Bosi wa JATU na wenzake waachiwa

Bosi wa JATU na wenzake waachiwa

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
221
Reaction score
487
Baada ya kukaa mahabusu kwa siku 1,324, hatimaye Mkurugenzi wa Kampuni ya Jatu Public Limited Company (PLC), Peter Gesaya, ameachiwa huru katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Gesaya na wenzake wanne, Nicholaus Fuime, Esther Kiya, Mariam Mrutu pamoja na Kampuni ya Jatu PLC wameachiwa baada ya kumalizana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa utaratibu wa kisheria wa majadiliano na kufikia makubaliano ya plea bargaining ya namna ya kumaliza kesi hiyo.

Gesaya alikaa mahabusu kuanzia Disemba 29, 2022 hadi Agosti 14, 2026, siku ya Ijumaa ambapo aliachiwa pamoja na wenzake hao.

Gesaya na wenzake hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Disemba 29, 2022 na tangu wakati huo walikuwa wakishikiliwa mahabusu hadi walipoachiwa jana.

Soma Pia: Mkurugenzi wa JATU PLC aendelea kusota Gerezani kwa zaidi ya siku 690

Wakati Gesaya na wenzake hao wakimalizana na DPP na kumaliza kesi dhidi yao kwa utaratibu huo, Washtakiwa wengine watatu, Habiba Magero, Mariam Kusaja na Lucy Izengo, wataendelea na kesi yao ambayo imepangwa kutajwa Agosti 20, 2026.
boss kuachiwa huru.png
 
View attachment 3650829
Hela za utapeli tamu sana, ila ukianza kizitapika, zinatokea kwenye kila tundu ulilonalo mwilini mwako
 
Back
Top Bottom