Mahakama yadai haijashindwa kusikiliza mashauri ya ugaidi

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mahakama imesema haijashindwa kusikiliza mashauri ya watuhumiwa wa ugaidi kwa sababu ya kukosa bajeti ya kusafirisha mashahidi na kwamba gharama hizo ziko chini ya Ofisi ya Taifa ya Mwendasha Mashtaka (DPP).

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama imetaka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji ambazo imesema hazina nia njema na Mhimili wa Mahakama.

Ikumbukwe Siku za hivi kumeibuka mjadala kuhusina na washtakiwa wa makosa ya ugaidi zaidi ya 100 kudaiwa kukaa gerezani muda mrefu (miaka sita hadi kumi) bila mashauri yao kutolewa uamuzi mahakamani.

Mahakama.jpg
 
Nilitarajia waelezee sababu za mashauri hayo kuchelewa, moja baada ya jingine, kwa yale ya mashekh wa Arusha,hasa ukizingatia mahakama in case management system, Kila ahirisho lazima litolewe sababu.
Hapa ndipo unaona waziwazi mahakama "ikijikumbatia" kwa kulazimisha yenyewe, sio kulazimishwa na DPP, mahakama imekuwa kama zezeta au limsukule.

Haya majitu SSH aangalie jinsi ya kuyashughulikia, ataunda tume mpaka atachoka.

#JumaMustgo
 
Sifahamu kuhusu mahakama, Ila kwa upande wa polisi , hakuna uchunguzi watafanya bila wewe mwananchi kutoa pesa, period
 
Awa jamaa wanafanya Mahakama kama kibanda umiza chao. Wajibu kwanini miaka kumi mashehe wamo ndani? Je watafidiwa nini wakiachiwa? Hi porojo wapeleke kwenye vijiwe vya kahawa. Mahakama inafanya kazi kwa maelekezo ya mtu sio sheria. Tunataka mahalama huru naajaji wa michongo waondolewe.
 
Nilitarajia waelezee sababu za mashauri hayo kuchelewa, moja baada ya jingine, kwa yale ya mashekh wa Arusha,hasa ukizingatia mahakama in case management system, Kila ahirisho lazima litolewe sababu.
Hapa ndipo unaona waziwazi mahakama "ikijikumbatia" kwa kulazimisha yenyewe, sio kulazimishwa na DPP, mahakama imekuwa kama zezeta au limsukule.

Haya majitu SSH aangalie jinsi ya kuyashughulikia, ataunda tume mpaka atachoka.

#JumaMustgo
Sababu washasema ,mahakama haiendeshi kesi ni dpp hivyo ,ofisi ya DPp ndio ilaumiwe sio mahakama
 
Sababu washasema ,mahakama haiendeshi kesi ni dpp hivyo ,ofisi ya DPp ndio ilaumiwe sio mahakama
Mahakama ina haki ya kufuta kesi ikiona haki ya msingi ya mtuhumiwa inaathirika. Mojawapo ni kesi kuchukua muda kupita kiasi na wakati huo huo yuko ndani. Haiwezi ikawa inamkubalia DPP maombi ya kuahirisha kesi kwa sababu zisizo za msingi ad infinitum. Mwaka mmoja tu ni too much, itakuwa miaka 10? Nakumbuka kuna Jaji aliwakaripia sana Jamhuri kwa kufanya mchezo huu huu kwenye kesi ya Lema na aliamua aachiliwe kwa dhamana.

Amandla...
 
Kwanza hizo kesi za ugaidi zote ni za kubambikiwa ndio maana unaona mchakato unaenda mwendo WA Kobe...
 
Mahakama inatakiwa itoe order ya kuwaachia watu wanaofikishwa mbele yake bila ushahidi kukumalika. Mahakama ina uwezo huo, kama haina inatakiwa iwe nao.
Sababu washasema ,mahakama haiendeshi kesi ni dpp hivyo ,ofisi ya DPp ndio ilaumiwe sio mahakama
 
Tatizo la mahakama ni kushindwa kulinda haki za watuhumiwa, DPP anapiga danadana miaka 10 na mahakama inaona ni sawa tu?

Inavyoonekana baadhi ya watuhumiwa kesi zao zinacheleweshwa kwa makusudi ikiwa ni mbinu ya kuwaweka 'kizuizini' kinyume na utaratibu.

Hakuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani, wakati huohuo serikali inahofia kuwaachia labda kwasababu ya viashiria na mienendo yao walipokuwa uraiani, japo ushahidi hautoshi.
 
Back
Top Bottom