Leo waislam wameshinda kesi waliofungua dhidi ya BAKWATA kujipa mamlaka ya kuwaongelea waislam na kukwamisha miradi Kwa ukiritimba ati wao ndo watoe vibali Kwa taasisi zingine za kiislam
Shehe Ponda amesema mahakama katika hukumu hiyo, mahakama imeitamka kuwa BAKWATA sio taasisi inayosimamia Waislam wote Bali wale waliohiari kuwa chini ya taasisi ya BAKWATA
Pia Shehe Ponda ameahidi kuandaa kongamano kutoa elimu juu ya umuhimu wa hukumu ya Leo Kwa waislam
Assalam Alyekum
=============
Kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu, Masijala ya Dar es Salaam, iliyotolewa leo Desemba 24, 2025 imebainishwa rasmi kuwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) si chombo kinachowakilisha Waislamu wote nchini. Katika uamuzi huo, Mahakama imerejea Katiba ya BAKWATA yenyewe ambayo inatambua dhehebu moja pekee la Ahlus Sunnah Wal Jama’ah (maarufu kama Sunni).
Uamuzi huu unaliweka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika hadhi sawa na vyombo vingine vya kidini, kama vile Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Hii ina maana kuwa madhehebu mengine ya Kiislamu, yakiwemo Shia, Ibadhi, Salafi (Mawahabi), na Ahmadiyya, kisheria hayatabanwa tena na mamlaka ya BAKWATA katika kujisimamia. Madhehebu haya sasa yana uhuru wa kisheria kuratibu mambo yao yenyewe, ikiwemo kutangaza mwandamo wa mwezi kwa ajili ya kuanza au kumaliza funga, kusimamia masuala ya ndoa, talaka, na mirathi, pamoja na kupata uwakilishi wa moja kwa moja katika shughuli rasmi za kijamii na kiserikali. Aidha, uamuzi huu unazipa taasisi hizo uwezo wa kusajili jumuiya zao bila kuhitaji ridhaa au udhamini wa BAKWATA kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa maelezo rahisi, kama ambavyo Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) hutoa matamko kwa niaba ya waumini wa Kanisa Katoliki pekee, ndivyo BAKWATA inavyopaswa sasa kutoa matamko kwa niaba ya Waislamu wa Sunni. Jambo linalobaki kuwa swali la msingi ni ikiwa BAKWATA italazimika kubadili jina lake ili liendane na uhalisia huo wa kisheria, kwa kuitwa Baraza la Waislamu wa Kisunni Tanzania au Baraza Kuu la Masunni Tanzania, ili kuondoa mkanganyiko wa uwakilishi wa Waislamu wote nchini.
View attachment 3520003