wa stendi
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 24,688
- 26,796
Kwani alikuwa rumande?MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuacha huru mbunge Viti Maalumu (asiyekuwa na chama), Halima James
Alifukuzwa uanachama wa Chadema, yeye pamoja na wenzake 18, tarehe 27 Novemba mwaka jana.
Alituhumiwa kwa makosa usaliti, ikiwamo kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhujumu Chadema; kughushi nyaraka za chama hicho, kujipeleka bungeni na kujiapisha kuwa wabunge wa Viti Maalum, kinyume na maekelezo ya chama chenyewe.
Mpaka sasa, bado yuko bungeni kufuatilia, Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuendelea kung’ang’aniza kuwa bado wanachama wa chama hicho.
Halima Mdee (kushoto), akiwa na Ester Bulaya kwenye jengo la mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu
Uamuzi wa kumuachia huru Mdee, umetolewa na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba leo Alhamisi, tarehe 25 Februari 2021. Akisoma uamuzu huo, Hakimu Simba amesema, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya Mdee.
Alisema, “…baada ya kupitia ushahidi wote, nimejitosheleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake. Hivyo, mshitakiwa nimeamua kumuachia huru.”
Mdee alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, tarehe 10 Julai mwaka 2017.
Mbunge huyo viti maalumu alidaiwa kutenda kosa hilo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya Chadema, ambapo alidaiwa kusema, “Rais John Magufuli anaongea ovyo ovyo, anapaswa kufungwa breki.”
Katika utetezi wake, Mdee alidai kuwa maneno aliyodaiwa kuyasema hayaoneshi kama yalikuwa yanamlenga nani; na kudai kuwa mtu anayeongea ovyo ovyo maana yake, anaongea vitu ambavyo sio kweli na havina mantiki.
Mdee amefika mahakamani hapo akiwa na swahiba wake mkuu, Ester Bulaya.
Chanzo: Mwanahalisi Online