Mahakama yatoa ONYO kali kwa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yatoa ONYO kali kwa Madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Jun 26, 2012.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kufuatia mwendelezo wa mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini, serikali imeamua kutumia mhimili wake wa Mahakama kushurutisha madaktari kusitisha mgomo na kurudi kazini.

  Wakuu naweka taarifa kama zilivyo hapa.


  Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kusitisha mgomo wa Madaktari

  Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi, Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

  Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;

  Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k

  Wajibu maombi, ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.

  Masharti hayo ni


  • Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
  • Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
  Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

  My Take:

  Serikali naweza kuwashurutisha madaktari kurejea kazini lakini je inaweza kuwalazimisha kufanya kazi??
   

  Attached Files:

 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hivi ni nani anayezisimamia hizi mahakama zetu kiutendaji au ndiyo zimeaminiwa kuwa zinauzalendo wa kutosha? Tunafahamu wote kuwa serikali inasimamiwa na bunge katika kutekeleza shughuli zake na katika muundo wa uongozi nchini kwetu tunazo Mahakama, Serikali kuu na Bunge! Sasa nauliza wanajamvi, ni nani au ni chombo gani kinachosimamia utendaji wa hizi mamlaka 2 yaani bunge ( who is the watch dog of our parliament)? na Mahamaka ni nani au ni chombo kipi kinasimamia hizi mahakama?

  Tukiacha ushabiki ya kisiasa, these organs have to be watched independently! wanapovurunda wakemewe kwa maslahi ya taifa letu. Tumezoea tu kuona serikali ikiwajibishwa na bunge, lakini bunge linafanya linavyotaka pengine kwa maslahi ya wanasiasa, hivyo hivyo na kwenye hili la mahakama tunaona jinsi wanavyojiamulia pengine wanaweza kupindisha sheria kwa ujanja ujanja wao na kuathiri mamilioni ya watu kisa wahusika wameteuliwa na wenye serikali.

  I think its time to give our opinions in the coming constitutions reforms to have independent institutions which will be responsible for watching closely the decisions/functions made by these organs.
   
 3. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ni hivi,tutapewa dawa za moyo(bp)kama dawa za kutibu malaria.
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Ni rahisi kumpeleka punda mtoni lakini ni kazi kubwa kumlazimisha kunywa maji !
   
 5. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sASA WAKITANGAZA KUWA MGOMO UMEISHA. NA WAKAWA OFISINI BILA KUTOA HUDUMU ITAWASAIDIA NINI?

  SERIKALI ITATUE TATIZO LA MSINGI.
   
 6. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  MAHAKAMA DHAIFU kwani wasipotii hiyo amri watafanywaje na hiyo mahakama?mahakama ina madaktari wakuwareplace hao wanaogoma au inadhani udaktari ni sawa na wale makarani wao au mahakimu ambao unaweza wafukuza wote kesho ukapata wengine wengi zaidi ya hao.
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  hakuna mahakama ninazozidharau kama hizi za bongo..
   
 8. k

  kitero JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi siku mahakama/wafanyakazi wa mahakama na polisi wakigoma itakuwa vipi ?maaana wengine wakigoma kudai hakizao hivi vyombo huwashughulikia siku wakigoma wao itakuwaje?
   
 9. P

  Pulpitis Senior Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waanzishe madaktari wa vodafasta basi, si wamezoea kwa walimu, walimu waligoma wakaanzisha walimu was vodasta, matokeo yake leo tunaona kiwango cha elimu jinsi kilivyo poromoka.
   
 10. Kakati

  Kakati Senior Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wabunge wanawajibishwa na wananchi moja kwa moja. Ukiweka chombo cha kuwajibisha mahakama itabidi pia uweke chombo cha kukiwajibisha na hicho chombo kinacho iwajibisha mahakama. Utaendelea mpaka wapi? Aaa, ndiyo!
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Matatizo ya madaktari wetu ni ya halali na ni ya msingi hivyo njia pekee ya kuyatafutia ufumbuzi ni kwa KUJADILIANA KAMA EQUAL PARTNERS katika masuala ya tiba nchini na wala si kurusha vitisho hewani kupitia mahakama.

  Tuwasikilize Madktari wetu tuwape hicho kidogo wanachodai kwa mujibu wa ujira wao, unyeti wa kazi zao, na jinsi gani nguvu za soko zinavyosema kwenye sekta yao hiyo kote duniani.

  Madaktari wetu wasiposikilizwa kilio chao basi tujue safari hii kuna tatizo kubwa zaidi inatusubiri.

  Hakika Madaktari wa kuazima kwa siku mbili tatu toka mataifa mengine, kama ambavyo wengine wameshaanza kuwasili nchini hadi hivi sasa tayari kwa kuagizwa 'kazi za dharura', wala si dawa hapa.

   
 12. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nadhani tunatakiwa tujifunze kutoka kwa jirani zetu hasa Wakenya na tume yao ya judges and magistrates vetting kama alivurunda katika kesi yoyote(kwa maana ya judge au hakimu) lazima uwajibishwe sio tunakuwa na chombo ambacho badala ya kutenda haki kinatumika kwa matakwa ya watu binafsi.

  Hii itasaidia kutunza "integrity" ya "judicial system" yetu ambayo iko hoi bin taaban ikilinda maslahi ya wachache wakati wanyonge wanakandamizwa katika hili la serikali kukimbilia mahakamani na zuio kutolewa mara moja ni ushahidi tosha kuwa mahakama zetu zinatumika ndivyo sivyo.
   
 13. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  bunge na mahakama vina mechanism ya kuji-regulate kupitia mahakama za rufaa na kwa bunge kamati ya kanuni na haki za bunge.
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Angekuwa Jaji Gabriel Rwakabarila ndiyo aliyetoa hiyo rulling, tungemuelewa vizuri.
   
 15. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kinachofuata hapo ni "GO SLOW"
   
 16. D

  Determine JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona hii noma
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri sasa kwa kuwa serikali haina la kufanya kuhusu mgomo wa madaktari, imeamua kuwabebesha zigo hilo katika mabega ya Mhimili wake wa Mahakama, mhimili ambao daima umekuwa unanyanyaswa na serikali, kupuuzwa, kuburuzwa na kuminywa bajet stahili ya kujiendesha.

  kama wanavyosema wahenga mzigo mzito mpe mnyamwezi! Hatua ya serikali ya CCM kupeleka suala la mgomo Mahakamani ni njia ya kujiondoa moja kwa moja katika kuwajibika katika sakata hilo la mgomo ambalo hakika limewakalia vibaya sana.

  Lengo kubwa ni serikali kujionyesha kuwa yatakoyotokea tangu sasa si yenyewe, bali ni mahakama. haieleweki Mahakama itafanya nini na mwisho wake itakuwa nini maana imekubali kujiingiza kichwa kichwa. Serikali inajua fika kwamba Mahakama ikiamuru madaktari wakamatwe kwa kugoma, basi serikali itasema 'unaona, sisyo sisi, ni mahakama hiyo!
   
 18. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 783
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Salaaleeh! kwa kweli kutapatapa kubaya!
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... and that's the naked fact that Mzee Othman has NOT foreseen coming his way in not a distant future.
   
 20. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 783
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kama madhara yake ni makubwa si wapewe wanachodai basi kuondoa mzizi wa fitini, hii mbona ni commom sense tu au ndo hawa 'viwongozi' wameshaipoteza?!!!
   
Loading...