- Thread starter
- #41
Kutoa hukumu dhidi ya mtu aliyekuteua ni almost haiwezekani..!!!
Pia hawachapishi hukumu zao kwa wakati, hata mtandao wa TANZLII Home - TanzLII wa kieletroniki hauna hukumu zote za kesi mkakati :
16 April 2024
Dar es Salaam, Tanzania
NGULI WA SHERIA WAKUTANA JUKWAA MOJA, UZINDUZI KITABU CHA MWAKA CHA KESI ZA UMMA 2022.. TANZANIA YEARBOOK PUBLIC LAW 2022
View: https://m.youtube.com/watch?v=aA9LchsP9uo
Majumuisho ya kesi mkakati zilizotolewa tangu miaka ya nyuma kuanzia 1983 hadi 2022 na maamuzi ya hukumu yakiangaziwa kwa kina kuona maamuzi ktk hukumu hizo
Ambazo Tanganyika Law Report walijitahidi kuchapisha zilizolenga kesi mashuhuri zilizowahi zilizosikilizwa Tanzania kwa ajili ya rejea kwa wadau wa sheria na umma kwa ujumla wanaotaka kufahamu kesi mkakati za masuala kama ya kisiasa, haki za binadamu, kijamii, kiuchumi.
Miaka 10 hadi sasa Tanganyika Law Report walikuwa hawajawahi kuchapa. Kazi data huwezi kuzipata katika mtandao wa TANZLII Home - TanzLII , hivyo kitabu hiki cha leo kitakuwa na mambo mengi mazito yaliyowahi kufika mbele ya mahakama zetu za Tanzania
Manguli wa sheria jaji mstaafu O Chande wa Tanzania,, Dr. Willy Mutunga – Chief Justice Republic of Kenya, (2011-2016) Jenerali Ulimwengu, prof. Issa Shivji na wengine wanatoa maoni ya haki za jinai mapungufu ya 2019 ya Plea Bargain, Kesi ya Mtikila, Makampuni, maslahi ya umma kuanzia 1983 hadi 2022 na kitakuwa kinatoka kila mara kuangali jinsi zinavyoamuliwa na manguli hawa wa Yearbook kukosoa inapobidi ....