Magufuli wewe ni mzazi unayejitambua

Magufuli wewe ni mzazi unayejitambua

Hata dada yangu alipitia uzoefu huu na leo anamshukuru Mungu kwa wema wa waalimu waliomsaidia kumaliza masomo. Leo ni mwenye furaha sana na anamshangaa sana bwana mkubwa! Udhalimu una mwisho na mwisho huo uko karibu kuliko ilivyokuwa jana.

Kwako wewe na unaofanana nao ni udhalimu kuipinga ngono ya utotoni ila ni uungwana na hekima kuitetea ngono na mimba za utotoni?

Dada anafurahia pia mimba yake ya utotoni na namna alivyoipata? tueleze alibakwa? alidanganywa kwa chips mayai na kokakola au alikuwa anafanya majaribio? ili tushawishike kukiona anachofurahia.
 
Mkuu nusu hela, ulitaka rais asimame majukwaani atangaze kuwa ngono kwa wanafunzi ni ruksa? Wewe binafsi ungemuelewaje? Dunia ingemuelewaje? Na kama akitangaza kuwa ngono kwa wanafunzi ni ruksa, madhara yake ni makubwa kuliko hili la kuzuia. Tafakari kidogo mkuu
baelezee baelewe
 
View attachment 530269

--- Kama umasikini ndio chanzo cha kupata mimba kwa wanafunzi wa kike, kwanini shule nzima wasiwe na mimba? Kama umbali wote wanatoka mbali na wanaishi katika mazingira yanayofanana.

--- Eti wanadai ni haki ya mtu kupata elimu kwa maana kuwa na elimu ndio silaha ya kwanza ya kupambana na umasikini. Hiyo ni sawa. Lakini haki ni lazima iendane na wajibu (to get your Rights you should behave responsibly)

--- Wengine wanadai eti serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa maadili mabovu kwa maana wao ndio wametufikisha hapa kwa miaka 50 ya utawala wao. Ninasema hapana. Serikali haiwezi kuja nyumbani kwako ikakwambia baba na mama flani sasa zimeni TV ili mtoto wenu aache kuangalia cartoons afanye homework yake. Huo ni mfano tu juu gani ya wazazi wanapaswa kutimiza wajibu wao katika maadili ya watoto.

Huku uswahilini ninapokaa sio jambo la kushangaza kukutana na mtoto wa kike darasa hata la 3 usiku wa 4 eti ametoka kwende kibanda kuangalia movie. Hivi binti kama huyu akibakwa na kupata mimba (achilia mbali magonjwa mengine) italaumiwa serikali? Let's be serious guys.

JPM stay focused. Wewe ni mazazi unayejitambua sana.

Mwenye macho na asome.

Nimemaliza.

View attachment 530265
 
Huyo binti kwenye picha hawezi kufaulu vizuri anasoma ili maradi tu atimize wajibu ili apate cheti chenye miswaki mingi ambacho hakitamfikisha popote. Tusishangulie kusoma tu! Ili ufaulu vizuri, unapaswa kuweka mkazo kwenye kile unachosoma, kulea mtoto huku unasoma kunapunguza concetration ya kwenye masomo. Hivyo basi ukipata mimba halafu urudi shule sidhani kama utafaulu vizuri na ukapata cheti kitakacho kuwezesha kuendelea na ngazi zingine za juu za masomo. Utapoteza muda, nguvu na mali zako. Kwani wakivumilia hiyo miaka ili wamalize masomo yao kuna kitu wanapungukiwa? Naungana na rais, wanaopata mimba wasiendelee na masomo, walee watoto na baadae waende veta kwa masomo ya ufundi tu

Mkuu wapo wanaopata mimba na wanapiga one kama vile hawajawai ku-do! Ni uamuzi tu, usikariri kila kitu. siungi mkono teen mothers, ila suluhu sio kuwaadhibu, badala yake ni vema tungejua mzizi wa tatizo ni upi!
 
Naam wajinga wengi nchini ndiyo mtaji mkubwa wa hawa wahuni na mafisadi. Hivyo wanapoona kuna namna ya kuzalisha wajinga wengi nchini kwa faida ya chama chao cha wahuni basi huwa hawasiti kufanya hivyo.

Mkikosolewa kwa hoja haraka haraka mnakimbilia kwenye kupingwa! Nani atawapinga, endeleeni kuzuia wanafunzi wasiendelee na masomo ili wazidi kuwa wajinga maana ni furaha yenu taifa likiwa na wajinga wengi!
 
View attachment 530269

--- Kama umasikini ndio chanzo cha kupata mimba kwa wanafunzi wa kike, kwanini shule nzima wasiwe na mimba? Kama umbali wote wanatoka mbali na wanaishi katika mazingira yanayofanana.

--- Eti wanadai ni haki ya mtu kupata elimu kwa maana kuwa na elimu ndio silaha ya kwanza ya kupambana na umasikini. Hiyo ni sawa. Lakini haki ni lazima iendane na wajibu (to get your Rights you should behave responsibly)

--- Wengine wanadai eti serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa maadili mabovu kwa maana wao ndio wametufikisha hapa kwa miaka 50 ya utawala wao. Ninasema hapana. Serikali haiwezi kuja nyumbani kwako ikakwambia baba na mama flani sasa zimeni TV ili mtoto wenu aache kuangalia cartoons afanye homework yake. Huo ni mfano tu juu gani ya wazazi wanapaswa kutimiza wajibu wao katika maadili ya watoto.

Huku uswahilini ninapokaa sio jambo la kushangaza kukutana na mtoto wa kike darasa hata la 3 usiku wa 4 eti ametoka kwende kibanda kuangalia movie. Hivi binti kama huyu akibakwa na kupata mimba (achilia mbali magonjwa mengine) italaumiwa serikali? Let's be serious guys.

JPM stay focused. Wewe ni mazazi unayejitambua sana.

Mwenye macho na asome.

Nimemaliza.

View attachment 530265
Hii itakuwa Elimu ya Watu wazima mkuu
 
Siasa na Utawala
Profesa Rwekaza Sympho Mukandala anazungumzia kigezo muhimu cha uongozi, ambacho ni je wananchi wanafuraha?

Prof. Mukandala anasema haitoshi baba wa nyumba kuleta nyama, samaki na chakula kila siku nyumbani lakini familia yake inaishi bila furaha.

Kipimo cha kutengeneza miundombinu lukuki na kulazimisha watu waridhike wakati wananchi hawana furaha kutokana na ukata kuwepo ktk shughuli zao za kujiingizia kipato huku wakiwa hawana furaha kwa kukosa pesa na umasikini unaosababishwa na sera za kiuchumi za serikali kukazania Maendeleo ya Vitu na kusahau kabisa Maendeleo ya Watu.
Source :
25 Nov 2018
African Intellectuals
Hali ya Uchumi na Siasa Nchini Tanzania Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano: "Tunatoka wapi, Tuko wapi na Tunakwenda wapi"
 
Huyo binti kwenye picha hawezi kufaulu vizuri anasoma ili maradi tu atimize wajibu ili apate cheti chenye miswaki mingi ambacho hakitamfikisha popote. Tusishangulie kusoma tu! Ili ufaulu vizuri, unapaswa kuweka mkazo kwenye kile unachosoma, kulea mtoto huku unasoma kunapunguza concetration ya kwenye masomo. Hivyo basi ukipata mimba halafu urudi shule sidhani kama utafaulu vizuri na ukapata cheti kitakacho kuwezesha kuendelea na ngazi zingine za juu za masomo. Utapoteza muda, nguvu na mali zako. Kwani wakivumilia hiyo miaka ili wamalize masomo yao kuna kitu wanapungukiwa? Naungana na rais, wanaopata mimba wasiendelee na masomo, walee watoto na baadae waende veta kwa masomo ya ufundi tu
Huo ni mtazamo wako. Ila uko hasi. Jipeleleze ila pia fanya research uone wangapi walizaa na wakarudi shule na kufaulu vyema kabisa
 
Back
Top Bottom