Mahaba na lugha zetu

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,647
Umeshawahi kumwambia mwenzi/mwenza wako kwa Kiswahili au kwa lugha ya kabila lako kuwa unampenda kama vile wasemavyo waongeaji wa lugha ya Kiingereza 'I love you'?

Unasemaje 'I love you' kwa Kiswahili? Kusema 'nakupenda' hata haiji kabisa. Matokeo yake na sisi Waswahili tukitaka kuonesha mahaba kwa wapenzi wetu tunajikuta tunaambiana 'I love you'. Yaani kwa Kiswahili hatuna kabisa msemo wa kimahaba utumikao kuonesha mapenzi/ mahaba kwa tuwapendao?

Au hata kusema 'I miss you'....kwa Kiswahili unasemaje - 'nimekukumbuka'? Yaani bado haiji. Kwa nini inakuwa hivi lakini? Ni kwamba lugha zetu na tamaduni zetu sio za kimahaba mahaba au? Maana hata mambo ya kukumbatiana (hug) kwa mfano, sidhani kama ni moja ya sehemu kubwa ya mila na tamaduni zetu. Au hata busu. Kubusiana mimi naona kama tumeiga vile kutoka kwa wazungu. Tena kulana denda ndio kabisaa tumeiga. Sidhani kama mababu na mabibi zangu kule Kolandoto na Nyakabindi walikuwa wanakulana denda wakati wakilana uroda.

Wadau mna maoni gani?
 
I miss you = nimekukumbuka au nimekukosa, I love you= nakupenda
Kuigana hakuna tatizo, zamani wazungu wengi walikuwa hawapendi wanawake wenye wowowo lakini siku hizi na wanalipenda sana hilo na hata wanawake wa kizungu hufurahia kuwa na wowowo ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa ni english figure tu mtu yuko kama namba moja wenyewe wanaita portable.
 
Lakini kumwambia mtu 'nimekukumbuka' na kumwambia 'I miss you' ni kama vile unasema vitu viwili tofauti. Something ain't right and I just can't put my finger on it....au chukulia kwa mfano, unaongea na kabinti kako kwenye simu halafu kanakwambia 'I love you daddy'.....kwa Kiswahili utasemaje...'nakupenda baba'.......sijui...lakini kwangu mimi ina sound awkward kidogo
 
Hahahahahahaha nakubaliana nawe kwamba kuna maneno mengine yanapendeza zaidi kwa kizungu kuliko kiswahili, lakini pamoja na hayo bado kuna haja ya kuitukuza lugha yetu ya Taifa ati!

Hakika! Haja ya kuienzi, kuitukuza, na kuipenda lugha yetu ipo na ningependa ikue na iwe kubwa kuliko ilivyo sasa.
 
Nyani,
Kiswahili ni lugha practical. Ni mara chache inakuwa abstractive. Kama umemmiss mpenzi wako mwambie tu nimekuwa mpweke bila wewe.
It is straight forward.
 
Na 'I love you baby' unasemaje?
 
nakupenda sana mpenzi wangu. siwezi kuishi bila ya wewe yaani natamani ninywe sumu ili nikukose wewe nikinywa maji nakuona kwenye glasi

Dah! A lot of words; wakati kwa kingereza, ukishasema, "I love you", ina maanisha yote hayo...
Ila kweli bwana NN, hilo tatizo nimeliona siku nyingi sana... Hata fikiria pia; ukisema, "I hate you..." au "nakuchukia..." ipi inauma sana???
 
Gosh ninywe sumu mie harafu yeye nimwache aendelee kuserebuka? ........No No No.
 
Tunafanya makosa kujaribu kutafsiri kiingereza kwenda kiswahili, moja kwa moja. Lugha inaunganisha pia na utamaduni wa jamii husika.
Nadhani ni makosa kutafuta maana ya 'i love u' , ' i miss u' nk katika kiswahili.
Haya maneno inafaa yatumike kwa kiingereza kwa sababu yanaendana na utamaduni wa uingereza.
La msingi hapa ni kutafuta jinsi mapenzi yanavyoenda kwa utamaduni wa mswahili ama msukuma badala ya kutafsiri.
 
Sifungwi na haya maneno! nayatumia kadri ninayopenda ilimradi nimetamka kitu kwa mpenzi wangu ambacho ni kiwakilishi cha feelings zangu wakati huo!
 
Umeshawahi kumwambia mwenzi/mwenza wako kwa Kiswahili au kwa lugha ya kabila lako kuwa unampenda kama vile wasemavyo waongeaji wa lugha ya Kiingereza 'I love you'?

Au hata kusema 'I miss you'....kwa Kiswahili unasemaje - 'nimekukumbuka'? Yaani bado haiji. Kwa nini inakuwa hivi lakini? Ni kwamba lugha zetu na tamaduni zetu sio za kimahaba mahaba au? Maana hata mambo ya kukumbatiana (hug) kwa mfano, sidhani kama ni moja ya sehemu kubwa ya mila na tamaduni zetu. Au hata busu. Kubusiana mimi naona kama tumeiga vile kutoka kwa wazungu. Tena kulana denda ndio kabisaa tumeiga. Sidhani kama mababu na mabibi zangu kule Kolandoto na Nyakabindi walikuwa wanakulana denda wakati wakilana uroda.

Wadau mna maoni gani?

Mkuu umenikumbusha mbali sana unajua kuna kipindi nilikuwa napita mitaa ile ya Bariadi......
 
NN Naona kama unajaribu zaidi kupinga jaribio lolote la kutafuta kiswahili chochote cha kuonesha mapenzi otherwise mi naona kama wakuu wengi juu hapo wamekupa sentensi nzuri tu zinaloleta ladha nzuri katika mahaba. Mimi nadhani mzee uko addicted sana na english love phrases kiasi kwamba hudhani kama kuna lugha nyingine inayoweza kuwa romantic zaidi ya Kiingereza!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Dah! A lot of words; wakati kwa kingereza, ukishasema, "I love you", ina maanisha yote hayo...
Ila kweli bwana NN, hilo tatizo nimeliona siku nyingi sana... Hata fikiria pia; ukisema, "I hate you..." au "nakuchukia..." ipi inauma sana???

Haloo una tatizo la kupenda sana kiingereza
 
NN Naona kama unajaribu zaidi kupinga jaribio lolote la kutafuta kiswahili chochote cha kuonesha mapenzi otherwise mi naona kama wakuu wengi juu hapo wamekupa sentensi nzuri tu zinaloleta ladha nzuri katika mahaba. Mimi nadhani mzee uko addicted sana na english love phrases kiasi kwamba hudhani kama kuna lugha nyingine inayoweza kuwa romantic zaidi ya Kiingereza!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Maneno ya Kingereza yanaleta hisia zaidi kuliko ya kiswahili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom