Mahari; Mchakato na viwango vyake

Mahari; Mchakato na viwango vyake

Mkuu ishu ya mahari ina mkanganyiko mkubwa na ndio maana nilianza kwa kujitetea kuwa namna ya utoaji hutofautiana kulingana na jamii mbalimbali za watu...
Binafsi sijawahi kuona mila ambayo binti ndiye hupewa mzigo wote wa mahari ila nimekuwa tu nikisikia...
Unajua kuwa mahari hutolewa kama ishara ya upande wa mwanaume kuwashukuru wazazi wa upande wa kike.
Katika imani ya ndoa, huwa inaaminika kuwa binti anapoolewa ni kama unamtoa kwenye familia yake na kumleta kwenye familia yako(mwanaume) hapo ndiposa mahari inapoingia.
Nimekuelewa mkuu, here comes another issue,

Zamani mahari ilikuwa inatolewa na mwanaume kama asante kwa wazazi kwa kumtunza na kumlinda binti mpaka kufikia wakati huo anapoolewa (ndipo kukawa na hadithi za kama binti anakutwa hana bikira basi mahali inarejeshwa) kwa mantiki hiyo basi na ulimwengu huu uliobadilika ambao tunaoa na kuolewa na watu ambao wameshakuwa na minimum ya mahusiano 10 nyuma kuna umuhimu kweli?
 
Kwenye makabila naweza kuelewa kwa mfano
wasukuma; wao akiwa mweupe mahari lazima iende juu maana wenzetu wale wako obsessed na rangi
Wakurya; wao kuoa ni kama kuuza na ndio maana binti akishaolewa hata akitolewa macho ni sawa tu maana anakuwa property ya mume.

Kwenye dini labda ungetusaidia Gaijin, dini inasemaje kuhusu mahari?

Inategemea na dini unayoizungumzia

Hivi sasa WaHindu wanatoza mwanamke mahari kumlipa mwanamme - nayo si yenye thamani ndogo - kutokana na sababu za kihistoria baada ya Princess wa Ureno kumpa mji mzima wa Bombay, King Charles wa pili wa Uingereza mnamo mwaka 1661

Waislam wao wana system ya mahari, lakini hayana shuruti za kiasi gani inafaa kutolewa. Ruhusa imetolewa kudai hata "twike ya ngamia" wakati huo huo imetajwa kuwa hata "pete ya chuma chakavu" inaweza kutosha kuwa mahari.

Hawa ni kwa mwanamme kwenda kwa mwanamke

Kwa hiyo unakuta utoaji wa mahari unaathiriwa zaidi na utashi binafsi wa wapangaji na kabila zaidi kwa vile dini haijaweka kiasi chochote
 
Uongo huo.
Mkuu nimewahi kuhudhuria moja ya majadiliano ya mahari kwa ndugu zangu wa huko so its true. Though kwa siku za hivi karibuni imebadilika sana hasa baada ya intermariages kuongezeka. Umewahi kujiuliza kwanini wasukuma wengi wanapenda kuoa wanawake toka Kilimanjaro na Arusha?
 
Yaani mie mbila mtu kujipinda na mahari, hanioi ng'o. Ni pride kwa msichana hasa kwa nilikotoka.
With their definition of beauty na ustaarabu? Mil 3 namkataza mzazi kuopea mahari khah!
 
Gaijin mi nimeipenda zaidi hii ya kidini, labda kwa mfano kwa waislam vitabu vinasema mahari inakuwa symbol ya nini?
 
Last edited by a moderator:

Mkubwa hilo tushalisikia sana kwa Wasukuma

Mimi nifikiria kuanza kutumia mkorogo nijiopolee mang'ombe mengi

Manake wale wazee wa Kisukuma hawawezi kutofautisha mkorogo na originale

*Salaam zimfikie Papa wa Wasukuma, Bwana Kiranga
 
Hahahahaa sa mzungu alitoa nini na wewe naye bhana!
 
Wee, kila mahari na utaratibu wake

Kuna sehemu binti ni mojawapo ya asset za familia kubwa sana
Na mabinti wengi wanaokoa familia zao, imagine ulikuwa maskini(kukosa ng'ombe ni umaskini wa hali ya juu) mara bintiyo anaolewa afu mara una zizi la ng'ombe 20? Ni pride kwa mzazi na mtoto pia

Nani hataki kuwa askari wa familia yake?

:: kitu gani hasa kinaangaliwa wakati wa kutaja mahari?

Nadhani mahari hutegemea na mtazamo wa anayepanga ambapo mara nyingi huwa ni wazazi au walezi upande wa mwanamke..

:: nini hasa maana ya mahari na nani anatakiwa kuchukua mahari?

Mahari ni aina ya malipo anayolipwa binti na mchumba wake au ni malipo yanayotolewa kwa binti na upande wa mume anayetaka kuoa. (Ingawaje kuna jamii nyingine mwanaume ndiye hutolewa mahari)
Nadhani utofauti wa mila hupelekea pia utofauti juu ya nani achukuaye mahari, kama ni binti ,mlezi au mzazi.
 
Mkuu nimewahi kuhudhuria moja ya majadiliano ya mahari kwa ndugu zangu wa huko so its true. Though kwa siku za hivi karibuni imebadilika sana hasa baada ya intermariages kuongezeka. Umewahi kujiuliza kwanini wasukuma wengi wanapenda kuoa wanawake toka Kilimanjaro na Arusha?

Bana eeh, mimi mwenyewe ni Mnantuzu 100%. Mshua hakutoa mahari kubwa kwa maza kama unavyodai wewe (na maza ni cheupe dawa)

Nina mabinamu ambao nao ni Wanantuzu 100% na wameolewa na wengine kuoa. Hata mara moja sijawahi kusikia dau la mahari likipanda au kushuka kulingana na skin tone ya muolewa.

Unachokizungumzia wewe at the most ni dhana potofu na at the least ni anecdotes tu za watu hapa na pale.

Kuhusu kuoa wanawake kutoka Kili na Arusha, hiyo haitoshi kuhitimisha kuwa Wanantuzu wanapenda zaidi wanawake walio light skinned.

Kuna Wanantuzu wengi tu ambao wameoa makabila mengine pia.
 
Hahahahaa kwahiyo Inflation ipo mpaka kwenye mahari eeh? Umenifurahisha mkuu
yaani wakati wazee wetu walivyo posa na kuoa ilikuwaje, na wakati huu tupo vipi.....
halfu Binti wa zamani alihitaji nini zaidi ya 2-3 items !! Loooh Lool binti wa leo bila kuondoka na kidedea Toyota pickup full loaded vopodozi tu mambo hayaendi !
Time will tell
 
Mkubwa hilo tushalisikia sana kwa Wasukuma

Mimi nifikiria kuanza kutumia mkorogo nijiopolee mang'ombe mengi

Manake wale wazee wa Kisukuma hawawezi kutofautisha mkorogo na originale

*Salaam zimfikie Papa wa Wasukuma, Bwana Kiranga
Hahahahaa, ngoja wakusikie wenyewe watakurukia haoo
 
Jamani, tunajua sana
Wanasubiri binti akitabasamu utasikia wazee wanasema 'wichubula' wakimaanisha amejichubua

Ni aibu kwa mzazi wa binti na hata mwoaji, unaweza kushangaa ndoa imevunjika hapo hapo.

Sifa nyinginezo ni kama kumaliza darasa la saba(imagine digrii ikihusika), meno meupe, mwanya, miguu mizito, tipwa tipwa kiasi.

Mkubwa hilo tushalisikia sana kwa Wasukuma

Mimi nifikiria kuanza kutumia mkorogo nijiopolee mang'ombe mengi

Manake wale wazee wa Kisukuma hawawezi kutofautisha mkorogo na originale

*Salaam zimfikie Papa wa Wasukuma, Bwana Kiranga
 
Bana eeh, mimi mwenyewe ni Mnantuzu 100%. Mshua hakutoa mahari kubwa kwa maza kama unavyodai wewe (na maza ni cheupe dawa)

Nina mabinamu ambao nao ni Wanantuzu 100% na wameolewa na wengine kuoa. Hata mara moja sijawahi kusikia dau la mahari likipanda au kushuka kulingana na skin tone ya muolewa.

Unachokizungumzia wewe at the most ni dhana potofu na at the least ni anecdotes tu za watu hapa na pale.

Kuhusu kuoa wanawake kutoka Kili na Arusha, hiyo haitoshi kuhitimisha kuwa Wanantuzu wanapenda zaidi wanawake walio light skinned.

Kuna Wanantuzu wengi tu ambao wameoa makabila mengine pia.
Haya yameisha mkuu
 
Mkubwa hilo tushalisikia sana kwa Wasukuma

Mimi nifikiria kuanza kutumia mkorogo nijiopolee mang'ombe mengi

Manake wale wazee wa Kisukuma hawawezi kutofautisha mkorogo na originale

*Salaam zimfikie Papa wa Wasukuma, Bwana Kiranga

Unanishusha eti Papa wa Wasukuma. Wakati nina Ikulu kutoka Mkuranga mpaka Umoja wa Mataifa.

For real, nimejaribu kuelewa the fascination on the part of ndugu zangu na wanawake weupe hata sijaielewa. Labda ni kwa sababu ni wachache pande zetu huko?

Halafu kuna hii Sukuma/Chagga alliance (ambayo zamani ilikuwa Sukuma Zaramo wasukuma walivyokuwa wanakuja pwani) inakuja kwa nguvu sana. Kila cousin anayeoa kama si anaoa Msukuma (a kind of inbreeding) basi Mchagga.

Mi nataka kuvuka bahari nitafute kitu cha marashi ya karafuu, muungano ukivunjika watoto wana dual citizenship kuchagua.
 
Jamani, tunajua sana
Wanasubiri binti akitabasamu utasikia wazee wanasema 'wichubula' wakimaanisha amejichubua

Ni aibu kwa mzazi wa binti na hata mwoaji, unaweza kushangaa ndoa imevunjika hapo hapo.

Sifa nyinginezo ni kama kumaliza darasa la saba(imagine digrii ikihusika), meno meupe, mwanya, miguu mizito, tipwa tipwa kiasi.
Kwahiyo unakubali kwamba ka rangi ni very important aspect ya kukuza mahari eeh? Hata kama sio siku hizi ila ilikuwa hivyo Ng'wanik angu"
 
Gaijin mi nimeipenda zaidi hii ya kidini, labda kwa mfano kwa waislam vitabu vinasema mahari inakuwa symbol ya nini?

Hapa sina uwalii kwenye suala tajwa, hivyo nitajibu kwa kadri ya ufahamu wangu

Mahari kimsingi ya Kiislam inaweza kutajwa kuwa ni zawadi, lakini zawadi hii ni ya lazima.

Kwa sababu hakuna ndoa bila ya (makubaliano ya malipo ya) mahari, japo kuwa unaweza kuoa kwa kukopeshwa mahari.

Lengo la mahari limetajwa kwa kutofautiana baina ya wachambuzi mbali mbali.

Wapo wanaosema ni kwa ajili ya akiba yya mke iwapo atatokea mume akafa ghafla nae mke ni mtegemezi wa moja kwa moja kwa mume wake. Wengine wanasema ni zawadi tu, kama umpavyo zawadi mpenzi wako kikawaida

Kwa vile maisha ya sasa yamebadilika, wanawake wanafanya kazi na wanapesa hata kuliko wanaume wanaotaka kuwaoa wakati mwengine, unakuta mahari yanakuwa ni symbol zaidi ya kuwa na faida kimaisha kadri siku zinavyosonga mbele
 
Leo tulikuwa na mjadala kuhusu mahali na hasa viwango vya mahali vinavyotolewa

Mtu mmoja akasema yeye aliomba Mil.3 kama mahari ya kumuoza binti yake. Ikanikumbusha mbali kidogo, nikiwa secondary school nilienda na team iliyokwenda kujadili mahali ya kaka yangu aliyetaka kumuoa binti mmoja wa kisukuma. Nakumbuka mzee mwenye binti alianza na mahari ya Mil 6 lakini ikaishia kuafikiwa laki mbili na nusu.

Sasa nimeona bora tujadili kidogo hapa kitu gani hasa kinaangaliwa wakati wa kutaja mahari, nini hasa maana ya mahari na nani anatakiwa kuchukua mahari?

Wale waliooa na kuolewa tayari, wao walitoa au kutolewa mahari kiasi gani na wale wenye mabinti, wanategemea kutaka mahari kiasi gani?

Mahari ni kitu au vitu(vya thamani)ambavyo hupewa wazazi au walenzi wa binti(anayetegemea kuolewa)katika mfumo wa zawadi.zawadi hii hutofautiana na zawadi nyingize za kawaida kwani huwa na makubaliano maalum kabla ya kutolewa.kwa kawaida lazima kuwepo kwanza na muafaka na makubaliano ya dhati kati ya muolewa na muoaji kabla ya wazazi/walezi kupanga mahari.mahari hutofautiana kulingana na makabila(mila),eneo husika na dini.
kwa kawaida huwa hakuna kusudio la moja kwa moja kuhusiana na mahari lakini tukitaka kupata umuhimu wa mahari lazima turejee kakita misingi ya dini na jamii(hasa ya kiafrika kwa upande wetu).umuhimu wa mahari huwa kama ifuatavyo:
1.tambiko la kuunganisha koo mbili.
mahari hutumika kama tambiko la kuunganisha koo mbili ambazo(kwa kawaida huwa hazina undugu,ndio maana mara nyingi wakati wa kutoa mahari lazima huwa kuna mnyama anachinjwa.sana sana,ni mbuzi,kondoo au ng;ombe.
2.zawadi kwa wazazi wa binti.
mahari hutumika kama zawadi kwa wazazi wa binti(muolewaji),mara nyingi huwa ni kutunukiwa kwa kuzaa chema.mara nyingi huwa tunasikia maneno kama mama mzaa chema tc.
3.shukrani.
mahari pia hutumika kama shukrani kwa wazazi wa binti kwa kazi kubwa walioifanya ya kumtunza binti yao hadi kufikia umri wa kuwaletea heshima kubwa katika mji wao.
4.mahari hutumika pia kama kivuko.
katika hili,mahari hutumika kama kivuko cha binti kutoka katika familia moja hadi nyingine.kwa mfano mtoto anapozaliwa na kutimiza siku arobaini huwa anafanyiwa sherehe ya kukaribishwa duniani,au mtu anapofariki huwa inafanyika sherehe ya arobaini.na pia wakati wa kuolewa kivuko cha bibi harusi ni mahari.
5.uwezo wa familia ktk matunzo.
mahari pia ni ishara kutoka katika familia ya mume kuwa inyo uwezo wa kumtunza member wao mpya katika familia yao,ambaye ni bibi harusi.
wadau naomba nikomee hapa,yapo mabo mengi sana ya kuandika kuhusu hii mada
 
Back
Top Bottom