemtweza; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.
Hivyo, hatua hiyo ya posa ikishavukwa, kinachofuata sasa ni kwenda kanisani.
Tulipowatoa, tumewatoa katika jamii. Watu wote walikuwa wanajua binti yule hajaolewa. Hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu, kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo. Na kijana naye vivyo hivyo, anatamka na kukiri kuwa ushuhuda. Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.
Mahari, wakati mwingine huitwa gharama ya bi arusi. Ilikuwa malipo ambayo mwanamume alitoa kama zawadi kwa familia ya mwanamke ambaye alitamani awe mke wake.
Tunamuona mtumishi wa Abrahamu akichukua ngamia kumi kati ya ngamia wa Abrahamu na vitu vizuri vya kila namna alivyokuwa navyo Abrahamu na kwenda navyo Aram-Naharaimu katika mji wa Nahori, ili kwenda kumtafuta mchumba kwa ajili ya Isaka (Mwanzo 24:10-14).
Tunaona katika siku za Yakobo, kutoa mahari kwa Raheli ilikuwa jukumu iliyotarajiwa kidesturi katika utamaduni. Kupanga kulipia mahari lilikuwa jambo lililokubalika pia.
Kwa kuwa Yakobo hakuwa na chanzo kingine kikubwa cha mapato wakati huo, alijitolea kufanya kazi, ndiyo Raheli awe mke wake. Alielewa kuwa hilo ndilo pendekezo pekee angefanya na limpendeze Labani. Labani, baba wa msichana, angeona pendekezo la miaka saba ya kazi bila malipo kuwa ukarimu sana. Yakobo alitaka kutoa pendekezo lake la kuvutia ili kuhakikisha Labani “ameitikia” kumpa Raheli katika ndoa (Mwanzo 29:18-20).
Tunauona mtindo wa kutoa mahari ukidhihirika pia wakati Shekemu akitaka kumuoa Dina binti wa Yakobo, pale Shekemu aliposema “Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoileta, hata iwe kubwa kiasi gani, nami nitawalipa chochote mtakachodai. Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu" (Mwanzo 34:12).
Aidha, Daudi aliua Wafilisti 300, akapata govi 100 zilizohitajika za kumpelekea Mfalme Sauli, ili aweze kuoa binti yake. Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake (1Samweli 18:25-27).
Bado leo hii, mfumo wa mahari unatumiwa katika sehemu nyingi za ulimwengu. Mchakato unahitaji ushirika wa familia zote mbili na kujitolea kwa kina kwa mume mtarajiwa kabla ya ndoa.
Mfumo wa mahari ni utaratibu wa muda mrefu katika tamaduni mbalimbali, ambao unatumika. Faida ni pamoja na uhusiano wa karibu kati ya familia zote mbili na uhakikisho wa kujitolea kwa mwanamume katika ndoa. Changamoto inaweza kuwa ukosefu wa fedha, ambacho hutumika kama kigezo kwa uwezo wa mtu kuoa.
Kulipa mahari katika biblia pia kunaonyeshwa kusisitizwa kwa kiwango maalum katika utamaduni wa kiyahudi kama inavyotajwa shekeli hamsini za fedha katika (Kumb 22:28-29) na (Kutoka 22:16-17).
Hebu tusome Kutoka 22:16, katika sheria za kijamii na kidini kuhusu mahari:
16 Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, LAZIMA ATATOA MAHARI KWA AJILI YAKE ILI AWE MKEWE.
Wazazi wengine huwakawiza binti zao wasiolewe kwa sababu wanamngoja atakayetoa kiasi kikubwa zaidi. Hilo linaweza kusababisha matatizo mazito. Baadhi ya vijana huamua kutoroka kwa siri na wapenzi wao ili kuepuka kudaiwa mahari ya juu na wakwe wagumu.
Wazazi Wakristo waweza kuwekaje kielelezo cha kuwa wenye kiasi, wenye kukubali sababu, wanapopatana juu ya malipo au upokeaji wa mahari? Jambo hili ni zito, kwa kuwa Biblia imeamuru hivi: “Hali yenu ya kukubali sababu na ijulikane kwa watu wote" (Wafilipi 4:5, 1Kor 10:32-33). Kwa kufanya hivyo, wanaonyesha kwamba wao si “wenye kupenda pesa, au wenye pupa" (2Tim 3:2).
Kwa ujumla, hakuna sehemu katika biblia inayolaumu juu ya suala la kutokulipa mahari, na wala hakuna mahali inapohimizwa kwamba mahari ni hitaji la msingi la ndoa. Lakini ipo mifano ya watu kadhaa katika biblia ambao walitoa mahari, kwa ajili ya kuoa.
Hata hivyo, katika sheria za kijamii na kidini, MAANDIKO YANATUAMBIA KUHUSU TAKWA LA KULIPA MAHARI KWA AJILI YA MKE (Kutoka 22:16 na Kumb Torati 22:28-29).
Hivyo, ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko.
Hata Yesu Kristo aliingia gharama, ili kututoa katika ulimwengu. Ilimgharimu uhai wake, ILI TU, ATUPATE SISI BIBI-ARUSI WAKE. Wanawali kumi walienda ili kumlaki Bwana Arusi (Mathayo 25:1-13).