Mahakama: BAKWATA si Chombo cha Waislam wote

Mahakama: BAKWATA si Chombo cha Waislam wote

Mimi ni mwislamu mkuu 😂. Lakini napenda haki itendeke.
Yaani mimi niko tofauti na hizo Taasisi ,bahati nzuri nimesoma markazi tatu pale Tanga : Zahrau , Shamsil na Nurul huda...So sijui mambi ya ushabiki wa Taasisi wala sina page Taasisi zaidi ni mashekhe tu wanaotoa masomo mbalimbali kama Osma maalim na kishki, hata yule Jalala namfutilia ni wa nyumbani... Sheikh Mkubwa wa BAKWATA ni wa nyumbani ila ni vile sipendi ushabiki wa Taasisi..
 
Leta ushahidi
Unataka risiti au nakala za cheki?.. BAKWATA ipo kulinda mfumo kristo,ukiondoa BAKWATA unabaki na akina ponda na sheikh kundecha,miaka miwili tu CCM chali, mfumo kristo chali
 
Unataka risiti au nakala za cheki?.. BAKWATA ipo kulinda mfumo kristo,ukiondoa BAKWATA unabaki na akina ponda na sheikh kundecha,miaka miwili tu CCM chali, mfumo kristo chali
Sisi wakristo tunamtaka Shehe Ponda, ambaye ni msomi na mpenda haki. Asiyehongwa Ubwabwa
 
SHEIKH PONDA - WAISLAMU TULIKUWA TUNABURUZWA NA SERIKALI KUPITIA BAKWATA, HUKUMU YA LEO IMETUPA UHURU WAISLAMU


View: https://m.youtube.com/watch?v=__5LhMXnxxE

Mapema kesi ilifunguliwa na Sheikh Ayoub Salim Muinge, Sheikh Prof. Hamza Mustafa Njozi, Sheikh Ponda Issa Ponda, Bi. Riziki na wengine


View: https://m.youtube.com/watch?v=GdMvflxOZtU


24 December 2025

MWANASHERIA MKUU WA BAKWATA AELEZEA MAANA YA HUKUMU YA LEO ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA. SHEIKH PONDA ANAPOTOSHA ​


View: https://m.youtube.com/watch?v=xr0sVtqVUcg
BAKWATA wasema kina Sheikh Ponda wanaleta taharuki kwa umma asisitiza mwanasheria wakati akiongoa na waandishi ili kuweka mambo sawa kufuatia hukumu ya kesi namba 27063 / 2924 iliyotolewa na masjala ndogo ya Mahakama Kuu ya Tanzania

Kesi 27063 / 2924 iliyokuwa inasikilizwa na jopo la majaji Mwanga, Mbangwa na Mwizu ambapo waislamu walilalamikia registrar of civil society, administrator general kwa kwenda kinyume na ibara za katiba, ibara ya 13 usawa mbele ya sheria na ibara 19 ya uhuru wa kuabudu na ibara ya 20 ijayohusu kujumuika na wengine ambayo wasalili hao wawili wamekuwa wakiwataka watu kwenda kupata barua ya utambulisho kutoka BAKWATA na hali hii inakwenda kinyume na ibara 13, ibara 19 na ibara ya 20 zote zilizo ktk Katiba ya Jamhuri ya Muungano

Supreme society ni ipi hiyo ni BAKWATA (1968) au ...
 
KESI YA SHEIKH PROF. NJONZI, SHEIKH PONDA & OTHERS NAMBA 27063 / 2924

1766680891659.jpeg
 
Chadema wanaunga mkono harakati zozote zinazoipinga ccm hata kama zina fubaza usalama wa nchi hii

Maoni yangu waislam wacheze karata zao vizuri wasije ingia mtego wa divide and rule policy
 
Bakwata ni kikundi cha wahuni, chenye kuijua dini, wanaitumia dini kwaanufaa yao wenyewe.
Nilishangaa hivi karibuni kabla ya Dec 9, masheikh wakubwa kabisa wanaita press kumjibu Mange.
Masheikh wanamchamba mange, pale ndio niliona kuna tatizo.

Masheikh wanaojilewa hawapaswi kabisa kuhangaika na mange
 
Kila kitu kina ubaya na uzuri wake, Bakwata ni mpango wa ccm kufubaza makali ya extremist Muslim nchi hii na uliasisiwa na Nyerere

Lakini pamoja na hayo kusingekuwa na hiyo Taasisi nchi hii isingekalika kwa uhasama wa kidini

Lakini pia waislam wangeonewa sana kwenye taasisi za kiserikali maana wagalatia wamejazana humo na wanafanya majengo ya Serikali kama makanisa kwa waliosoma Iringa, mbeya watatoa ushahidi

Bakwata ipingwe kwa ustaraabu Ina mazuri yake mengi tu kwa waislamu wa nchi hii japo kuna mengi pia inakosea mfano kupanga sherehe za kidini kuendana na ratiba ya viongozi na mengine mengi
 
Leo waislam wameshinda kesi waliofungua dhidi ya BAKWATA kujipa mamlaka ya kuwaongelea waislam na kukwamisha miradi Kwa ukiritimba ati wao ndo watoe vibali Kwa taasisi zingine za kiislam

Shehe Ponda amesema mahakama katika hukumu hiyo, mahakama imeitamka kuwa BAKWATA sio taasisi inayosimamia Waislam wote Bali wale waliohiari kuwa chini ya taasisi ya BAKWATA

Pia Shehe Ponda ameahidi kuandaa kongamano kutoa elimu juu ya umuhimu wa hukumu ya Leo Kwa waislam
Assalam Alyekum

=======

WAISLAMU WAISHINDA KESI DHIDI YA SERIKALI NA BAKWATA MAHAKAMA KUU LEO 24/12/2025.

Majaji watatu leo wametoa hukumu ya kesi ya kikatiba iliyowasilishwa na Waislamu 12, Novemba 2024. Katika kesihiyo Waislamu hao walikuwa wanadai uhuru kwa Waislamu wa Tanzania wa kujiamulia mambo yao bila ya kulazimishwa kuwa chini ya taasisi nyingine yoyote ikiwemo BAKWATA.

Walioshitakiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama Wizaraya Mambo ya Ndani, RITA, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na pia Bakwata na Baraza Kuu waliunganishwa.

Katika hukumu hiyo (ndefu), Jaji Mkwizu kwa niaba yamajaji wenzake 2, (waliokuwepo Mahakamani), alisema kwamujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waislamu kama raia wengine, wako huru kuendesha shughulizao za kidini bila ya kulazimishwa kuwa chini ya chombochochote.

Jaji aliyasema hayo baada ya kusoma nyaraka kadhaa za vyombo hiyo vya serikali na Bakwata ambazo maudhui yake yanawalazimisha Waislamu kuwa chini yao kabla ya kupewa huduma zinzotolewa na mamlaka za serikali.

Akifafanua zaidi baada ya kunukuu vifungu vya Katiba ya Bakwata na Katiba ya nchi, alisema kwa mujibu wa sheria hizo Bakwata si Taasisi mama ya taasisi zote za Waislamu wala haina hadhi hiyo kwa Waislamu wote wa Tanzania.

Hukumu hiyo imezitaka mamlaka za serikali RITA na Msajili Wizara ya Mambo ya Ndani kuzingatia uhuru wa Waislamu kama raia wengine wanapohitaji haki zao za msingi kutoka kwao.

Hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu imewapa uhuru vyombo vya serikali na Bakwata wa kukata rufaa endapo wanahisi hawakuridhika na hukumu hiyo.

Miongoni mwa matatizo wanayoyapata Waislamu waTanzania kutokana na kulazimishwa kuwa chini ya chombo kimoja ni pamoja na kukosa haki sawa na dini nyingine pale panapotakiwa uwakilishi au mgao wa haki mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Kutokana na hukumu hii taasisi zilizoingizwa kwa hila bila yahiyari yao chini ya Bakwata au chombo kingine chochote, ziko huru kuendelea kua chini ya Baraza hilo au kujitoa nakuendesha mambo yake zikiwa huru.

Aidha waislamu waliopeleka shauri hilo Mahakamani (chiniya udhamini wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania), wanaandaa utaratibu utakao wezesha Misikiti yote na Taasisizote za Kiislamu Tanzania kupata hukumu hiyo kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza ili waweze kuona uhuru wanaoupata kutokana na hukumu hiyo.

Ust. MUSTAFA M. ABEIDI

MSEMAJI WA JOPO LA WALIOSHITAKI - 0785998872
BAKWATA nashauri wasikate rufaa maana waislamu wengi hatutaki na ni batili hatuitambui
 
Yaani mimi niko tofauti na hizo Taasisi ,bahati nzuri nimesoma markazi tatu pale Tanga : Zahrau , Shamsil na Nurul huda...So sijui mambi ya ushabiki wa Taasisi wala sina page Taasisi zaidi ni mashekhe tu wanaotoa masomo mbalimbali kama Osma maalim na kishki, hata yule Jalala namfutilia ni wa nyumbani... Sheikh Mkubwa wa BAKWATA ni wa nyumbani ila ni vile sipendi ushabiki wa Taasisi..
Vyema mkuu, ushabiki hausaidii.
 
TOKA MAKTABA:

MZEE MOHAMED SAID - BAKWATA MWIBA MZITO KWA WAISLAMU WA TANZANIA

Sheikh Mohamed Said akitoa muhadhara kwa vijana wa kiislamu kufahanu historia ya taasisi za kiislamu Tanzania na michango ya taasisi hizi :

View: https://m.youtube.com/watch?v=IvodWTgWpSM
East African Muslim Welfare Society, migongano ya waislamu tanzania kwa kufuata asili ya mtu.

Mambo yakawa mazito 1968 muafaka miongoni mwa waislamu wa Tanzania ukashindwa kufikiwa.

Kina mama wa kiislamu watokwa macho kwa hali hii ya waislamu kuhitafiliana kwa kuangaliana asili, badala ya kuwa umma mmoja usio na chembe za kibaguzi .

Kuanzia hapo maendeleo na mipango ya waislamu ikavuzurugika, makundi ndani ya uislamu Tanzania yakaibuka

Wafadhili waliotaka kujenga Chuo Kikuu chini ya ufadhili wa Aga Khan wakatoweka kutokana na kutofautiana waislamu ndani ya Tanzania

Mzee Mohamed Said akaendelea na mudhara wake akawapa changamoto wanafunzi kama wanaelewa kwanini wanavaa hijabu, haikuwa kazi ndogo nitawaeleza ..
 
Back
Top Bottom