Wakili Mkuu: Jaji Mkuu kuongezewa muda, ni sahihi Kikatiba

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
305
519
JAJI MKUU KUONGEZEWA MUDA NI SAHIHI KIKATIBA

Tarehe 22 Septemba, 2023; Mahakama Kuu (Masijala Kuu) Dar es salaam ilitoa uamuzi katika shauri la Kikatiba Na. 07/2023 baina ya Humphrey Simon Malenga dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutupilia mbali shauri hilo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mahakama imefikia uamuzi huo wa kutupilia mbali shauri hilo (dismissed) kupitia Mhe. Jaji G. N. Isaya kwa sababu zifuatazo:-

(i) Jaji Mkuu wa Tanzania ana sifa kama Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani na hawezi kutenganishwa na Majaji wa Mahakama hiyo kwa mujibu wa ibara ya 118 (2);

(ii) Ibara ya 118 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kusimama yenyewe kwa sababu inafanya marejeo katika ibara ya 120(1) ambapo ibara ya 120 (1) inasomwa kwa pamoja na ibara ya 120 (2) & (3); na

(iii) Mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumuongezea muda Jaji Mkuu wa Tanzania yalikuwa sahihi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ibara ya 120 (2), (3) & (4) inatumika pia kwa Jaji Mkuu.

Hivyo, kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuongezea muda Jaji Mkuu wa Tanzania hakikuwa kinyume na katiba (it was constitutional).

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilishiriki kwenye Shauri tajwa hapo juu kwa mujibu wa majukumu yake ya kusimamia na kuendesha mashauri ya madai, usuluhishi, katiba, uchaguzi na haki za binadamu kwa niaba ya Serikali na taasisi zake.

Imetolewa na:

Prisca J. Ulomi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
23 Septemba, 2023

IMG-20230923-WA0031.jpg
 
Kuongezewa muda kwa profesa kunasaidia kumpa sifa yule Jaji kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa kupata sifa za kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu pale profesa "atakapostaafishwa" (maana yeye alishastaafu)
 
JAJI MKUU KUONGEZEWA MUDA NI SAHIHI KIKATIBA

Tarehe 22 Septemba, 2023; Mahakama Kuu (Masijala Kuu) Dar es salaam ilitoa uamuzi katika shauri la Kikatiba Na. 07/2023 baina ya Humphrey Simon Malenga dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutupilia mbali shauri hilo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mahakama imefikia uamuzi huo wa kutupilia mbali shauri hilo (dismissed) kupitia Mhe. Jaji G. N. Isaya kwa sababu zifuatazo:-

(i) Jaji Mkuu wa Tanzania ana sifa kama Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani na hawezi kutenganishwa na Majaji wa Mahakama hiyo kwa mujibu wa ibara ya 118 (2);

(ii) Ibara ya 118 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kusimama yenyewe kwa sababu inafanya marejeo katika ibara ya 120(1) ambapo ibara ya 120 (1) inasomwa kwa pamoja na ibara ya 120 (2) & (3); na

(iii) Mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumuongezea muda Jaji Mkuu wa Tanzania yalikuwa sahihi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ibara ya 120 (2), (3) & (4) inatumika pia kwa Jaji Mkuu.

Hivyo, kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuongezea muda Jaji Mkuu wa Tanzania hakikuwa kinyume na katiba (it was constitutional).

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilishiriki kwenye Shauri tajwa hapo juu kwa mujibu wa majukumu yake ya kusimamia na kuendesha mashauri ya madai, usuluhishi, katiba, uchaguzi na haki za binadamu kwa niaba ya Serikali na taasisi zake.

Imetolewa na:

Prisca J. Ulomi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
23 Septemba, 2023

View attachment 2759448
JE BUNGE KUWA NA WABUNGE 19 WASIO NA CHAMA NI HALALI KWA MUJIBU WA KATIBA?
 
Back
Top Bottom