Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Mahakama Kuu ya Tanzania, imemuamuru Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kumlipa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kiasi cha Sh.Bilioni 6 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.

Hukumu hiyo ni ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018 na imetolewa na Jaji Joacquine De Mello ambapo amesema mbali na mambo mengine Musiba amlipe Sh.Bilioni 6 Membe, pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.

Mahakama imesema Sh.Bilioni 5 ni fidia ya hasara halisi na Sh. Bilioni 1 hasara ya jumla, katika kesi hiyo Membe alimshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo aliwadai Sh. Bilioni 10 kwa kumchafua.

Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.
#MillardAyoMAHAKAMANI
Huyu anastahili kukutwa na hili... Amekashifu sana wenzie...
Mbwembwe zake zilimsababishia kufukuzwa shule pale Ifunda Tech ambako aliingia kwa jina OBEID MLAGA
 
kevins-smile.png

Yako wapi Mwanaharakati hahaa..., hili liwe ni fundisho CCM hainaga rafiki, inakutumia tu kama Condom. salamu zimfikikie huyo jaji aliambiwa amfunge Mbowe burda burda!
 
Wanamkimbia...CCM wahuni sana, wanakutumia na kukupamba, ukitokea msala wote wanakukimbia wanakuacha peke yako, wao wanaenda kuimba mapambio kwa mwenye mpini wakati huo! Tha same thing kinamtokea Sabaya, alikuwa na marafiki kila kona huko CCM, kwa sasa wote kimyaa, hakuna hata mmoja anainua mdomo kumzungumzia! Ndicho kinachomtokea/kitamtokea Bashite, kuna watu wanasema eti anasiri za viongozi wengi hagusiki, CCM dont give a shit, wakiamua kukuchinjia baharini wanakuchinja mchana kweupe hata bila ya chembe la aibu

Kuhusu BASHITE ni suala la muda tu kwani siku moja atakuja sema BEN SAANANE na wengine walipotea vipi na nani walihusika na nani walihusika kummiminia risasi Lissu!! Sio leo wala kesho lakini iko siku BASHITE atasimama mbele ya PILATO!
 
Kuhusu BASHITE ni suala la muda tu kwani siku moja atakuja sema BEN SAANANE na wengine walipotea vipi na nani walihusika na nani walihusika kummiminia risasi Lissu!!
Hivi yupo wapi yule jamaa kwa sasa?
 
Hiyo tuzo kutoka kwa MAMA MBOGA ni ya nini na lini?
 
Hayo ni maneno ya mtaani kaka!!!membe akiamua kumkomoa anamfunga jela, kama mfungwa wa madai, kwa kumgharamikia gharama zote akiwa jela.
Na yule dingi alivyo mjeuri atafanya hivyo, kwa back up ya Msoga, Kinana, Mzee Makamba na wote walioumizwa na lile tahira
 
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Nimeipenda HIPC
 
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Natumai sasa tutaanza kutoa cheti cha Highly Indebted Poor Person (HIPC)
 
Back
Top Bottom