15 December 2023
Mbeya, Tanzania
WIMBO MNATUONA MANYANI
Hii ni baada ya jamhuri kuamua kutoendelea na kesi hii iliyovuta umma mpana kuijadili huku ikiituhumu serikali kubana uhuru wa kujieleza.
Wasanii waimbaji Sifa Boniventura Bujune, Salome Mwampeta na Hezekiel Miliyashi walifunguliwa mashtaka mwezi September 2023 kwa kusambaza "ujumbe usio sahihi - false information" chini ya kifungu cha sheria Cybercrime Act 2015 baada ya kuimba wimbo unaoshutumu ukatili wa polisi na utawala usio sikivu (police brutality and irresponsive governance).
Katika wimbo wao wenye title : Mnatuona Mayani , mstari wake mmoja uendao kwa ujumbe 'kijana kangolewa jino lake na Polisi bila sababu' jamhuri iliona mstari huo siyo kweli .
Baada ya kesi hiyo kuendeshwa kwa miezi minne katika mahakama ya wilaya ya Mbeya, leo tarehe 14 December 2023 Hakima wa Wilaya ameamua kuifuta baada ya upande wa jamhuri kuonesha haina niya ya kuendelea na kesi hii iliyoshutumiwa na wananchi kutoka kila kona ya nchi.
Mbali ya wananchi kushutumu kuminywa kwa haki ya wasanii kuelezea hali ya mambo yanayoendelea katika jamii pia wanataaluma na watetezi wa uhuru wa kujieleza kama wakili msomi Fatma Karume rais wa zamani wa TLS, pia Robert Mwampembwa kutoka taasisi ya kukuza ubunifu pia wakili wa kujitegemee Philip Mwakilima walishutumu kesi hiyo waliyoita haina mashiko zaidi ya kuminya uhuru wa kufikiri na kujieleza kupitia majukwaa mbalimbali.