Je, bunge litatii amri hii ya mahakama ya rufani?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,120
Reaction score
871,374
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania leo imetoa uamuzi katika kesi ya kikatiba ya Rufaa Na. 134 ya Mwaka 2022, iliyofunguliwa na mtetezi wa haki za binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rufaa hiyo ilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa: Jaji Rehema Levira, Jaji Wilfred Rumanyika na Jaji Gerald Ngwembe. Wakili Olengurumwa aliwakilishwa na jopo la mawakili maarufu likiongozwa na Prof. Issa Shivji pamoja na Dkt. Rugemeleza Nshala, Mpale Mpoki na Wakili John Seka.

Kesi hiyo ilihusu kupinga vifungu vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, vilivyobadili Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Sura ya 3) kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5). Vifungu hivyo vilionekana kuweka vikwazo katika mashauri ya kikatiba yenye maslahi kwa umma, maarufu kama Public Interest Litigation.

Maelezo ya Vifungu Vilivyolalamikiwa:
Kifungu cha 4(2): Kilihitaji mtu anayetaka kufungua kesi ya kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza namna alivyoathirika binafsi na ukiukwaji huo.

Kifungu cha 4(3): Kiliongeza kizuizi kwa mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji aonyeshe maslahi binafsi sawa na Ibara ya 30(3) ya Katiba.

Kifungu cha 4(4): Kiliweka sharti kuwa kesi dhidi ya viongozi waandamizi serikalini – Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Jaji Mkuu – zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya wahusika hao moja kwa moja.

Kifungu cha 4(5): Kilimtaka mtu anayepanga kufungua kesi kutafuta kwanza nafuu kupitia sheria nyingine zilizopo kabla ya kufungua kesi chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi.

Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania iliitupilia mbali kesi hiyo mnamo Februari 15, 2022, kwa maelezo kuwa vifungu hivyo havivunji Katiba wala mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa vifungu hivyo vinakamilisha Ibara ya 26(2) na 30(3) ya Katiba, na vinaakisi misingi ya utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka, na mfumo wa kimataifa wa haki.

Hata hivyo, Wakili Olengurumwa hakuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka huo huo wa 2022.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa

Leo Juni 13, 2025, Mahakama ya Rufaa kupitia kwa Naibu Msajili Mhe. Joseph Fovo, imesoma uamuzi huo kwa njia ya mtandao na kubatilisha vifungu vyote vinne vilivyolalamikiwa.

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa:

Kifungu cha 4(2) kinavunja dhana ya mashauri ya maslahi kwa umma kwa kuhitaji waathirika binafsi pekee, hali inayokinzana na Ibara ya 26(2) ya Katiba.

Kifungu cha 4(3) ni batili kwa kuwa kinachanganya masharti ya Ibara ya 30(3) (maslahi binafsi) na haki za maslahi kwa umma zinazolindwa chini ya Ibara ya 26(2).

Kifungu cha 4(4) ni batili kwa kuwa Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kikatiba kuwakilisha mihimili mingine, hasa Mahakama au viongozi wa kisiasa walio huru kikatiba kama Jaji Mkuu.

Kifungu cha 4(5) pia ni batili kwa kuwa hakuna sheria nyingine zinazotoa nafuu ya moja kwa moja kwa mashauri ya maslahi ya umma.

Agizo kwa Bunge

Mahakama ya Rufaa imeagiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta vifungu hivyo vinne ndani ya kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe ya hukumu. Uamuzi huu umetajwa kuwa ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi wanaotetea masuala ya kijamii kupitia Mahakama.

Taarifa hii imetolewa na mtetezi wa haki za binadamu ambaye pia ndiye aliyekuwa mrufani katika kesi hii, Onesmo Kasale Olengurumwa! Je, Bunge litatii amri ya Mahamaka ya Rufani?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 14 Juni 2025; Saa 2:15 asubuhi
 
baada ya kupitia kwa kina maoni ya walitoa hukumu, wajibu wa bunge ni kushauriana na hatimae kuboresha mahali penye kasoro na kuimarisha sheria ili ziwe nzuri zaidi kwa maslahi mapana ya umma.

Jambo hilo tutashughulika nalo bunge lijalo baada ya uchaguzi mkuu kipindi cha miswada ya sheria.

Tunafuhi kwa maoni ya jopo la majaji 🐒
 
Kwani bado mna matumaini na kufanya uchafuzi kwa gharama kubwa?
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Kwani bado mna matumaini na kufanya uchafuzi kwa gharama kubwa?
Gentleman,
ni vizuri kuelewa kwamba bunge huru tukufu la Tanzania haliwajibiki kwa muhimili wowote wa dola ya Tanzania, ispokua kwa wananchi wa Tanazania.

There is no way vijana vitatu tu vikae mahali eti halafu vije viwakoromee wawakilishi wa wananchi zaidi ya milioni 64. That one will never happen on earth gentleman.

By the way,
Tanazania itafanya uchaguzi mkuu huru, wa haki na wazi mapema October mwaka huu 2025, kwa gharama zake za ndani. Haihitaji kufadhili wa nje.
Mkumbushe na mwenzako 🐒
 
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania leo imetoa uamuzi katika kesi ya kikatiba ya Rufaa Na. 134 ya Mwaka 2022, iliyofunguliwa na mtetezi wa haki za binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rufaa hiyo ilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa: Jaji Rehema Levira, Jaji Wilfred Rumanyika na Jaji Gerald Ngwembe. Wakili Olengurumwa aliwakilishwa na jopo la mawakili maarufu likiongozwa na Prof. Issa Shivji pamoja na Dkt. Rugemeleza Nshala, Mpale Mpoki na Wakili John Seka.

Kesi hiyo ilihusu kupinga vifungu vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, vilivyobadili Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Sura ya 3) kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5). Vifungu hivyo vilionekana kuweka vikwazo katika mashauri ya kikatiba yenye maslahi kwa umma, maarufu kama Public Interest Litigation.

Maelezo ya Vifungu Vilivyolalamikiwa:
Kifungu cha 4(2): Kilihitaji mtu anayetaka kufungua kesi ya kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza namna alivyoathirika binafsi na ukiukwaji huo.

Kifungu cha 4(3): Kiliongeza kizuizi kwa mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji aonyeshe maslahi binafsi sawa na Ibara ya 30(3) ya Katiba.

Kifungu cha 4(4): Kiliweka sharti kuwa kesi dhidi ya viongozi waandamizi serikalini – Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Jaji Mkuu – zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya wahusika hao moja kwa moja.

Kifungu cha 4(5): Kilimtaka mtu anayepanga kufungua kesi kutafuta kwanza nafuu kupitia sheria nyingine zilizopo kabla ya kufungua kesi chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi.

Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania iliitupilia mbali kesi hiyo mnamo Februari 15, 2022, kwa maelezo kuwa vifungu hivyo havivunji Katiba wala mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa vifungu hivyo vinakamilisha Ibara ya 26(2) na 30(3) ya Katiba, na vinaakisi misingi ya utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka, na mfumo wa kimataifa wa haki.

Hata hivyo, Wakili Olengurumwa hakuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka huo huo wa 2022.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa

Leo Juni 13, 2025, Mahakama ya Rufaa kupitia kwa Naibu Msajili Mhe. Joseph Fovo, imesoma uamuzi huo kwa njia ya mtandao na kubatilisha vifungu vyote vinne vilivyolalamikiwa.

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa:

Kifungu cha 4(2) kinavunja dhana ya mashauri ya maslahi kwa umma kwa kuhitaji waathirika binafsi pekee, hali inayokinzana na Ibara ya 26(2) ya Katiba.

Kifungu cha 4(3) ni batili kwa kuwa kinachanganya masharti ya Ibara ya 30(3) (maslahi binafsi) na haki za maslahi kwa umma zinazolindwa chini ya Ibara ya 26(2).

Kifungu cha 4(4) ni batili kwa kuwa Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kikatiba kuwakilisha mihimili mingine, hasa Mahakama au viongozi wa kisiasa walio huru kikatiba kama Jaji Mkuu.

Kifungu cha 4(5) pia ni batili kwa kuwa hakuna sheria nyingine zinazotoa nafuu ya moja kwa moja kwa mashauri ya maslahi ya umma.

Agizo kwa Bunge

Mahakama ya Rufaa imeagiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta vifungu hivyo vinne ndani ya kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe ya hukumu. Uamuzi huu umetajwa kuwa ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu na wananchi wanaotetea masuala ya kijamii kupitia Mahakama.

Taarifa hii imetolewa na mtetezi wa haki za binadamu ambaye pia ndiye aliyekuwa mrufani katika kesi hii, Onesmo Kasale Olengurumwa! Je, Bunge litatii amri ya Mahamaka ya Rufani?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 14 Juni 2025; Saa 2:15 asubuhi
Bunge lao haliwajibiki kutii amri za mahakama, hivyo halitatii na mambo yataendelea kama kawaida.
 
Gentleman,
ni vizuri kuelewa kwamba bunge huru tukufu la Tanzania haliwajibiki kwa muhimili wowote wa dola ya Tanzania, ispokua kwa wananchi wa Tanazania.

There is no way vijana vitatu tu vikae mahali eti halafu vije viwakoromee wawakilishi wa wananchi zaidi ya milioni 64. That one will never happen on earth gentleman.

By the way,
Tanazania itafanya uchaguzi mkuu huru, wa haki na wazi mapema October mwaka huu 2025, kwa gharama zake za ndani. Haihitaji kufadhili wa nje.
Mkumbushe na mwenzako 🐒
Kwa hiyo unataka kusema jaji hajui kazi yake?
 
😂😂😂

Mkumbushe na mwenzako🥶
Huu upuuzi kawadanganye wengine
 
Hao walio kuwa wanakingiwa kushitakiwa, km mahakama ya juu imeamua washitakiwe ni vizuri zaidi. Lakini ningefurahi sana mno km mahakama ingesema wakisha patikana na hatia pamoja na adhabu ya kufungwa haitoshi bali waletwe uwanja wa taifa wpigwe na viboko yaa fimbo za kutosha bila kujali walikuwa na nyadhifa gani.
 
Wala hata bunge halijui mahakama imeagiza nini. Bunge linasikiliza muhimili wa serekali unataka nini, na si mahakama inaagiza nini?
Ila CCM ni wajinga kweli kweli. Yani wao wanadhani wana uhakika wa kuendelea kutawala milele. Wasichojua ni kuwa mambo yanaweza kugeuka mara moja precedence zote za kutumia uhuni badala ya katiba kutawala walizoziweka zikatumika kuwakaanga wao. Hata hii ya rais kuwa na kinga ya kutoshtakiwa siyo salama kama wanavyodhani. Akiingia rais yoyote anaweza kuipuuza kama wao wanavyopuuza sheria za sasa.
 
Back
Top Bottom