Mahakama ya Rufani yabariki mtu binafsi kufungua mashitaka yanayohusu "Haki za Msingi na Majukumu" ( Basic Rights and Duties Enforcement )

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,136
Reaction score
96,161
Sijui kama tafsiri yangu ni sahihi lakini the take home message ni hii kama nilivyoinakiri kutoka Tweeter kutoka kwa Olengurumwa

Asante timu y’a mawakili na jomo la Majaji

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania leo imetoa uamuzi katika kesi ya kikatiba ya Rufaa Na. 134 ya Mwaka 2022, iliyofunguliwa na mtetezi wa haki za binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rufaa hiyo ilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa: Jaji Rehema Levira, Jaji Wilfred Rumanyika na Jaji Gerald Ngwembe. Wakili Olengurumwa aliwakilishwa na jopo la mawakili maarufu likiongozwa na Prof. Issa Shivji pamoja na Dkt. Rugemeleza Nshala, Mpale Mpoki na Wakili John Seka.

Kesi hiyo ilihusu kupinga vifungu vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, vilivyobadili Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Sura ya 3) kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5). Vifungu hivyo vilionekana kuweka vikwazo katika mashauri ya kikatiba yenye maslahi kwa umma, maarufu kama Public Interest Litigation.

Maelezo ya Vifungu Vilivyolalamikiwa:

Kifungu cha 4(2): Kilihitaji mtu anayetaka kufungua kesi ya kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza namna alivyoathirika binafsi na ukiukwaji huo.

Kifungu cha 4(3): Kiliongeza kizuizi kwa mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji aonyeshe maslahi binafsi sawa na Ibara ya 30(3) ya Katiba.

Kifungu cha 4(4): Kiliweka sharti kuwa kesi dhidi ya viongozi waandamizi serikalini – Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Jaji Mkuu – zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya wahusika hao moja kwa moja.

Kifungu cha 4(5): Kilimtaka mtu anayepanga kufungua kesi kutafuta kwanza nafuu kupitia sheria nyingine zilizopo kabla ya kufungua kesi chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi.

Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania iliitupilia mbali kesi hiyo mnamo Februari 15, 2022, kwa maelezo kuwa vifungu hivyo havivunji Katiba wala mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa vifungu hivyo vinakamilisha Ibara ya 26(2) na 30(3) ya Katiba, na vinaakisi misingi ya utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka, na mfumo wa kimataifa wa haki.

Hata hivyo, Wakili Olengurumwa hakuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka huo huo wa 2022.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa

Leo Juni 13, 2025, Mahakama ya Rufaa kupitia kwa Naibu Msajili Mhe. Joseph Fovo, imesoma uamuzi huo kwa njia ya mtandao na kubatilisha vifungu vyote vinne vilivyolalamikiwa.

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa:

Kifungu cha 4(2) kinavunja dhana ya mashauri ya maslahi kwa umma kwa kuhitaji waathirika binafsi pekee, hali inayokinzana na Ibara ya 26(2) ya Katiba.

Kifungu cha 4(3) ni batili kwa kuwa kinachanganya masharti ya Ibara ya 30(3) (maslahi binafsi) na haki za maslahi kwa umma zinazolindwa chini ya Ibara ya 26(2).

Kifungu cha 4(4) ni batili kwa kuwa Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kikatiba kuwakilisha mihimili mingine, hasa Mahakama au viongozi wa kisiasa walio huru kikatiba kama Jaji Mkuu.

Kifungu cha 4(5) pia ni batili kwa kuwa hakuna sheria nyingine zinazotoa nafuu ya moja kwa moja kwa mashauri ya maslahi ya umma.

Agizo kwa Bunge

Mahakama ya Rufaa imeagiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta vifungu hivyo vinne ndani ya kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe ya hukumu. Uamuzi huu umetajwa kuwa ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi wanaotetea masuala ya kijamii kupitia Mahakama
 
Attachments

Hapo mahakama ipo huru ee?
Lakini ikitoa hukumu tofauti na matarajio au mkiangukia pua, inakuwa mhimili wa mahakama unaingiliwa!
 
Retired Asante kwa ku-share pdf ya hukumu... nimeisoma na hapa chini naweka analysis kuongezea bandiuko lako.

TAHMINI YA KIUNDANI YA UAMUZI WA SHAURI LA ONESMO OLENGURUMWA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, NA ATHARI ZA KATIBA YA TANZANIA KWA MUSTAKABALI WA NCHI

I. UTANGULIZI

Shauri hili lilihusu rufaa ya Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General), kupinga marekebisho ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi (BRADEA) kupitia Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Act, 2020. Marekebisho haya yaliongeza masharti mapya kwenye kifungu cha 4 cha BRADEA yanayolazimisha:
  1. Mleta maombi aonyeshe jinsi alivyoathirika binafsi.
  2. Kutumia masharti ya Kifungu cha 30(3) cha Katiba hata kwenye mashauri ya maslahi ya umma.
  3. Kupeleka mashauri dhidi ya viongozi wa juu serikalini kupitia Mwanasheria Mkuu pekee.
  4. Kuhitajika kuonyesha kuwa njia mbadala za kisheria zimetumika kabla ya kufungua kesi.
II. UCHAMBUZI WA KIKATIBA
1. Kifungu cha 26(2) cha Katiba: Ulinzi wa Katiba kwa Raia

“Kila mtu ana haki ya kuchukua hatua za kisheria kulinda Katiba na sheria za nchi.”

Haki hii ni ya mtu yeyote – si lazima awe ameathirika binafsi. Ni msingi wa mashauri ya maslahi ya umma (public interest litigation). Mahakama ya Rufaa ilisisitiza kuwa kifungu hiki kinatoa haki ya mtu yeyote kulinda Katiba, hata bila kuathirika binafsi.

Marekebisho yaliyotaka waombaji waonyeshe maslahi binafsi yalikinzana moja kwa moja na Kifungu hiki, hivyo ni kinyume na Katiba.

2. Kifungu cha 13(1), (4), (6)(a): Usawa mbele ya Sheria na Haki ya Kusikilizwa

Mahakama iligundua kuwa marekebisho haya:
  • Yanawanyima watu haki ya kuwasilisha mashauri kwa misingi ya umma.
  • Yanapendelea watu fulani kwa kuwanyima wengine haki ya kufungua kesi moja kwa moja.
  • Yanaathiri usawa mbele ya sheria kwa kuwalinda viongozi fulani kwa kutumia Mwanasheria Mkuu kama kizuizi.
Hii ni kuvunjwa kwa usawa wa kikatiba.
3. Kifungu cha 30(3) cha Katiba: Maslahi Binafsi
Haki hii ni kwa mtu aliyeathirika binafsi na ukiukwaji wa haki zake. Mahakama ilisema kuwa kifungu hiki hakiwezi kuchanganywa na Kifungu cha 26(2). Kuvifanya vifanye kazi pamoja ni sawa na “kufuta Katiba kupitia mlango wa nyuma” – jambo lisilokubalika.

4. Kifungu cha 107A cha Katiba: Uhuru wa Mahakama
Mahakama ilikemea kuwa sheria ya BRADEA inavyoelekeza mashauri dhidi ya viongozi waandamizi waendeshwe kupitia Mwanasheria Mkuu tu, ni kuingilia uhuru wa mahakama na kuzuia utekelezaji wa haki kikamilifu. Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kutekeleza maagizo ya mahakama kwa niaba ya viongozi hao.

Huu ni uvunjaji wa msingi wa utawala wa sheria na uwajibikaji.

III. UAMUZI WA MAHAKAMA YA RUFAA

Mahakama ya Rufaa imeamua yafuatayo:
  • Kifungu cha 4(2), (3), (4) na (5) cha BRADEA ni kinyume na Katiba.
  • Viongozi waandamizi kama Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, nk wanaweza kushtakiwa moja kwa moja, na si kwa kupitia Mwanasheria Mkuu tu.
  • Haki ya mtu binafsi au kikundi kufungua shauri la kulinda Katiba isihitaji uonesho wa madhara binafsi.
  • Filtration doctrine (mfumo wa kuchuja mashauri) uliowekwa na marekebisho hayo haukubaliki kikatiba.
  • Kiwango cha uthibitisho katika mashauri ya kikatiba ni balance of probabilities, siyo “beyond reasonable doubt”.
IV. ATHARI KWA MUSTAKABALI WA TANZANIA ( Maoni yangu)

A. Uimarishaji wa Mashauri ya Maslahi ya Umma

Uamuzi huu umefungua milango kwa raia, mashirika ya kiraia, na wanaharakati kufungua mashauri ya kupinga ukiukwaji wa Katiba bila kuhitaji kuonyesha madhara binafsi.

B. Kuzuia Ujanja wa Bunge au Serikali “Kupunguza nguvu za katiba yetu” kupitia Sheria za Kawaida

Uamuzi huu ni kengele kwa Bunge na Serikali kuwa Katiba haiwezi kubadilishwa kwa njia za mkato. Ni lazima kufuata taratibu za Kifungu cha 98 cha Katiba kinachoelekeza jinsi ya kubadilisha Katiba.

C. Utawala wa Sheria na Uwajibikaji

Uamuzi huu umeondoa kinga isiyoeleweka kwa viongozi wa juu na kuweka msingi wa kuwa kila mmoja yuko sawa mbele ya sheria, na anapaswa kuwajibika kwa matendo yake.

D. Uhuru wa Mahakama Umeimarishwa
Mahakama imethibitisha kuwa ni msimamizi mkuu wa Katiba, na haiwezi kufungwa mikono na masharti ya kiutawala au kisiasa yanayozuia upatikanaji wa haki.

V. Mwisho
Uamuzi wa kesi ya Onesmo Olengurumwa ni ushindi mkubwa wa Katiba, demokrasia, utawala wa sheria, na haki za binadamu nchini Tanzania. Mahakama imetumia mamlaka yake kulinda misingi ya Katiba dhidi ya sheria za kawaida zinazokiuka haki za raia.

Hili ni fundisho muhimu kuwa Katiba ni chombo cha wananchi, na kila raia ana wajibu wa kuitetea, bila woga wala masharti.

Bunge sasa fanyeni kazi bila kupunguza kitu kwenye hukumu hiyo.
 
Mahakama kwa sehemu kubwa imeshakuwa compromised na dola chafu ya CCM. Na hapo ndo wananchi tunapiga kelele.

Ila still kuna majaji wachache wanaojitambua. Jaji Rumanyika na Ngwembe wanafahamika kuwa sehemu ya majaji wachache sana wanaojitambua.
 
Sijui kama tafsiri yangu ni sahihi lakini the take home message ni hii kama nilivyoinakiri kutoka Tweeter kutoka kwa Olengurumwa

Asante timu y’a mawakili na jomo la Majaji

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania leo imetoa uamuzi katika kesi ya kikatiba ya Rufaa Na. 134 ya Mwaka 2022, iliyofunguliwa na mtetezi wa haki za binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rufaa hiyo ilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa: Jaji Rehema Levira, Jaji Wilfred Rumanyika na Jaji Gerald Ngwembe. Wakili Olengurumwa aliwakilishwa na jopo la mawakili maarufu likiongozwa na Prof. Issa Shivji pamoja na Dkt. Rugemeleza Nshala, Mpale Mpoki na Wakili John Seka.

Kesi hiyo ilihusu kupinga vifungu vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, vilivyobadili Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Sura ya 3) kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5). Vifungu hivyo vilionekana kuweka vikwazo katika mashauri ya kikatiba yenye maslahi kwa umma, maarufu kama Public Interest Litigation.

Maelezo ya Vifungu Vilivyolalamikiwa:

Kifungu cha 4(2): Kilihitaji mtu anayetaka kufungua kesi ya kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza namna alivyoathirika binafsi na ukiukwaji huo.

Kifungu cha 4(3): Kiliongeza kizuizi kwa mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji aonyeshe maslahi binafsi sawa na Ibara ya 30(3) ya Katiba.

Kifungu cha 4(4): Kiliweka sharti kuwa kesi dhidi ya viongozi waandamizi serikalini – Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Jaji Mkuu – zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya wahusika hao moja kwa moja.

Kifungu cha 4(5): Kilimtaka mtu anayepanga kufungua kesi kutafuta kwanza nafuu kupitia sheria nyingine zilizopo kabla ya kufungua kesi chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi.

Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania iliitupilia mbali kesi hiyo mnamo Februari 15, 2022, kwa maelezo kuwa vifungu hivyo havivunji Katiba wala mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa vifungu hivyo vinakamilisha Ibara ya 26(2) na 30(3) ya Katiba, na vinaakisi misingi ya utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka, na mfumo wa kimataifa wa haki.

Hata hivyo, Wakili Olengurumwa hakuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka huo huo wa 2022.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa

Leo Juni 13, 2025, Mahakama ya Rufaa kupitia kwa Naibu Msajili Mhe. Joseph Fovo, imesoma uamuzi huo kwa njia ya mtandao na kubatilisha vifungu vyote vinne vilivyolalamikiwa.

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa:

Kifungu cha 4(2) kinavunja dhana ya mashauri ya maslahi kwa umma kwa kuhitaji waathirika binafsi pekee, hali inayokinzana na Ibara ya 26(2) ya Katiba.

Kifungu cha 4(3) ni batili kwa kuwa kinachanganya masharti ya Ibara ya 30(3) (maslahi binafsi) na haki za maslahi kwa umma zinazolindwa chini ya Ibara ya 26(2).

Kifungu cha 4(4) ni batili kwa kuwa Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kikatiba kuwakilisha mihimili mingine, hasa Mahakama au viongozi wa kisiasa walio huru kikatiba kama Jaji Mkuu.

Kifungu cha 4(5) pia ni batili kwa kuwa hakuna sheria nyingine zinazotoa nafuu ya moja kwa moja kwa mashauri ya maslahi ya umma.

Agizo kwa Bunge

Mahakama ya Rufaa imeagiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta vifungu hivyo vinne ndani ya kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe ya hukumu. Uamuzi huu umetajwa kuwa ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi wanaotetea masuala ya kijamii kupitia Mahakama
Umechelewa sana, mpaka mtoto kazaliwa,kaota meno!Haki haipaswi kuchelewa,iwe nzuri iwe mbaya!
 
Hapo kwenye agizo kwa bunge ivifute vifungu husika ndani ya miezi 12 naona muda mrefu, walau ndani ya miezi sita ni fair.
 
Kumbe bado kuna majaji wanasimamia misingi ya taaluma zao!
Maamuzi mazuri na muhimu sana! Wasiwasi wangu ni kwenye utekelezaji wa hilo agizo upande wa bunge la Serikali ya ccm.
 
Retired Asante kwa ku-share pdf ya hukumu... nimeisoma na hapa chini naweka analysis kuongezea bandiuko lako.

TAHMINI YA KIUNDANI YA UAMUZI WA SHAURI LA ONESMO OLENGURUMWA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, NA ATHARI ZA KATIBA YA TANZANIA KWA MUSTAKABALI WA NCHI

I. UTANGULIZI

Shauri hili lilihusu rufaa ya Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General), kupinga marekebisho ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi (BRADEA) kupitia Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Act, 2020. Marekebisho haya yaliongeza masharti mapya kwenye kifungu cha 4 cha BRADEA yanayolazimisha:
  1. Mleta maombi aonyeshe jinsi alivyoathirika binafsi.
  2. Kutumia masharti ya Kifungu cha 30(3) cha Katiba hata kwenye mashauri ya maslahi ya umma.
  3. Kupeleka mashauri dhidi ya viongozi wa juu serikalini kupitia Mwanasheria Mkuu pekee.
  4. Kuhitajika kuonyesha kuwa njia mbadala za kisheria zimetumika kabla ya kufungua kesi.
II. UCHAMBUZI WA KIKATIBA
1. Kifungu cha 26(2) cha Katiba: Ulinzi wa Katiba kwa Raia

“Kila mtu ana haki ya kuchukua hatua za kisheria kulinda Katiba na sheria za nchi.”

Haki hii ni ya mtu yeyote – si lazima awe ameathirika binafsi. Ni msingi wa mashauri ya maslahi ya umma (public interest litigation). Mahakama ya Rufaa ilisisitiza kuwa kifungu hiki kinatoa haki ya mtu yeyote kulinda Katiba, hata bila kuathirika binafsi.

Marekebisho yaliyotaka waombaji waonyeshe maslahi binafsi yalikinzana moja kwa moja na Kifungu hiki, hivyo ni kinyume na Katiba.

2. Kifungu cha 13(1), (4), (6)(a): Usawa mbele ya Sheria na Haki ya Kusikilizwa

Mahakama iligundua kuwa marekebisho haya:
  • Yanawanyima watu haki ya kuwasilisha mashauri kwa misingi ya umma.
  • Yanapendelea watu fulani kwa kuwanyima wengine haki ya kufungua kesi moja kwa moja.
  • Yanaathiri usawa mbele ya sheria kwa kuwalinda viongozi fulani kwa kutumia Mwanasheria Mkuu kama kizuizi.
Hii ni kuvunjwa kwa usawa wa kikatiba.
3. Kifungu cha 30(3) cha Katiba: Maslahi Binafsi
Haki hii ni kwa mtu aliyeathirika binafsi na ukiukwaji wa haki zake. Mahakama ilisema kuwa kifungu hiki hakiwezi kuchanganywa na Kifungu cha 26(2). Kuvifanya vifanye kazi pamoja ni sawa na “kufuta Katiba kupitia mlango wa nyuma” – jambo lisilokubalika.

4. Kifungu cha 107A cha Katiba: Uhuru wa Mahakama
Mahakama ilikemea kuwa sheria ya BRADEA inavyoelekeza mashauri dhidi ya viongozi waandamizi waendeshwe kupitia Mwanasheria Mkuu tu, ni kuingilia uhuru wa mahakama na kuzuia utekelezaji wa haki kikamilifu. Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kutekeleza maagizo ya mahakama kwa niaba ya viongozi hao.

Huu ni uvunjaji wa msingi wa utawala wa sheria na uwajibikaji.

III. UAMUZI WA MAHAKAMA YA RUFAA

Mahakama ya Rufaa imeamua yafuatayo:
  • Kifungu cha 4(2), (3), (4) na (5) cha BRADEA ni kinyume na Katiba.
  • Viongozi waandamizi kama Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, nk wanaweza kushtakiwa moja kwa moja, na si kwa kupitia Mwanasheria Mkuu tu.
  • Haki ya mtu binafsi au kikundi kufungua shauri la kulinda Katiba isihitaji uonesho wa madhara binafsi.
  • Filtration doctrine (mfumo wa kuchuja mashauri) uliowekwa na marekebisho hayo haukubaliki kikatiba.
  • Kiwango cha uthibitisho katika mashauri ya kikatiba ni balance of probabilities, siyo “beyond reasonable doubt”.
IV. ATHARI KWA MUSTAKABALI WA TANZANIA ( Maoni yangu)

A. Uimarishaji wa Mashauri ya Maslahi ya Umma

Uamuzi huu umefungua milango kwa raia, mashirika ya kiraia, na wanaharakati kufungua mashauri ya kupinga ukiukwaji wa Katiba bila kuhitaji kuonyesha madhara binafsi.

B. Kuzuia Ujanja wa Bunge au Serikali “Kupunguza nguvu za katiba yetu” kupitia Sheria za Kawaida

Uamuzi huu ni kengele kwa Bunge na Serikali kuwa Katiba haiwezi kubadilishwa kwa njia za mkato. Ni lazima kufuata taratibu za Kifungu cha 98 cha Katiba kinachoelekeza jinsi ya kubadilisha Katiba.

C. Utawala wa Sheria na Uwajibikaji

Uamuzi huu umeondoa kinga isiyoeleweka kwa viongozi wa juu na kuweka msingi wa kuwa kila mmoja yuko sawa mbele ya sheria, na anapaswa kuwajibika kwa matendo yake.

D. Uhuru wa Mahakama Umeimarishwa
Mahakama imethibitisha kuwa ni msimamizi mkuu wa Katiba, na haiwezi kufungwa mikono na masharti ya kiutawala au kisiasa yanayozuia upatikanaji wa haki.

V. Mwisho
Uamuzi wa kesi ya Onesmo Olengurumwa ni ushindi mkubwa wa Katiba, demokrasia, utawala wa sheria, na haki za binadamu nchini Tanzania. Mahakama imetumia mamlaka yake kulinda misingi ya Katiba dhidi ya sheria za kawaida zinazokiuka haki za raia.

Hili ni fundisho muhimu kuwa Katiba ni chombo cha wananchi, na kila raia ana wajibu wa kuitetea, bila woga wala masharti.

Bunge sasa fanyeni kazi bila kupunguza kitu kwenye hukumu hiyo.
UBARIKIWE SANA TENA SANA. MAKES A LOT OF SENSE.
 
Back
Top Bottom