Mahakama yamwachia huru Halima Mdee

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,152
2,000
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuacha huru mbunge Viti Maalumu (asiyekuwa na chama), Halima James
Mdee alifikishwa mahakamani hapo na Jamhuri akituhumiwa kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Jamhuri, John Magufuli. Alidaiwa kutenda kosa hilo, tarehe 3 Julai 2017, alipokuwa mbunge wa Kawe, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Alifukuzwa uanachama wa Chadema, yeye pamoja na wenzake 18, tarehe 27 Novemba mwaka jana.

Alituhumiwa kwa makosa usaliti, ikiwamo kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhujumu Chadema; kughushi nyaraka za chama hicho, kujipeleka bungeni na kujiapisha kuwa wabunge wa Viti Maalum, kinyume na maekelezo ya chama chenyewe.

Mpaka sasa, bado yuko bungeni kufuatilia, Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuendelea kung’ang’aniza kuwa bado wanachama wa chama hicho.

05b14b78-eaa0-46e4-bd57-4eb8629a8642.jpg


Halima Mdee (kushoto), akiwa na Ester Bulaya kwenye jengo la mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu

Uamuzi wa kumuachia huru Mdee, umetolewa na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba leo Alhamisi, tarehe 25 Februari 2021. Akisoma uamuzu huo, Hakimu Simba amesema, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya Mdee.

Alisema, “…baada ya kupitia ushahidi wote, nimejitosheleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake. Hivyo, mshitakiwa nimeamua kumuachia huru.”

Mdee alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, tarehe 10 Julai mwaka 2017.

Mbunge huyo viti maalumu alidaiwa kutenda kosa hilo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya Chadema, ambapo alidaiwa kusema, “Rais John Magufuli anaongea ovyo ovyo, anapaswa kufungwa breki.”

Katika utetezi wake, Mdee alidai kuwa maneno aliyodaiwa kuyasema hayaoneshi kama yalikuwa yanamlenga nani; na kudai kuwa mtu anayeongea ovyo ovyo maana yake, anaongea vitu ambavyo sio kweli na havina mantiki.

Mdee amefika mahakamani hapo akiwa na swahiba wake mkuu, Ester Bulaya.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,377
2,000
Hii iwe Precedent, yoyote kesho atakayetoa kauli kama hizi kwa Kiongozi na asifanywe kitu, na hii ndivyo inavyobidi sio kila tukisema tunayoyaona kuhusu kiongozi tunazibwa midomo kwamba ni lugha chafu kwa raisi.

Kwangu mimi hakuna lugha chafu kwa Rais, inabidi awe na ngozi ngumu kupokea yote (it comes with the territory)
 

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
5,008
2,000
Et mbunge vit maalum asiekuwa na chama

Koo na we mwandishi ni mwanasiasa sio? Mbona chama ruzuku inapokea?
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,358
2,000
Hakuna linaloshimdikana baada ya kukubaliana nao kuwabutua wenzako!!

Utaishi kama upo peponi ila roho yako (nafsi) haitakuwa na amani.

Kupanga ni kuchagua..sisi wanadamu tumepewa utashi huo na Muumba mwenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom