GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,638
- 109,006
"Tumevitaka Vyombo vyote vya Habari nchini hasa kwa Watangazaji wa Redio na Runinga kutumia tu Lugha ya Kiswahili wawapo Hewani na siyo Kuchanganya Kiswahili na Kiingereza. Na kibaya zaidi unamsikia Mtangazaji anachanganya hizo Lugha halafu hata hilo neno lenyewe la Kiingereza hajui kulitamka au analikosea ila ilimradi tu nae ajitutumue kwa Wasikilizaji ili wajue kuwa Wanakijua" amesema Afisa Mwandamizi wa TCRA jana ( Alhamisi ) alipokuwa katika Studio za EFM Radio.
Haya TCRA nami GENTAMYCINE nawashauri ili hili Tamko lenu ( Mkwara Mbuzi wenu huu ) ukubalike kwa Wadau wenu ( Watangazaji ) mngeweka Sheria itakayoambatana na Faini Kubwa kwa Mtangazaji na Chombo husika ili Lifanikiwe vinginevyo naona ni kama vile mnapaka tu Rangi Upepo.
Ninakipenda mno Kiswahili changu.