Magufuli wewe ni mzazi unayejitambua

Magufuli wewe ni mzazi unayejitambua

Acha kupotosha, wasipewe elimu..kwani hawapewi?? mimba inapatikana kwa kufanya ngono, ukimwi pia..nashangaa mnashikilia kujadili matokeo badala ya kufikiria kile tamko linataka kutatua..mtoto hatakiwi afanye ngono! ili asipate ukimwi na amalize masomo yake vzr kwa ajili ya maisha yake na taifa kwa ujumla.
Tamko linataka kutatua nini? Tumekwambia kuna sheria, acha tamko, inayozuia watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo. Elewa kwamba tamko halitazuia wanafunzi kufanya ngono kwa kuwa wanafahamu tangu zamani kwamba wakifanya ngono wakapata mimba hawataruhusiwa kuendelea na masomo.

Tamko limeingilia mjadala ulioibuka baada ya kuona sheria zimeshindwa kuwa suluhisho kwenye tatizo la wanafunzi kupata mimba. Wenye wisdom wakaona wawe na mjadala wenye lengo la kuwasaidia hawa mabinti kuendelea kupata elimu kwa kuwa, sheria hiyo licha ya kushindwa lakini inaongeza idadi ya wajinga. Hawa wanafunzi wanakosa elimu, watoto wanaowazaa nao wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kukosa elimu, pengine hata wajukuu watakosa elimu; nakadhalika.

Na mjadala huo ndio ulikifanya CCM kuweka kwenye Ilani yake kipengele kinachoonyesha kuwa kama kingepewa ridhaa ya kuongoza serikali kingewaruhusu wanafunzi wanaopewa ujauzito kuendelea na masomo ili wapate elimu, waondokane na ujinga pengine wakuzidi kuzalishwa hovyo, na hata kuwa katika hatari ya kuambukizwa ukimwi. Hii ndio hoja.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nchi sio familia ndugu yangu.
Nchi haiongozwi kwa hisia, inaongozwa kwa umakini na kutumia akili nyingi.

Hebu jiulize, ni lini wanafunzi waliozaa walisomeshwa na serikali?????

Kama jibu ni hakuna, basi kauri hiyo ni mbaya sana maana inalenga kuwatenga na kuwanyanyapaa watoto wanaopata mimba.

Unajua madhara yake??
Tutazika sana watoto waliokua wakijaribu kutoa mimba ili aibu hiyo isiwakute

Tutasikia matukio mengi ya kujiua kwa watoto waliopata mimba

Suala la mimba kwa watoto, linasababishwa na mambo mengi. Hayo mambo ndo ilitakiwa tupambane nayo. Kumbuka kutompa elimu mama mmoja, ni kutoipa elimu jamii nzima

Busara kwenye uongozi ni kitu cha muhimu sana
Kachukue fomu na wewe
 
Nitashangaa wanawake kumuumga mkono Magufuli!!Samia Suluhu sijui anajisikiaje huko aliko!
usiishie kupiga kelele hapa, kuonyesha unawathamini unaowatetea weka boksi la kondom nyumbani kwako kwa ajili ya watoto ili hata usipate shida kusema mara kwa mara..
 
Mfumo wa elimu ya msingi na sekondari shule ina vyombo na kamati kuzuia na kuondoa changamoto zote wanazopata watoto, wabakaji hawatoki mbiguni ni miongoni mwa jamii shule ilipo..kama wazazi wana nia watoto wao wasome na kufaulu vyema kesi za ubakaji haziwezi kuwepo! tamko la Rais linaelekeza pia kila mmoja afanye wajibu wake ipasavyo, huwezi kukimbilia kurekebisha kosa badala ya kuzuia lisitokee! utakuwa sio mjinga tu ni mp.umba.vu wa mwisho!
Hapo ndio nazidi kuwaona wajinga wa kiwango cha juu!
Unadhani watoto wote wanaopata mimba ni kwamba wazazi hawatimizi wajibu wao??Kama unafikiri hivyo then utakuwa na walakini!Kuna watoto wengi sana ambao wamelelewa vema na familia zao lakini wameishia kupewa ujauzito!Kuna mambo ambayo huwezi kupata ufumbuzi wa kudumu,unachoweza ni kupunguza wahanga!
Tumieni na akili zenu kufikiri,sio kila mnachoambiwa mnameza tu kama kilivyo!
 
Tamko linataka kutatua nini? Tumekwambia kuna sheria, acha tamko, inayozuia watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo. Elewa kwamba tamko halitazuia wanafunzi kufanya ngono kwa kuwa wanafahamu tangu zamani kwamba wakifanya ngono wakapata mimba hawataruhusiwa kuendelea na masomo.

Tamko limeingilia mjadala ulioibuka baada ya kuona sheria zimeshindwa kuwa suluhisho kwenye tatizo la wanafunzi kupata mimba. Wenye wisdom wakaona wawe na mjadala wenye lengo la kuwasaidia hawa mabinti kuendelea kupata elimu kwa kuwa, sheria hiyo licha ya kushindwa lakini inaongeza idadi ya wajinga. Hawa wanafunzi wanakosa elimu, watoto wanaowazaa nao wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kukosa elimu, pengine hata wajukuu watakosa elimu; nakadhalika.

Na mjadala huo ndio ulikifanya CCM kuweka kwenye Ilani yake kipengele kinachoonyesha kuwa kama kingepewa ridhaa ya kuongoza serikali kingewaruhusu wanafunzi wanaopewa ujauzito kuendelea na masomo ili wapate elimu, waondokane na ujinga pengine wakuzidi kuzalishwa hovyo, na hata kuwa katika hatari ya kuambukizwa ukimwi. Hii ndio hoja.
Kuwa na sheria ni moja utelezaji wa sheria ni kitu kingine..wapi na nani alisema sheria zilizopo zimeshindwa?? basi msimamizi wa sheria kapatikana, subiri uone..fuata hicho anachosema.
 
Mbona mnawatetea sana hawa mabinti wanaopata mimba na mnataka waruhusiwe kusoma. Vipi wanafunzi wenzao wanaowapa ujauzito mbona sio wanaowatetea kuwa wasishitakiwe?
 
Je ilikuwa ni free style kama ya bongo fleva yani unafuata vina au yaliandikwa Yale.....maana nasikia Joh makini ni mkali wa free style ndio tunavyoambiwa.
 
Huyo binti kwenye picha hawezi kufaulu vizuri anasoma ili maradi tu atimize wajibu ili apate cheti chenye miswaki mingi ambacho hakitamfikisha popote. Tusishangulie kusoma tu! Ili ufaulu vizuri, unapaswa kuweka mkazo kwenye kile unachosoma, kulea mtoto huku unasoma kunapunguza concetration ya kwenye masomo. Hivyo basi ukipata mimba halafu urudi shule sidhani kama utafaulu vizuri na ukapata cheti kitakacho kuwezesha kuendelea na ngazi zingine za juu za masomo. Utapoteza muda, nguvu na mali zako. Kwani wakivumilia hiyo miaka ili wamalize masomo yao kuna kitu wanapungukiwa? Naungana na rais, wanaopata mimba wasiendelee na masomo, walee watoto na baadae waende veta kwa masomo ya ufundi tu

nakuona umekua mtabiri maarufu zaidi ya shekh Yahaya, we umejuaje kama hatofaulu? una roho mbaya kama ya yule mtoa kauli yako
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapo ndio nazidi kuwaona wajinga wa kiwango cha juu!
Unadhani watoto wote wanaopata mimba ni kwamba wazazi hawatimizi wajibu wao??Kama unafikiri hivyo then utakuwa na walakini!Kuna watoto wengi sana ambao wamelelewa vema na familia zao lakini wameishia kupewa ujauzito!Kuna mambo ambayo huwezi kupata ufumbuzi wa kudumu,unachoweza ni kupunguza wahanga!
Tumieni na akili zenu kufikiri,sio kila mnachoambiwa mnameza tu kama kilivyo!
unachoweza kuwaza na kufikiri ni cha level ya familia yako..akili haifikiri kabisa kile serikali inalenga kwa watu wake sasa na siku zijazo,
 
unachoweza kuwaza na kufikiri ni cha level ya familia yako..akili haifikiri kabisa kile serikali inalenga kwa watu wake sasa na siku zijazo, jaza huo ujinga kichwani..utakusaidia?
Ewe kizazi cha nyoka usiyeamini bila kuona,subiri uje upate matokeo ya uamuzi wa serikali pengine akili kidogo itakurudia!
 
Mkuu ungemwambia anaroho mbaya peke yake tu ningelike sasa umemtaja na mwingine. Uwiiii kulike huku wengine twaogopa Noah

mkuu hiyo ni kwa wenye akili tu ndio wataelewa ila kisheria nawatoa kapa asubuhi kweupeee, sihitaji hata ku hire wakili maaana sijamtaja jina faru john wala faru fausta
 
View attachment 530269

--- Kama umasikini ndio chanzo cha kupata mimba kwa wanafunzi wa kike, kwanini shule nzima wasiwe na mimba? Kama umbali wote wanatoka mbali na wanaishi katika mazingira yanayofanana.

--- Eti wanadai ni haki ya mtu kupata elimu kwa maana kuwa na elimu ndio silaha ya kwanza ya kupambana na umasikini. Hiyo ni sawa. Lakini haki ni lazima iendane na wajibu (to get your Rights you should behave responsibly)

--- Wengine wanadai eti serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa maadili mabovu kwa maana wao ndio wametufikisha hapa kwa miaka 50 ya utawala wao. Ninasema hapana. Serikali haiwezi kuja nyumbani kwako ikakwambia baba na mama flani sasa zimeni TV ili mtoto wenu aache kuangalia cartoons afanye homework yake. Huo ni mfano tu juu gani ya wazazi wanapaswa kutimiza wajibu wao katika maadili ya watoto.

Huku uswahilini ninapokaa sio jambo la kushangaza kukutana na mtoto wa kike darasa hata la 3 usiku wa 4 eti ametoka kwende kibanda kuangalia movie. Hivi binti kama huyu akibakwa na kupata mimba (achilia mbali magonjwa mengine) italaumiwa serikali? Let's be serious guys.

JPM stay focused. Wewe ni mazazi unayejitambua sana.

Mwenye macho na asome.

Nimemaliza.

View attachment 530265
Sasa unauliza kama Magufuli nae ni mzazi. Magufuli sio mzazi kama unakumbuka amewahi kutuumiwa kuwa alitembea na binti yake na binti akajiua. Sasa mtu kama huyo atakuqa na huruma ya watoto aa wenzie kama wake kamla
 
Kuwa na sheria ni moja utelezaji wa sheria ni kitu kingine..wapi na nani alisema sheria zilizopo zimeshindwa?? basi msimamizi wa sheria kapatikana, subiri uone..fuata hicho anachosema.
Hapo ndipo unazidi kupotea! Unataka nani aseme sheria zimeshindwa wakati idadi ya wanafunzi wanaotiwa mimba wakiwa shule imepaakwa kiwango cha kutisha. Akili yako inakutuma ngono inaweza kuzuiwa na sheria? Ngoja tuone huyo msimamizi wa sheria atakavyozuia ngono!
 
ongeza maradufu hyo addiction yako ya kupinga pinga kila kitu itakusaidia kupunguza ujinga ulio nao.
Mkikosolewa kwa hoja haraka haraka mnakimbilia kwenye kupingwa! Nani atawapinga, endeleeni kuzuia wanafunzi wasiendelee na masomo ili wazidi kuwa wajinga maana ni furaha yenu taifa likiwa na wajinga wengi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naona Magu yuko upande sahihi yeye hataki ngono iendekezwe ila hao wengine na upuuzi wao ambao wao watoto wao hajazaa mashuleni wanataka wa wenzao wazae mashuleni
 
Wewe kama unafurahia na unapenda watoto wajazwe mimba mashuleni na waendelee kusoma zaa wa kwako. Ila wa wenzako tutaendelea kuwaambia wasipate mimba wakiwa shule kwa kuwa kuna madhara mengi sana ikiwemo na kufukuzwa shule. There are consequences in every stupid decision wanachukua.
 
Huyo binti kwenye picha hawezi kufaulu vizuri anasoma ili maradi tu atimize wajibu ili apate cheti chenye miswaki mingi ambacho hakitamfikisha popote. Tusishangulie kusoma tu! Ili ufaulu vizuri, unapaswa kuweka mkazo kwenye kile unachosoma, kulea mtoto huku unasoma kunapunguza concetration ya kwenye masomo. Hivyo basi ukipata mimba halafu urudi shule sidhani kama utafaulu vizuri na ukapata cheti kitakacho kuwezesha kuendelea na ngazi zingine za juu za masomo. Utapoteza muda, nguvu na mali zako. Kwani wakivumilia hiyo miaka ili wamalize masomo yao kuna kitu wanapungukiwa? Naungana na rais, wanaopata mimba wasiendelee na masomo, walee watoto na baadae waende veta kwa masomo ya ufundi tu
Halafu na bado anatakiwa kuhudhuria darasa Clinic huko nako waalimu wa elimu ya uzazi wanamsubiri anatakiwa kwa mujibu wa kanuni kuhudhuria bila kukosa.
 
Back
Top Bottom