Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,645
Umeshawahi kumwambia mwenzi/mwenza wako kwa Kiswahili au kwa lugha ya kabila lako kuwa unampenda kama vile wasemavyo waongeaji wa lugha ya Kiingereza 'I love you'?
Unasemaje 'I love you' kwa Kiswahili? Kusema 'nakupenda' hata haiji kabisa. Matokeo yake na sisi Waswahili tukitaka kuonesha mahaba kwa wapenzi wetu tunajikuta tunaambiana 'I love you'. Yaani kwa Kiswahili hatuna kabisa msemo wa kimahaba utumikao kuonesha mapenzi/ mahaba kwa tuwapendao?
Au hata kusema 'I miss you'....kwa Kiswahili unasemaje - 'nimekukumbuka'? Yaani bado haiji. Kwa nini inakuwa hivi lakini? Ni kwamba lugha zetu na tamaduni zetu sio za kimahaba mahaba au? Maana hata mambo ya kukumbatiana (hug) kwa mfano, sidhani kama ni moja ya sehemu kubwa ya mila na tamaduni zetu. Au hata busu. Kubusiana mimi naona kama tumeiga vile kutoka kwa wazungu. Tena kulana denda ndio kabisaa tumeiga. Sidhani kama mababu na mabibi zangu kule Kolandoto na Nyakabindi walikuwa wanakulana denda wakati wakilana uroda.
Wadau mna maoni gani?