Mahakama yaamuru nyumba ya mtoto wa Mbowe ipigwe mnada

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,820
4,572

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi imeamuru kukamatwa na kupigwa mnada nyumba ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe iliyoko Mikocheni, ili kulipa deni la Sh62.7 milioni anazodaiwa na waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo.

Sambamba na amri hiyo iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mary Mrio, pia imemteua dalali wa kutekeleza amri hiyo, Jesca Massawe kutoka kampuni ya udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo kufuatia maombi yaliyowasilishwa na waandishi hao, Maregesi Paul na wenzake tisa ili kutekeleza tuzo yao waliyopewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), katika shauri la mgogoro wa kikazi walilolifungua dhidi ya mwajiri wao huyo.

Akizungumza na Mwananchi, Paul amesema wakati amri hiyo inatolewa, Dudley ambaye ni mtoto wa Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema, hakuwepo mahakamani licha ya kwamba alikuwa ameahidi kuwa angefika na fedha za kuwalipa.
 
Mbowe hajafanya poa. Kwenye ruzuku ya 2.7b alishindwa kuchomoa 62m na kulipa waandishi? Huyu ni kiongozi mbinafsi anayejijali peke yake na familia yake. Halafu kumbe Tanzania Daima ni mali yake binafsi na sio CHADEMA? Hakika huyu ni mjasiriamali na nyumbu ni mtaji wake.
 
ugali moto
mchuzi moto
 

Akifanya hivyo mnakuja kumnanga tena anatumia ruzuku kwa manufaa yake, binadamu hamueleweki
 
Wanafanya maigizo ili kuonesha kuwa Mbowe haibi ruzuku. Mlalamikiwa hakwendà mahakamani makusudi. Hao wadai watalipwa kimyakimya.
 
Kuna sehemu imeandikwa anadaiwa Freeman Mbowe?
 
Dawa ya Deni ni kulipa tu hakuna namna nyingine.
 
Kwahiyo baba mtu amekosa hiyo mil 62 akamlipia mwanae??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…